Mkuu Fidelity, sijutii uamuzi wangu kusomesha vijana wangu shule za kata, bali naumizwana kijana wangu kichwa wa hisabati, kupata daraja C.
Mwaka juzi, binti yangu last but one, aliomba kujiunga St. Marian Girls nini nikamgomea wife akawasha moto, hadi kumpeleka kufanya usahili, matokeo alikosa, alilia sana baada ya kuambia cut off point ni makisi 150/200. Akamthibitishia mama yake kuwa amedhulumiwa, hawezi kukosa average ya 75 kwa mitihani mitatu waliofanya!, binti analia tuu, hatimaye nikakubali, mimi, binti na mama, hao Bagamoyo kwa mkuu wa shule, tuki demand kuona matokeo halisi ya mwanetu!.
Kwanza tulikataliwa, nilipoeleza sababu nyeti nilizozisikia kuhusu selection ya St. Marian, Mkuu wa shule akanikubalia, ikaitishwa file, narking scheme na pepa za mwanangu, wamefanya pepa 4. hesabu, sayansi, Kiingereza na maarifa!. Kila pepa maswali 50 na kila swali makisi 1. Cut of point ni makisi 150/200. Binti kapiga 42, 32, 38 na 36. Total ni zaidi ya 150/200 hivyo ni over and above ile cut off point yao, kuuliza sasa kwa nini hakuchaguliwa, nikaletewa hadithi!.
Kufuatia matokeo haya mabaya, wale wazazi tunao waaminia wenetu, hatuwezi kukubali hili likapita hivi hivi tuu!.
Mimi ni kama Tomaso, sikubali mpaka nione pepa moja tuu, ya hesanu ya kijana wangu!. Kiukweli, pamoja na mengine yote, " The games that NECTA plays on poor people!, its very dangerous gamea!".
Pasco.