Dr. Kitila Mkumbo awa Profesa

Dr. Kitila Mkumbo awa Profesa

hongera zake kafaidi jasho lake.lazima atakua na publications..
 
Oh yeah...ulikuwa hujui? Sikujua kama alikuwa anaandikia Pambazuka pia. Big up.

Mijitu humu inabisha bisha as if inabishana na watu wasiojua lolote kumbe wengine walikuwa majirani zake kabisa . Some of these people man!



Mi wala sijapotea. Halafu hufai kabisa wewe. Sijui kwa nini tu unapenda kunibania.....mpe Hi basi ukimwona.

- Hiyo ya Prof nilipitiwa tu huwa anapaongelea sana Yard
- WN jana nimemwona ila ujumbe wako ndio nauona leo
 
Bora yeye kazipata kwa jasho, kuna mtu hata hajasome ila anaitwa Dr fulani

Ha ha ha! Kuna watu mna majungu! Yeah. Kila m2 na bahati yake. Kuna wengine wanasotea mali, ila wengine wanarithi, hawajui hata machungu yake, lakin ndio ivo, nao wanaitwa matajiri. sawa tu na wale waliosota!
 
Wakuu, mimi mawazo yangu ni kwamba pale Mlimani pana utaratibu wa kupanda kwenda kuwa Professor, wenyewe wanaita Academic posts.

Posts zenyewe zipo kama ifuatavyo:

Tutorial Assistant

Assistant Lecturer

Lecturer

Senior Lecturer

Associate Professor

Na mwisho ni Professor kamili

Sasa kama walivyochambua wakuu NN na Kiranga, professor ni mwalimu wa kiwango cha juu katika eneo lake la ufundishaji au taaluma.

Professor mara nyingi hutumia muda wake mwingi chuoni anapofundisha na hata kama anapata fursa ya kuwa mshauri wa serikali ni kwa mkataba wa muda fulani.

Ikiwa atafanya kazi katika taasisi fulani basi mara nyingi ni taasisi isiyofanya biashara au non profit organization.

Hawa ma-professor wetu wengi wao kwa miaka nenda rudi wamekuwa wakijihusisha na siasa, biashara na hata mambo mengine yasiyo ya kutumia taaluma yao katika kuendeleza taifa letu lenye umaskini wa kujitakia.

Ndio maana kuna mwenzetu mmoja hapo juu ametanabaisha majina ya ma-professor ambao mpaka sasa wamelitosa taifa letu ambalo linazidi kukuza idadi ya wananchi wajinga na wasofahamu kitu.

Hata matokeo ya kidato cha sita mwaka huu yamedhihirisha hali hiyo ya ujinga ulokithiri kwenye jamii ya kitanzania, maana hata walimu hamna na hata kama wapo hawalipwi mishahara inayostahiki.

Hivi kweli professor ambae anaishauri serikali kuhusu utendaji wa shirika kama la TTCL anaweza kuamua kwamba TTCL iuziwe kampuni ya Air- Tel na sio kuikodisha mitambo ya TTCL kampuni hiyo na iwe inalipa serikali fedha ambazo zingeelekezwa kwenye mambo mengine ya maendeleo?

Au Professor kama Juma Kapuya anaweza kuacha kushughulika na taaluma yake ya sayansi ya zoology (kama sikosei)na akawa anawinda visichana vidogo ili akavibake kweli? (kwa mujibu wa taarifa za magazeti)

Kwahio kuna haja ya kutenganisha siasa na u-professor na kuhakikisha kwamba hawa wataalam wanakuwa wakitumia taaluma zao kutengeneza jamii ilio na uelevu.

Hata hivyo nampongeza bwana Kitila Mkumbo kwa kuteuliwa kwake kuwa professor mshiriki na nampa wazo moja tu, kwamba aachane na siasa na akazanie hata kwenda kuandika vitabu maana makabrasha pekee hayatoshi na mara nyingi ni rahisi kuwekwa kabatini kama sio kusomwa.

Ila akiandika vitabu na vikauzwa basi anakuwa anajitengenezea kiinua mgongo na hapo hapo analipwa na chuo anachofundisha bila kukimbilia kuwa mwanasiasa.

Always akumbuke siasa ni kitu kimoja na taaluma ni kitu kingine tofauti na cha maana.
 
