Dr. Kitila Mkumbo awa Profesa

Hongera Assocaite Proffessor Kitila Mkumbo, umefika wakati wa kujitofautisha na Siasa sasa kama mwana taaluma, Fanya kazi yako ya taaluma zaidi achana na Siasa, Siasa za Bongo si za Wasomi bali wababaishaji ndio maana wasomi mkiingia kwenye siasa mnakuwa wababaishaji.
 
waheshimiwa, habari nilizonazo ni kuwa juzi kikao cha senet chuo kikuu cha dar es salaam imemtunuku hadhi ya uprofesa dr. Kitila mkumbo. Kwa hiyo kuanzia sasa sio tena doctor bali ni professor. Hongera profesor mkumbo

big up prof

ila kuwa makini sana kunawengine humu watakukaribisha kwenye kashukrani loh
sikuhizi wana dawa za kumaliza mtu baada ya miezi sita...kumbuka wengi wanakukumbuka maumivuuliyowapatia
 

Mazee, kibongo bongo profesa ina ujiko zaidi. Sijui kwa nini hasa ila nadhani ni vile linavyo-sound (I know it's silly). Lakini pia, kwa UDSM hususan enzi zile ambapo chuo kikuu kilikuwa kimoja tu (ukiacha Sokoine), associate professors na professors mishahara yao ilikuwa zaidi ya senior lecturers.

So a move up in rank went along with a bump in pay. Maybe this could partly explain the perception of prestige.

Halafu zamani mtu kuwa profesa hapo UDSM haikuwa lazima uwe na PhD. Siku hizi sina hakika kama bado wana huo utaratibu.

Sasa sijui hiyo dhana ya profesa kuwa prestigious zaidi ya PhD inatokana na nini maana kitaaluma mtu mwenye PhD asiye profesa atakuwa kamzidi profesa asiye na doctorate.

Kinyamwezi hai make sense sababu wao hata mtu kuwa na PhD si nongwa kivile. Kuna watu kibao tu wana PhD lakini hata huwezi kuwajua kama wanazo. Case in point - Maj.Gen. Harold Greene aliyeuliwa majuzi huko Afghanistan. Huyo angekuwa mbongo titles zote zingekuwa zinajulikana Dr. Maj. Gen Harold Greene....lakini unyamwezini kama hayuko kwenye academia ni ngumu kujua. Wangapi wanajua kuwa Newt Gingrich ana PhD? Ushawahi kusikia anaitwa Dr.Newt Gingrich?

Hapo UD zamani ilikuwa rahisi kujua hata nani kasoma wapi. Wale washua waliosomea Marekani walikuwa hawana nyodo za ku flaunt titles zao. Ila wale waliosomea Ujerumani Mashariki, Romania, Hungary, Yugoslavia na kwingine huko kwa Masoshalisti walikuwa na nyodo sana za kutaka kujulikana.
 
WanaJF,

Naamini wote tunamfahamu ndugu Kitila Mkumbo kwa wadhifa wake wa uhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam. Katika wadhifa wake huo yeye amesimama kwa kiwango cha elimu cha Ph.D na alikuwa akiitwa Dr. Kitila Mkumbo kwa kipindi kirefu kwa sasa.

Ila kwa sasa ndugu Kitila Mkumbo ameukwaa u-professor rasmi na kuanzia leo atakuwa akijulikana kama Prof. Kitila Mkumbo!

Taarifa hii ni dhahiri itawatia hasira sana watu wa CHADEMA huku wakiongozwa na babu Slaa bila kumsahau Mbowe!

Jamani, wote kwa pamoja tutumie fursa hii kumpongeza ndugu Kitila Mkumbo kwa kuukwaa u-professor!
 
Uwe unasoma mabandiko mengine kabla ya kuleta uzi wako hapa. Hiyo habari tayari iko jamvini.Acha misifa na kujipendekeza
 
Hivi vigezo vya mtu kuwa professor ni vipi?
 

I thought so.

They should take it from someone who should know.

Professor maana yake ni mwalimu.

Kifaransa ukitaka ku distinguish mwalimu wa chuo kikuu unasema le professeur dans le superieur, otherwise hata mwalimu.wa shule ya msingi ni "le proffeseur".

Kuna jamaa alikuwa anafundisha historia first year, wanafunzi wakimwita Dr. ilibidi awasahihishe.na kuwaambia kwamba "mimi.si Dr. kwa maana sijafanya Ph.D yangu bado, mimi.ni professor tu".

Sasa bongo nashangaa kuona "professor", which is basically "teacher", inakuwa na prestige kuliko Dr. which is an actual academic distinction denoting that someone has a Ph.D .

Hata Obama alikuwa professor wa sheria, lakini hana Ph.D
 
Uwe unasoma mabandiko mengine kabla ya kuleta uzi wako hapa. Hiyo habari tayari iko jamvini.Acha misifa na kujipendekeza

Kama habari tayari umeisoma kilichokuleta humu kwenye huu uzi nini!? Au ni kiherehere?
 
Alienda sabbatical leave lini? Amefanya utafiti gani ? Kaandika juu ya nini?
 
Ccm ina maprofessor wengi lakini idadi kubwa ni hawana mchango wowote zaidi ya madudu ref;.Magembe
 
Ndio raha tu ya kuwa CCM, hata kipindi kile Prof. Baregu angekubali kuwasujudia CCM asingeondolewa na Ghasia pale UDSM. Alaimua kuutunza na kuuheshimu U-professa wake.

CCM ni jinga kubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…