Dr. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji wa NECTA! "It's Time To Go!.

Nashukuru kwa wewe kuweweka nyama za kutosha kamanda, ndio maana nami naungana na wewe kuwa hao hawajui kusoma kwasababu walimu wao pamoja na wanafunzi hawana vitendea kazi wala motisha, so hata ufundishaji unakua wa kukomoana
 
Mkuu Matola, binadamu wengi ni wagumu kuona far distance, wengi wanaangalia tuu matokeo, sio wengi wanaozama ndani zaidi kwenye the motive behind, na kwa kawaidfa binadamu huwa tuu wabishi hakuna mfano!, hata Masiya alikataliwa kwao na wakamsulubisha!. Endeleeni tuu kuwa wabishi, mtajifunza na matokeo!.

Wenye kumbukumbu ya maneno yangu haya nawaombeni sana myaweke kwenye kumbukumbu!
"UTUNGAJI MITIHANI WA NECTA NA USAHIHISHAJI, UKO SET NIN SUCH A WAY, KUJENGA MATABAKA YA WALIONACHO NA WASIONACHO!, WENYE NACHO, WANAONGEZEWA, WASIO NACHO WANANYANGWANYWA HICHO KIDOGO WALICHO NACHO!, IN A LONG WAY, WALE WASIONACHO WAKISHA KUJA KUJIGUNDUA KUMBE NI KUNDI FULANI LA JAMII, THEN WATAFIKIA KIPINDI, WATAWANYANGANYA WALE WALIONACHO ILI AMA NA WAO WAPATE, AUY WATATEKETEZA MALI ZA WALIONACHO ILI TUKOSE WOTE!". Mwisho wa kunukuu!.

Pasco.
 
Kuna mambo mengi sana yanayohusiana na ufaulu wa wanafunzi. Mfumo wenyewe, ari ya wanafunzi, vitabu vya kiada na ziada, ari ya walimu etc
 
 
Last edited by a moderator:
This is total nonsense, si kwamba wengine tunaishi kwenye space ili tusijuwe tatizo ni nini, je unaelewa hoja ya Mbatia ilikuwa ni nini?

Na unaweza kunieleza sisi tuliosoma miaka ya 90 0 level mitihani ilikuwa inatungwa na kusahihishwa wapi? hivi ingekuwaje kama mpaka leo mitihani ingekuwa inatoka Uingereza kama kipindi Baba zetu wanasoma?
 

NECTA kazi yake ni kutunga mitihani na kuisahihisha, sio kufundisha wanafunzi madarasani. Kwa hiyo Dr. Ndalichako na NECTA wanahusikaje na wanafunzi kufeli?
 
Elimu ya Tanzania bado imekaa katika mfumo wa kukomaa sana na kujibana sana ili utoke...sasa nadhani kwa hili watoto wengi wa kizazi hiki na waliofeli wameshindwa kulimudu
 
Hizi simu na music na head/erphone yaani mtu ataelewa nini....kutwa ni kuhangaika na mambo ambayo yana mchango mdogo sana kwenye elimu yetu,....na hata kwa sisi wazee
 
Mkuu Fidelity, sijutii uamuzi wangu kusomesha vijana wangu shule za kata, bali naumizwana kijana wangu kichwa wa hisabati, kupata daraja C.

Mwaka juzi, binti yangu last but one, aliomba kujiunga St. Marian Girls nini nikamgomea wife akawasha moto, hadi kumpeleka kufanya usahili, matokeo alikosa, alilia sana baada ya kuambia cut off point ni makisi 150/200. Akamthibitishia mama yake kuwa amedhulumiwa, hawezi kukosa average ya 75 kwa mitihani mitatu waliofanya!, binti analia tuu, hatimaye nikakubali, mimi, binti na mama, hao Bagamoyo kwa mkuu wa shule, tuki demand kuona matokeo halisi ya mwanetu!.

Kwanza tulikataliwa, nilipoeleza sababu nyeti nilizozisikia kuhusu selection ya St. Marian, Mkuu wa shule akanikubalia, ikaitishwa file, narking scheme na pepa za mwanangu, wamefanya pepa 4. hesabu, sayansi, Kiingereza na maarifa!. Kila pepa maswali 50 na kila swali makisi 1. Cut of point ni makisi 150/200. Binti kapiga 42, 32, 38 na 36. Total ni zaidi ya 150/200 hivyo ni over and above ile cut off point yao, kuuliza sasa kwa nini hakuchaguliwa, nikaletewa hadithi!.

Kufuatia matokeo haya mabaya, wale wazazi tunao waaminia wenetu, hatuwezi kukubali hili likapita hivi hivi tuu!.
Mimi ni kama Tomaso, sikubali mpaka nione pepa moja tuu, ya hesanu ya kijana wangu!. Kiukweli, pamoja na mengine yote, " The games that NECTA plays on poor people!, its very dangerous gamea!".
Pasco.
 
Kumbe Pasco ni miongoni mwa wale wanaolala wakiwaza kuandamana kwenda NECTA kumng'oa Ndalichako? Halafu wengine wanafuataga mkumbo tu kusema Ndalichako, ukiwauliza hawajui ni mwanaume au mwanamke, ili mradi tu wamekaririshwa na wakubwa zao "tukamng'oe Ndalichako NECTA"
 
Ndugu Mkodoleaji, ukikodoa sawa sawa utaona maelezo yako hapo kwenye RED na mfano ulioutoa vinahitilafiana!! Unadhani mitihani ingetungwa nje ya Muhtasari hayo maandamano yangezuilika???