Profesa Mkumbo ni miongoni mwa maprofesa wenye umri mdogo nchini, ambaye ni chapakazi na mpiganaji kielimu na kimaisha aliyeanza kazi mwaka 2001 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akiwa Ofisa Tawala na pia alikuwa mwanafunzi wa shahada ya pili ya Saikolojia chuoni hapo.

Safari ya maisha ya Profesa Mkumbo ilipitia mambo mengi, ikiwa ni pamoja na malezi yasiyo na wazazi. Juni 21, mwaka 1971, ndiyo siku aliyozaliwa huko kijijini Mgela, Iramba mkoani Singida."Kwa bahati mbaya wazazi wangu walitengana mapema na kuondoka nyumbani nikiwa bado mdogo chini ya umri wa miaka mitatu, hivyo nililelewa na bibi na mjomba wangu," anasimulia Profesa Mkumbo.

Pamoja na changamoto hiyo, walezi wake walijitahidi kumlea ambapo alianza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Mgela na alipokuwa darasa la nne ndipo alipomfahamu mamaye, ila mamaye huyo alifariki muda mfupi baada ya kumfahamu.

Jambo hilo likawa tatizo kwake, kwani aliendelea kuishi na walezi wake na kwamba katika familia yake walizaliwa wawili. Yeye na dada yake ambaye hivi sasa ameolewa na anaishi na familia yakehuko Mombasa, Kenya.

Anasema kwa kuwa alizoea kuishi na bibi na mjomba, maisha yaliendelea na yeye alijitahidi kwenye masomo kwa kuwa aliamini mkombozi wake ni elimu.

Jitihadazake za masomo zikazaa matunda, kwani alipomaliza elimu ya msingi alichaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Mwenge, alikosoma kidato cha kwanza hadi cha nne."Nilisomeshwa na walezi wangu kwa msaada pia wa wasamaria, kwani sikumfahamu baba yangu wakati huo na wakati nimemfahamu mama, naye akafariki muda mfupi tangu nimjue," ni kauli ya Profesa Mkumbo.

Jambo hilo likaendelea kumpa nguvu Mkumbo na kuongeza juhudi kwenye masomo ambapo baada ya kumaliza kidato cha nne alifaulu na kuchaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari Pugu kwa masomo ya sayansi."Hapo nikapata furaha, nilifahamu mwanzo wa safari ya mafanikio imewadia, nilifurahi sana na nikaendelea kusaidiwa na wasamaria na walezi wangunikaenda shuleni Pugu", anasisitiza Profesa Mkumbo.

Juhudi zake zikawa zile zile kwani aliamini kusoma kwa malengo ndiko kutakakomkomboa kimaisha na hapo akaongeza juhudi iliyomfanya afaulukidato cha sita na kuchaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kusomaShahada ya Sayansi kwenye Elimu na kuhitimu mwaka 1999.

Hakuishia hapo, mwaka 2001 alipoajiriwa chuoni hapo alikutana na mkewe huyo na kufunga ndoa mwaka huo huo. Mkewe ambaye ni Ofisa Tawala chuoni hapo, amekuwa msaada mkubwa kwa Profesa Mkumbo, ambaye kila wakati anamsifia kwa kumfanikishia na kusisitiza kwamba nguvu kuu ya mafanikio ni huyu mkewe.

"Kwa kweli mke wangu ndio mafanikio yangu, nampenda sana, yeye ndiye aliyefanikisha nikafika hapa na leo nimepata uprofesa, yote ni kwa ajili ya juhudi na msaada wake mkubwa katika familia yetu", alisema Profesa Mkumbo.

Akiwa msomi na pia mmoja wa waanzilishi wa Chama kipya cha Siasa chaACT-Tanzania baada ya kuenguliwa Chadema, Profesa Mkumbo amepitia mambo mengi na changamoto mbalimbalikatika maisha.Baada ya kuajiriwa chuoni hapo kama Ofisa Tawala, wakati huo alikuwa anasoma shahada ya pili ya Saikolojia chuoni hapo na alihitimu mwaka 2002.

Ilipita mwaka mmoja tu tangu amalize masomo yake hayo na yeye akahamishiwa kwenye Idara ya Taaluma akiwa Mhadhiri Msaidizi.Kupenda kwake masomo kulimfanya aende kusoma tena Shahada ya Falsafa ya Udaktari (PhD) ya Saikolojia katika Chuo cha Southampton, Uingereza.

