DR Congo imewanyonga Majambazi 102, Tanzania tunacheka na Panya Road, Wadudu na Magenge Mengine ya Wahalifu

DR Congo imewanyonga Majambazi 102, Tanzania tunacheka na Panya Road, Wadudu na Magenge Mengine ya Wahalifu

Serikali ya Congo imewaua wanaume wapatao 102 kwa njia ya kunyongwa wiki iliyopita, na wengine 70 wanatarajiwa kuuawa. Waziri wa sheria wa nchi hiyo alisema Jumapili katika taarifa kwa Shirika la Habari la Associated Press.

Waziri alisema wanaume hao, wenye umri wa miaka 18 hadi 35, walikuwa majambazi wenye silaha na "wahuni wa mijini," wanaojulikana kama Kulunas, waliouawa katika gereza la Angenga, kaskazini-magharibi mwa DrCongo.

Amesema 45 waliuawa mwishoni mwa Desemba, na wengine 57 waliuawa ndani ya saa 48 zilizopita.

Waziri wa Sheria Constant Mutamba, ambaye anasimamia mauaji hayo, alisema Jumapili jioni kuwa "kundi la tatu litanyongwa, kwa hivyo makundi mawili ya kwanza tayari yameshapewa adhabu ya kifo.
Si bora huko, huku unatekwa na kumalizwa na kutupwa.., hawana muda wa kupoteza mahakamani
 
Wazungu watetea haki za Binadamu bado hawajatia neno huko?
Au mpaka iwe North Korea,Iran au Russia imenyonga watu ndio watokwe povu?
 
Nyie si watukutu, hamsikiii nyie jeuri kiburi...basi dawa yenu ni kuwaondoa duniani...ndiyo maamuzi hayo

Ova
 
wamewanyonga au wamewapiga risasi?? mbona sielewi???
 
Katika kitu nakipenda duniani ni kuona binadamu muuaji akifa huku anajiona huyu mwamba mutamba ambae ni waziri wa sheria kutoka congo anafaa kuwa raisi kabisa sababu kafanya kazi nzuri sana napenda sana kuona binadamu anaeibia na kuua wenzake akifa kwa kuuwawa huwa siku hiyo napiga sana bia halafu kinachoshangaza Hawa wahuni wengine ni wanyarwanda aisee congo ilichezewa sana Hawa vijana video zao wakifanya uhalifu sio za kuangalia mara mbili mbili anaewatetea atakua Hana akili timamu dawa ya watu kama Hawa Shaba na kunyonga
 
Katika kitu nakipenda duniani ni kuona binadamu muuaji akifa huku anajiona huyu mwamba mutamba kutoka congo anafaa kuwa raisi kabisa sababu kafanya kazi nzuri sana napenda sana kuona binadamu anaeibia na kuua wenzake akifa k'kwa kuuwawa huwa siku hiyo napiga sana bia halafu kinachoshangaza Hawa wahuni wengine ni wanyarwanda aisee congo ilichezewa sana Hawa vijana video zao wakifanya uhalifu sio za kuangalia mara mbili mbili anaewatetea atakua Hana akili timamu dawa ya watu kama Hawa Shaba na kunyonga
Duuh we noma!
 
Katika kitu nakipenda duniani ni kuona binadamu muuaji akifa huku anajiona huyu mwamba mutamba ambae ni waziri wa sheria kutoka congo anafaa kuwa raisi kabisa sababu kafanya kazi nzuri sana napenda sana kuona binadamu anaeibia na kuua wenzake akifa k'kwa kuuwawa huwa siku hiyo napiga sana bia halafu kinachoshangaza Hawa wahuni wengine ni wanyarwanda aisee congo ilichezewa sana Hawa vijana video zao wakifanya uhalifu sio za kuangalia mara mbili mbili anaewatetea atakua Hana akili timamu dawa ya watu kama Hawa Shaba na kunyonga
Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom