Uchaguzi 2020 Dr. Bashiru: Kama Membe anasema tatizo ni Urais agombee kwa chama chochote tukutane uwanjani

Uchaguzi 2020 Dr. Bashiru: Kama Membe anasema tatizo ni Urais agombee kwa chama chochote tukutane uwanjani

Habari Jf!
Kuna nini kwani kimetokea mbona kila kona nasikia Membe Membe???

Inamaana ss CHADEMA mshampata shujaa wenu naye ni Benard Membe ,maana kila nikipita katika kurasa za Jf naona jina la Membe limepambwa vizuri kwa mbwembwe nyingi na akibatizwa majina makubwa kama mwanaharakati,mwanadiplomasia wengine washampa cheo cha ukamanda.

Ila mm nawaambia wapinzani neno moja tu kwamba Membe hafai hata kwa kurumangia,nimalizie tu na kwa kusema kidagaa kilichomponza Ndobe ndio kitakachomponza kambare.

Wapo wanaongoja tamko rasmi la Membe kwamba atafanya nn baada ya kufukuzwa CCM ,wengine washaanza kumtamani Benard Membe ili kujihimarisha kuelekea uchaguzi mkuu .

Fanyeni mipango yenu yote ila CCM itatawala mpaka miaka 100 ijayo hakuna wakuiangusha na waakikishia,upinzani ulishakufa .
Umeuliza swali, badala ya kusubiri ujibiwe, umejijibu mwenyewe na kuweka hitimisho kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NOT THAT MUCH SIMPLE, AMEJENGA NGOME YAKE CCM, IWEJE AENDE KWINGINE..... AMEWEKEZA CCM, KWINGINE ATAPATA KURA ZA KUOKOTEZA KUMUINUA, HE BELIEVES IN HIGHER NUMBER OF VOTES FROM CCM.....WAPINZANI WAKIFANYIWA YA SERIKALI ZA MITAA? KUNA FACTORS NYINGI SANA IN THIS ERA, SHALLOW ANALYSIS OF ISSUES!

Ndo wameshamtimua sasa.

CCM si baba yake wala mama yake.

Kama kweli kaijenga ngome yake huko CCM si aondoke nayo tu...

Tena hiyo ndo itakuwa fursa murua kabisa ya kukibomoa hicho chama.

Aondoke tu na hao watu wake.

So your so called analysis is fatuous.
 
Sawa nimekuelewa ila nakazia Kama ambavyo magufuli hana haja ya kusubiri 2025 pia membe naye hana haja ya kusubiri 2025, bushiri alitakiwa kuacha mchakato wa kuchuja mgombea ndani ya chama, siyo kusema membe akagombee chama chochote make hata magufuli naye anaweza kwenda kugombea chama chochote!

Okay, wameshamtimua sasa. Wewe na yeye mtafanya nini zaidi ya kunung’unika mitandaoni?

Hamjakatazwa na mtu kugombea huo urais.

Nendeni kwingine mkagombee au anzisheni chama chenu halafu mgombee.

Msing’ang’anie ambako hamtakiwi.

Ila, lengo lenu sidhani kama ni kugombea urais.

Lengo lenu ni kuleta vurugu tu ndani ya chama.
 
Ndo wameshamtimua sasa.

CCM si baba yake wala mama yake.

Kama kweli kaijenga ngome yake huko CCM si aondoke nayo tu...

Tena hiyo ndo itakuwa fursa murua kabisa ya kukibomoa hicho chama.

Aondoke tu na hao watu wake.

So your so called analysis is fatuous.
BADO HOJA MOJA HUJAIJIBU! YAKITOKEA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA UNASEMAJE?
ONE OF THE SHALLOW MINDS ON JF! CRAMMING OF BOMBASTIC WORDS! THIS IS SHALLOW MINDEDNESS!
 
BADO HOJA MOJA HUJAIJIBU! YAKITOKEA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA UNASEMAJE?
ONE OF THE SHALLOW MINDS ON JF! CRAMMING OF BOMBASTIC WORDS! THIS IS SHALLOW MINDEDNESS!

🤣🤣🤣🤣

Andika tu kwa Kiswahili aisee.

Usilazimishe lugha usiyo na uwezo nayo kivile.

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hayo maneno angetakiwa kusema tukutane kwenye mkutano mkuu wa kuchagua mgombea wa ccm 2020, kwanini mmempora haki yake?
Traditionally wanamwachiaga incumbent second term, Membe alitaka Kula ubwabwa bila kunawa mikono.. nadhani sio Sawa na ni kukosa heshima na kujiona Bora zaidi...
 