Anasema kipindi hicho akisoma Uingereza, ndipo baba yake mzazi alirejeanyumbani mwaka 2005 na alifariki muda mfupi wakati huo yeye alikuwa masomoni.

"Baba yangu mzazi alirudi nyumbani, ila wakati huo mimi nilikuwa masomoni Uingereza mwaka 2005, na alifariki muda mfupi, hapo ukawa mwisho wa uhai kwa wazazi wangu wote," alisemaProfesa Mkumbo.

Tukio hilo halikukatiza masomo yake, kwani alifanikiwa kumaliza masomo yake mwaka 2008 na kurejea nchini kuendelea na kazi chuoni UDSM, ambapo alipanda cheo na kuwa Mhadhiri Mwandamizi mwaka 2011.

Maisha yake na siasa Wakati huo akiendelea na taaluma yake, pia alipendasiasa na kwamba alishawahi kuwa mwanachama cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) hadi mwaka 2005. Mapenzi yake kwenye siasa yakahamia Chadema, ambako alidumu kwa miaka kadhaa hadi mwaka 2013 alipofukuzwa uanachama akiwa Mjumbe muhimu wa Kamati Kuu yachama hicho.

"Nimekuwa nikifanya siasa kama sehemu ya harakati, niliwahi kuwa CCM, na nilihamia Chadema sio kwa sababu ni chama bora kuliko CCM, la hasha! Niliamini kujiunga kwangu huko kuna fursa ya kujenga chama, na tulifanikiwa kweli na kuifanya Chadema kuwa mstari wa mbele kiitikadi na kisera," alisema.

Na kwamba kwa bahati mbaya ile nia yaoya kuibadilisha Chadema kiuongozi ilishindwa na hivyo akaishia kufukuzwa uanachama. Profesa Mkumbo aliwahi kuwa Mkuu wa Idara chuoni hapo mwaka 2009 hadi 2011, pia kuwa Mkuu wa Kitivo cha Elimu katika Shule Kuu ya Elimu Dar es Salaam (DUCE), Julai 2012 hadi Novemba 2013 alipojiuzulu.

Kuhusu ACT-Tanzania Akizungumzia kuhusu chama kipya cha ACT-Tanzania, ambacho kimeanzishwa hivi karibuni, Profesa Mkumbo anasema yeye ni miongoni mwa waanzilishi na kwamba Watanzania watarajie mengi mazuri, kiuongozi, kiitikadi, kisera na hata kifalsafa.

Anabainisha kuwa wanatengeneza chamakitakachobadilisha na kuondosha dhana ya kwamba vyama vingi ni ubabaishaji, uhuni, upatukaji na uropokaji.

"Tunajenga chama chenye nidhamu, kiuongozi, kisera, kiitikadi na kimtazamo, wananchi wataona na kushuhudia hayo na hivyo tuna imani tutaendelea kupata wanachama wengi zaidi", anasema Profesa Mkumbo.

Kuhusu kupata ngazi hiyo ya uprofesa, Mkumbo anasema anashukuru kwa Baraza la Wasomi chuoni hapo kuona kazizake na kutambua mchango wake katika jamii, hivyo kumpandisha ngazi hiyo kutoka udaktari hadi uprofesa.

Kupanda kwake ngazi kulitangazwa Agosti11, mwaka huu na baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na kwamba Makamu Mkuu wa UDSM (Taaluma), Profesa Makenya Maboko alisema Dk Mkumbo nawenzake wamepata hadhi hiyo.

Hata hivyo, taarifa kamili itatolewa wiki inayoanza kesho kuhusu kazi alizofanya na alama alizopata hadi akafanikiwa kupanda ngazi hiyo. Profesa Mkumbo ni baba wa watoto watatu, wa kiume wawili mmoja mwenye umri wa miaka 11, na mwingine miaka minane na wa kike.
 