NECTA wanapotunga mitihani, lazima wazingatie mambo mengi. waelewe kuwa kuna shule hazina walimu wakutosha, maabara, nk...... lazima kuwe na 25% ya maswali mepesi sana, 50% ya maswali ya kati na 25% ya maswali magumu. dk. joyce lazima ajiuzulu kwa sababu ofisi yake ilipotunga mitihani haikuzingatia haya yote.
La hasha. Sidhani kama kuna swali lilitoka nje ya Muhtasari na kama kuna mwenye ushahidi aweke humu. Pili unanishangaza unapotaka eti mitihani itungwe toka kwenye kitabgu/vitabu fulani...Nadhani cha msingi ni kuzingatia mada zilizopo kwenye muhtasari na maarifa anayotakiwa kuwa nayo mtahiniwa wa level hiyo. issue sio kitabu!!
 
Leo nilikuwa ninasoma gazeti moja la serikali, waalimu wakuu wa baadhi ya shule (Feza Boys, Marian Girls n.k) wamelalamika kuwa mfumo wa utunzi wa mitihani umekuwa tofauti na miaka ya nyuma ikiwemo mwaka jana. Pia wamesema hata "Grading System" imekuwa tofauti na miaka ya nyuma. Sasa sijui hizi ndio huenda zikawa sababu za msingi, anyway ngoja tuwasubirie hao wakuu sana wa Wizara na Baraza watoe tathmini yao.

 
wewe Pasco uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana. yaani unaarisha utumbo. siku nyingine usiposti utumbo wako hapa unadhihirisha jinsi ulivyo kihiyo

ngoja tukupe shule,

wakati James Mbatia andai mitaala ya elimu ulifuatilia mjadala bungeni??.ni kosa la nani kutokuandaa mitaala ya elimu?? ni wizara au Baraza la mitihani??

baraza la mitihani linatunga mtihani kutokana na mitaala ya elimu haliandai mitaala na syllubus ya kufundishia ,

hata hivyo wengi tulitahiniwa na hili baraza, huwezi kujastfy eti baraza limetunga mitihani mi sijawahi kuona mtihani mgumu toka nianze kusoma na
kama mitihani ni migumu mbona kuna waliopata daraja la 1 na daraja la 2

baraza linatahini wanafunzi kulingana na sylabus, usiogope kuibebesha mzigo serikali yako acha ukipofu,

ni juzi tu walimu waligoma serikali ikakimbilia mahakamani. kufuta mgomo halali kibabe leo wewe hayo huyaoni??

baraza la mitihani limetimiza wajibu wake, serikali iwajibike


 
katika maisha yangu sikuwahi kuona mtu wa ajabu kama wewe Pasco
nina maswali muhimu nataka nikuulize wewe kijana ,wacha msumeno ukate pande zote Pasco ili tutie akili.
Naendelea kutafakari nitakujibu, ila mimi sio kijana, labda ka ni kijana wa zamani!
Pasco.
 

Pasco,

Nikijumlisha hapo kwenye bluu napata jumla ya alama 148......! Kwa maana hiyo binti yako hakufikisha alama 150!
 
Kwa grading system sidhani kama inaweza badilishwa maana lazima iandikwe nyuma ya cheti ambazo tayari waliopita wameshaandikiwa hivyo itawezekanaje ichi ikawa na grading tofauti,kuhusu utunzi ni vizuri pia tukaishi kwa uhalisia kuliko kukalili kama hawatunga nje ya syllabus sioni shida ila haya kuangalia ya enzi hizo ndio maana ichi inarudi nyuma hakuna mawazo mapya kulingana na wakati
 
Hapa sijakuelewa.......maswali yaoke kwenye kitabu? Sio yatungwe na wataalamu wa NECTA?


upo sahihi maswali lazima yatungwe na wataalamu wa necta kwa kufuata mihutasari inayotumika mashuleni. mihutasari iliandaliwa na necta. NECTA wanapotunga mitihani, lazima wazingatie mambo mengi. waelewe kuwa kuna shule hazina walimu wakutosha, maabara, nk...... lazima kuwe na 25% ya maswali mepesi sana, 50% ya maswali ya kati na 25% ya maswali magumu. lazima mtunzi wa maswali azingatie table of specification ambayo hufuata formula ya knowledge, comprehension, application, analysis, synthesis na evaluation (KCAASE). ukichunguza mitihani mingi ya necta, utakuta ina kasoro nyingi. haiendani na formula ya kcaase ambayo ni maarufu katika utunzi wa mitihani.

dk. joyce lazima ajiuzulu kwa sababu ofisi yake ilipotunga mitihani haikuzingatia haya yote. mwaka jana, umoja wa walimu wa kiislamu wa somo la maarifa ya kiislamu, walilalamika kuwa wanafunzi wanaofanya mtihani wa maarifa wanafelishwa. ilibidi kamati iundwe na ikabainika madai haya yana ukweli. dkt hakujiuzulu. i think it is the right time for her to quit.
 
Kwani Huyu mama ndo anawafundisha kutukana si wazazi tunamtukana spika na watoto wanafuata kutukana kwenye paper. Na bado watatumia cms za matsusi wazazi wao. Maji hufuata mkondo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…