DR Congo imewanyonga Majambazi 102, Tanzania tunacheka na Panya Road, Wadudu na Magenge Mengine ya Wahalifu

DR Congo imewanyonga Majambazi 102, Tanzania tunacheka na Panya Road, Wadudu na Magenge Mengine ya Wahalifu

Serikali ya Congo imewaua wanaume wapatao 102 kwa njia ya kunyongwa wiki iliyopita, na wengine 70 wanatarajiwa kuuawa. Waziri wa sheria wa nchi hiyo alisema Jumapili katika taarifa kwa Shirika la Habari la Associated Press.

Waziri alisema wanaume hao, wenye umri wa miaka 18 hadi 35, walikuwa majambazi wenye silaha na "wahuni wa mijini," wanaojulikana kama Kulunas, waliouawa katika gereza la Angenga, kaskazini-magharibi mwa DrCongo.

Amesema 45 waliuawa mwishoni mwa Desemba, na wengine 57 waliuawa ndani ya saa 48 zilizopita.

Waziri wa Sheria Constant Mutamba, ambaye anasimamia mauaji hayo, alisema Jumapili jioni kuwa "kundi la tatu litanyongwa, kwa hivyo makundi mawili ya kwanza tayari yameshapewa adhabu ya kifo.
uku kwetu panyalodi tunawachekea tu
 
Tunazungumzia wanaoua watu na kupora Mali,hao wengine Wana adhabu zao
Kwahio wala Rushwa, Rasilimali za Nchi huko sio Kupora Mali ? Au unadhani kufuja kodi za Mwananchi hivyo wengi kukosa Basic needs na kufa kwa kukosa Huduma huko sio Kuua ? Kwa taarifa yako wengine hao vibaka wameingia huko baada ya kukosa alternative inayoeleweka.
 
Back
Top Bottom