Mkumbo ni aina ya wachezaji ambao maisha yao yote wako bench, yaani anavaa na jezi kabisa, wakati mwingine mpaka anatrot, unaweza kudhani ataingia kucheza.

wapiii, anajaza nafasi kwenye benchi tu na kushangilia magoli ya wenzake, na wakifungwa ndio analia sana pia
 
nimemfuatilia hii historia yake na kuitafakari kwa mapana nikagundua mambo mawili

1;hana malezi ya wazazi, alilelewa zaidi na bibi, kwahiyo akajengwa kwenye mazingira ya kimtaa,,na kudekezwa hata ukifanya utumbo, !!!WALIOLELEWA NA BIBI WANATAMBUA HILI

2:Ana laana ya wazz wake(BABA).nimejaribu kusoma na kurudiarudia sikuona jitihada zake kuhusu kunfuatilia bb yake,kumthamini,kumsaidia kiuchumi na hata kuja kumzika bb yake(hana utofauti na kigwa)

kwa hali hiyo inatosha kusema jamaa laana inamuandama sana na hata ACT itakuwa hivyo kama alivyosaliti cdn
labda aende akaombe bb yake msamaha hapo ndipo atakapokombolewa kifkra na baadaye kukomboa jamii
 
nimemfuatilia hii historia yake na kuitafakari kwa mapana nikagundua mambo mawili

1;hana malezi ya wazazi, alilelewa zaidi na bibi, kwahiyo akajengwa kwenye mazingira ya kimtaa,,na kudekezwa hata ukifanya utumbo, !!!WALIOLELEWA NA BIBI WANATAMBUA HILI

2:Ana laana ya wazz wake(BABA).nimejaribu kusoma na kurudiarudia sikuona jitihada zake kuhusu kunfuatilia bb yake,kumthamini,kumsaidia kiuchumi na hata kuja kumzika bb yake(hana utofauti na kigwa)

kwa hali hiyo inatosha kusema jamaa laana inamuandama sana na hata ACT itakuwa hivyo kama alivyosaliti cdn
labda aende akaombe bb yake msamaha hapo ndipo atakapokombolewa kifkra na baadaye kukomboa jamii

1) Kulelewa na bibi imekua dhambi? Wangapi wamelelewa na bibi zao na ni watu wanaojitambua na wanamichango chanya. Je inafuatilia kuwa kila naelelewa na bibi anadekezwa?

2) Kilichoandikwa kwenye taarifa #1 (sijui source yake ni ipi na madhumuni yake yalikia yapi?) hakijitoshelezi kukuruhusu wewe kufikia conclusion unazozitoa. Tafakuri yako iko flawed.

3) Prof. ndani ya Chadema alichukua a calculated risk bahati mbaya au nzuri strategy "yake" ikagunduliwa na akafukuzwa uanachama. Hii haitoshi?
 
Nimeshangaa sana kusikia kuwa kabla ya 2005 Kitila alikuwa CCM,
Kumbe miaka ya mid to late 1990's tulipokuwa DARUSO tukifanya harakati za chuo kumbe mwenzetu alikuwa kada wa CCM huku akitudanya kuwa yeye ni mpiganaji na mpinzani 4 life?
Nilikuwa naamini hukumu aliyopewa CDM alionewa ila sasa naanza kupata wasi wasi na huyu jamaa, vinginevyo aje jamvin kukanusha
 
1) Kulelewa na bibi imekua dhambi? Wangapi wamelelewa na bibi zao na ni watu wanaojitambua na wanamichango chanya. Je inafuatilia kuwa kila naelelewa na bibi anadekezwa?

2) Kilichoandikwa kwenye taarifa #1 (sijui source yake ni ipi na madhumuni yake yalikia yapi?) hakijitoshelezi kukuruhusu wewe kufikia conclusion unazozitoa. Tafakuri yako iko flawed.

3) Prof. ndani ya Chadema alichukua a calculated risk bahati mbaya au nzuri strategy "yake" ikagunduliwa na akafukuzwa uanachama. Hii haitoshi?

unapingana na uhalisia,,malezi ya bibi au babu kwa watoto tena kwa wale ambao hawakusoma outocome yake ndo akina profesa

lkn hata hivyo kwann tunajidili kulelewa na bibi peke yake tunakacha kujadili yy kumkimbia,kumsahau na kumdhalilisha bb yke??
 
Nimeshangaa sana kusikia kuwa kabla ya 2005 Kitila alikuwa CCM,
Kumbe miaka ya mid to late 1990's tulipokuwa DARUSO tukifanya harakati za chuo kumbe mwenzetu alikuwa kada wa CCM huku akitudanya kuwa yeye ni mpiganaji na mpinzani 4 life?
Nilikuwa naamini hukumu aliyopewa CDM alionewa ila sasa naanza kupata wasi wasi na huyu jamaa, vinginevyo aje jamvin kukanusha

huyo ndiye mwasisi wa chama mbadala wa cdm nchini taz!!!!!
ukishangaa ya mkumbo utayaona ya dotto c rangimoto
 
Mtasema yote Kitila ndo ilikuwa engine ya CdM sasa haipo lazma CDM ipotee tu,angalia record ya chama toka waanze vugu vugu na huyu Kitila?haijashangilia ushind wa aina yyte ile hii n ishara tosha kuwa mzigo haitofika kule ulkokusudiwa only because engne ilyokuwa inasupport operation imeondolewwa kwenye machine.R.I.P Chadema


Sent from my iPhone using JamiiForums.🔩🔨uuuu
 
nimemfuatilia hii historia yake na kuitafakari kwa mapana nikagundua mambo mawili

1;hana malezi ya wazazi, alilelewa zaidi na bibi, kwahiyo akajengwa kwenye mazingira ya kimtaa,,na kudekezwa hata ukifanya utumbo, !!!WALIOLELEWA NA BIBI WANATAMBUA HILI

2:Ana laana ya wazz wake(BABA).nimejaribu kusoma na kurudiarudia sikuona jitihada zake kuhusu kunfuatilia bb yake,kumthamini,kumsaidia kiuchumi na hata kuja kumzika bb yake(hana utofauti na kigwa)

kwa hali hiyo inatosha kusema jamaa laana inamuandama sana na hata ACT itakuwa hivyo kama alivyosaliti cdn
labda aende akaombe bb yake msamaha hapo ndipo atakapokombolewa kifkra na baadaye kukomboa jamii

We naye kumbe ni Kilaza yaani mtoto wa miaka mitatu angewezaje kuwatafuta wazazi wake ulitakiwa ujishughulishe kwanza kujua ni kwa nini alitengana na wazazi wake katika umri mdogo kiasi kile
 
huyo ndiye mwasisi wa chama mbadala wa cdm nchini taz!!!!!
ukishangaa ya mkumbo utayaona ya dotto c rangimoto

Sasa kuna chama gani hapa Tanzania ambacho waasisi wake hawajatoka CCM?
 
Halafu siku hizi hizi anasifiwa sana na serikali na gazeti la habari leo! Wakati kipindi kile walitaka kumfukuza chuo walipogundua alikuwa chadema. Sasa baada ya kugundua sasa hivi kitila sio hatari tena kwa CCM anasifiwa na vyombo vyote vya CCM. Maana yake nini? Ni ngumu sana kwa Kitila kukiosoa tena serikali waziwazi km tulivyozoea. Eti ndio mwanaharakati wa mageuzi tanzania.

Hivi Kitila kabisa uliamini kwamba uongozi wa chadema uliokuwapo madarakani ungeweza kuondolewa kwa njia za siri halafu chama kibaki kimoja na chenye nguvu? Hata ungepata uprofesa X100. Hapa nimeshindwa kukuelew kabisa busara zako. Uharaka wa kupindua uongozi uliokuwepo ulikuwa wa nini kma sio tamaa? Wew kama msomi hukujua umuhimu wa kutumia ushawishi wa kistaarabu ili wenzako waone umuhimu wa kubadili uongozi? Tabia uliyoonesha chadema was very immature! Huoni kwamba makakati wenu ungefaniiwa ungekigawa chama katika makundi? Hujui kwamba ili taasisi yoyote iwe imara mambo yanatakiwa yafanyike kwa consensus na sio kwa mbinu za kichinichini? Dharau mlizoonesha kwenye waraka wenu mbona hazishabihiani na haya unayotaka kuwaaminisha watu. Mlichokifanya kwenye waraka ule ndio siasa za kistaarabu mnazoenda kufanya ACT? Kusema kweli kitila umetuangusha sana wasomi wenzako kwa tamaa ya fedha na madaraka.

Kwa hiyo mlikuwa mmepanga kwamba Zitto awe mwenyekiti, wewe katiba mkuu na mwigamba mtunza fedha? Uwazi mnaouhubiri nyie kina mkumbo huko ACT ni upi? Wa waraka wa siri? Give us a break!
 
Haya sasa Prof. KITILA MKUMBO vs Ndugu TUNDU LISSU, lissu aokote makopo.
bunge limejaa maprof na madr lakini ndiyo hao wanaozomea ndiyooo kama hakuna matatizo yanayopasa kushughurikiwa kwa weledi.
 
Back
Top Bottom