DPP, TAKUKURU na Polisi: Wasikilizeni CHADEMA. Kuna jinai kubwa imetendeka

DPP, TAKUKURU na Polisi: Wasikilizeni CHADEMA. Kuna jinai kubwa imetendeka

Majina yamepelekwa na Halima Mdee ambae ndio mwenyekiti wa wanawake wa CHADEMA

Na waliwahi kukaa na wa walikubaliana kuhusu kupeleka majina NEC nadhani Kuna sehemu walipishana kwenye Nani awepo na Nani asiwepo hapo ndio shida imekuja
 
Ndugu usichokijua ni kwamba DPP,TAKUKURU pamoja na Polisi tayari walishawekwa mfukoni mwa shati!
87659087.jpg
 
Wewe acha uongo, mlalamikaji ndiye anayetakiwa apeleke lalamiko hilo kwenye hivyo vyombo vya uchunguzi sio kuwasemea.

Wabunge wale wametamka wana baraka zote za Chadema na Mwenyekiti wa chama.

Chukueni hatua kwa Mh.Freeman Aikael Mbowe kama mnazo guts hizo
 
Hii Scandal ni kubwa sana, Tanzania haiwezi kuheshimiwa tena; GOVERMENT kutengeneza FRAUD; sasa tumekuwa LAWLESS STATE! TUTAAMINI Document ipi ya SERIKALI?

Hii inatoa imani kabisa, unforgivable, UNFORGIVABLE, must be punished!!
kwa Tanzania hii sio scandal,ila kwa nchi za maana hii ni skenda ya karne
 
Wewe acha uongo, mlalamikaji ndiye anayetakiwa apeleke lalamiko hilo kwenye hivyo vyombo vya uchunguzi sio kuwasemea.

Wabunge wale wametamka wana baraka zote za Chadema na Mwenyekiti wa chama.

Chukueni hatua kwa Mh.Freeman Aikael Mbowe kama mnazo guts hizo
unajua jinai wewe?hebu kachome shule hapo halafu wakipeleka polisi useme mbona hakuna aliyepeleka malalamiko
 
Ndugu usichokijua ni kwamba DPP,TAKUKURU pamoja na Polisi tayari walishawekwa mfukoni mwa shati!View attachment 1634410
Behaviorist you are now crossing the red-line for posting this figurative cartoon which represents bashing, trolling and provocative, you may eventually pay the price for entertaining these kind of unacceptable ridicule. Your ID is on eavedrop track to account the assault
 
Wewe acha uongo, mlalamikaji ndiye anayetakiwa apeleke lalamiko hilo kwenye hivyo vyombo vya uchunguzi sio kuwasemea.

Wabunge wale wametamka wana baraka zote za Chadema na Mwenyekiti wa chama.

Chukueni hatua kwa Mh.Freeman Aikael Mbowe kama mnazo guts hizo
Unamuita mwenzio muongo wakati wewe unaiamini kauli uliyoisikia toka kwa Mdee simply because aliitolea bungeni, kwani bungeni hawawezi kudanganya?

Sasa wameitwa na chama, Ijumaa tarehe 27 wakatoe utetezi wao, mbivu na mbichi zitajulikana hapo, na ikithibitika vinginevyo ni kufukuzwa.
 
Nasikitika kwamba kwa staili ya utawala tulionao sasa, na kasi kubwa ya kuvunjwa katiba, sheria na taratibu za demokrasia na haki katika nchi hii, hilo unalosema/pendekeza hutaona likifanyika!
 
Kama huwajui wanasiasa wa bongo, yaani 19people zikaape bila kujadiliwa so angeenda yoyote na ingezuka vita pale bungeni.
Hapa tutapigwa siasa mpaka jambo litulie watu waendeleee kula mema ya nchi bila kuwakumbuka wale wanaosota rumande kwa kesi zakubambikizwa za uchaguzi
 
Hii Scandal ni kubwa sana, Tanzania haiwezi kuheshimiwa tena; GOVERMENT kutengeneza FRAUD; sasa tumekuwa LAWLESS STATE! TUTAAMINI Document ipi ya SERIKALI?

Hii inatoa imani kabisa, unforgivable, UNFORGIVABLE, must be punished!!
This is the naked truth, bahati mbaya hatuna vyombo vya sheria vya kuaminika vya kutoa maamuzi kwa sasa, suala kama hilo kumpelelekea Sirro alifanyie uchunguzi ni utani.
 
Yaani unaweza ukadhani unaangalia show ya mashabiki wa Trump wanaokesha wakiamini atapindua na kubaki Ikulu.
 
Umeandika vizuri ila kwa speed ya ajabu.

Twende kwenye uharisia wa mfumo wetu huu huu mbovu, kuna wafungwa wa kisiasa watano na juzi wametolewa mmojawapo amekula kiapo jana, tuhoji hapo kwenye kuwatoa na haraka kapelekwa kula kiapo, kuna nini kimejificha, je jinai haikuanzia hapo?

Kuna msemo unasema "Mfumo ukiharibika hata waliomo wameharibika" serikali inajinasibu kufanya uchaguzi mzuri toka kuwepo kwa taifa la Tanganyika kama si Tanzania, ila wale wanaotakiwa kuwepo siyo waliopo ila wanalazimisha kuwekwa wasiokuwepo kwenye ubunge.

Hakuna msimamizi wa sheria za nchi atakayekuwa tayari kusikiliza kilio cha mwananchi huko nje 'eti' katiba na sheria imevunjwa na muhimili wakati kila mtu ana hofu na nafasi yake.
Huenda TAKUKURU walijulishwa kabla nini kinaendelea, hivyo hawawezi kuchukua hatua.
 
Kuna jinai kubwa imetendeka.

Kuna uvunjaji mkubwa wa Katiba na Sheria za nchi umetokea. Mhusika lazima abainishwe na achukuliwe hatua kali za kisheria. Mambo yako hivi: CHADEMA wamesema na wanaendelea kusema kuwa hawakuwasilisha Orodha ya Wabunge wa Viti Maalum NEC. Hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye ndiye mhusika wa kupeleka majina na mjazaji wa Fomu za kisheria.

Katiba imevunjwa, sheria zimevunjwa. Orodha haikupelekwa. Orodha aliyopewa Spika, kuiamini na kuwaapisha jana ameitoa wapi? Anzeni na Spika. Kama ameipata Orodha kutokea NEC, NEC wamepewa na nani? Nendeni na NEC. Halafu, wote 19 walioapishwa jana wahojiwe na waeleze, pamoja na mambo mengine, waliambiwa na nani kuwa wameteuliwa kuwa wabunge. Waseme waliambiwa kwa njia gani.

Hapa kuna mambo ya pesa za umma. Kuna mambo ya katiba na sheria. Hapa kuna mambo ya jinai kubwa. DPP, TAKUKURU na Polisi, wasaidieni watanzania. Lindeni pesa zao, katiba yao na sheria zao. Mtaheshimiwa na kuthaminiwa. Wakati ni huu!

Mwaka 2020 kulikuwa na uchafuzi mkuu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Huu ndio ukweli...je wahusika wapo tayari kuyafanyia kazi hayo ulioshauri?hayo yakitendeka mbivu na mbichi zitajulikana
 
Hapa kuna mambo ya pesa za umma. Kuna mambo ya katiba na sheria. Hapa kuna mambo ya jinai kubwa. DPP, TAKUKURU na Polisi, wasaidieni watanzania. Lindeni pesa zao, katiba yao na sheria zao. Mtaheshimiwa na kuthaminiwa. Wakati ni huu!

Tatizo Magufuli hajui kitu, ila kujitia kujua ndio kwingi. Watoto wa mjini wanampiga sana kodi zetu.
CCM mlitoa wapi huyu kiumbe.
 
Hii Scandal ni kubwa sana, Tanzania haiwezi kuheshimiwa tena; GOVERMENT kutengeneza FRAUD; sasa tumekuwa LAWLESS STATE! TUTAAMINI Document ipi ya SERIKALI?

Hii inatoa imani kabisa, unforgivable, UNFORGIVABLE, must be punished!!
Tatizo lako umesikiliza upande mmoja.Hakuna sheria imekiukwa akina Halima and Co wanabaraka za chama.
Kwa taarifa za uhakika subirini 27/11 mtashangaa
 
Chadema haiwezi kubeba lawama kwenye hili , ilishaweka wazi kwamba hawakuteua wala kupeleka majina Tume , na Mahera alikiri hilo , sasa huu ujinga uliofanywa na ndugai na mfumo wao umefanyika kwa sababu hakuna kiongozi yeyote wa awamu ya 5 mwenye aibu
Mnyika ametoa ufafanuzi mzuri sana.

Hapo kwenye form no. 8(d) inayotakiwa kuwasilishwa bungeni ikiwa na jina la mhusika na Mnyika amesema bado anazo form zote, hii pekee inaonesha nchi inavyoendeshwa kiajabu siku hizi.

Taasisi zote hazifuati sheria tena, wanafanya mambo ya ajabu.
 
Back
Top Bottom