Kabisa.

Si lazima agombee kupitia CCM.

Kwanza keshawahi kugombea kupitia CCM na akashindwa.

Aende TADEA akagombee huko kama kweli nia yake ni kugombea urais na si ajenda zingine.
Membe hana nguvu hizo. Kazi aliyoifanya ndio anataka aitumie kumbeba
 
CCM ni membe 2020 mtake msitake.

Hiyo inaitwa niguse unuke!!
 
Kaka masahihisho kidogo hapo, ni Independent Candidate siyo Private Candidate.

Semantics.
Private Candidate na Independent Candidate tofauti yake nini?

Mimi naona zinatumika interchangeably.

Soma "Court of Appeal and Independence of The Judiciary" pp 89.

Kesi ya Mtikila imetajwa kuhusiana na Private Candidate.

Law and Justice in Tanzania
 
Unajuaje Membe anaafikiana kisiasa na chama chochote kilichopo?

Aende kuokota chama chochote mradi agombee urais tu?

Wamruhusu agombee kama mgombea binafsi, halafu waseme agombee.

Sent using Jamii Forums mobile app
Katiba inaruhusu mgombea binafsi? Kama sio, kwanini hakupigania kubadili hali hiyo wakati ana nguvu? Vinginevyo atumie njia ile ile inayotumika kwa kila anayegombea, halafu apate huo Urais.
 
Traditionally wanamwachiaga incumbent second term, Membe alitaka Kula ubwabwa bila kunawa mikono.. nadhani sio Sawa na ni kukosa heshima na kujiona Bora zaidi...
Angeachwa angeleta kipindupindu
 
Membe anaweza akagombea mwaka huu kama shida yake ni kugombea tu urais.

Hakuna aliyemkataza kabisa kuwa asigombee mwaka huu.

Na kusema siyo lazima agombee mwaka huu si kumkataza asigombee. Ni kusema ukweli tu.

Au ni lazima agombee mwaka huu?
Hata Magufuli si lazima agombee mwaka huu.

Ulazima si tatizo, tatizo ni, je, ni haki yake ya kikatiba?
 
Uwanja gani hasa?. Huu wa kuongezea herufi "a^ kwenye neno Sinza ili iwe Sinzaa kwa minajili ya kuengua mpinzani? Wenye PoliceCCM? Wenye NEC ya mwenyewe? Yenye Wakurugenzi wasimamizi wa uchaguzi waliopewa V8 GXR na Serikali??? Which exactly playing ground are you talking about??.
Exactly!

Just as simple as that!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katiba inaruhusu mgombea binafsi? Kama sio, kwanini hakupigania kubadili hali hiyo wakati ana nguvu? Vinginevyo atumie njia ile ile inayotumika kwa kila anayegombea, halafu apate huo Urais.
Simzungumzii mtu, nazungumzia mfumo. Hili jambo ni zaidi ya Membe, ni mfumo mzima una makosa.
 
Kwanini unamlazimisha aende chama fulani? Kama hakioendi?

Sijamlazimisha aende chama kingine.

Hiyo ni option tu aliyonayo.

Pia, ana option ya kubaki bila chama, kama nilivyo mimi.

Option zilizopo ni kadhaa. Siyo lazima awe CCM.

Na kama anaona ni lazima awe CCM, basi ni akubaliane na taratibu, tamaduni za chama, na kadhalika.

Kulazimisha awepo tu CCM kana kwamba hakuna kwingineko anakoweza kwenda ni wehu.
 
Traditionally wanamwachiaga incumbent second term, Membe alitaka Kula ubwabwa bila kunawa mikono.. nadhani sio Sawa na ni kukosa heshima na kujiona Bora zaidi...
Which overrides the other, Katiba ya CCM or utamaduni wa kuachiana?
 
Hata Magufuli si lazima agombee mwaka huu.

Ulazima si tatizo, tatizo ni, je, ni haki yake ya kikatiba?

Naam, si lazima agombee.

Lakini chama kina taratibu na tamaduni zake. Rais aliyepo madarakani huwa anagombea tena muhula wa pili bila pingamizi.

Huyo Membe lengo lake ni kuleta mvurugano tu kwenye chama. Sidhani kama anataka kugombea kweli na kushinda.

Wenyewe wamemtimua. Wana haki ya kufanya hivyo.

Na kama yeye lengo lake kweli ni kugombea tu urais, basi sasa hana kizuizi tena.
 
Back
Top Bottom