Dr. Kitila Mkumbo awa Profesa

Nyani Ngabu na Kiranga

Kimsingi nakubaliana na mitazamo yenu.

Lakini katika academic rankings za kwenye academic institutions za Tanzania, mtu kuwa 'Professor' ni ishara ya kupanda kitaaluma.

Ngoja niwape mchanganuo:

1. Tutorial Assistant (B.Sc. or B.A) ,

2. Assistant Lecturer (M.Sc. or M.A),

3. Lecturer (PhD),

4. Associate Professor (PhD and other requirements), na

5. Professsor (PhD and other requirements)

Hata kama neno 'Professor' lina maana ya mwalimu kwa kifaransa, katika academic rankings linamaana kubwa sana. Professor (nazungumzia aliye na PhD na vigezo vingine vinavyohitajiwa) anakuwa ni nguli katika eneo lake la kitaalamu.

Tatizo kwa upande wa Tanzania linakuja katika namna ya vigezo vingine (zaidi ya kuwa na PhD) vinavyopatikana na kuwa assessed. Kwa mfano, moja ya vigezo ni kuwa na published articles katika 'international journals'. Kwa Tanzania, vyuo vikuu havina utaratibu wa kurank hizi international journals. Mwishowe, watu wanakuwa promoted to 'Professorship' katika journals ambazo hata published articles zao haziwe kusomwa wala kuinfluence policy, knowledge, theories n.k.

Katika publishing world kuna namna journals zinakuwa ranked kwa namna articles zinazochapishwa katika journals hizo zinavyokuwa cited na kuinfluence the state of knowledge. Hapa ndipo unasikia journal inakuwa na 'impact factor'. Kwa sasa, journals zenye high impact factor katika ulimwengu wa sayansi ni journals za 'Nature', 'Cell', 'PLoS', na Science'. Pia kuna journals zingine zinakuwa na high impact factor katika eneo husika la kitaaluma kama fizikia, kemia, uchumi, elimu, biashara, siasa, tiba, mazingira, sheria n.k.

Kwa vyuo vikuu vya nje, promotion based on published works inakuwa scrutinised kwelikweli kwa assessors kuangalia aina za journals ambazo mtu anaye seek promotion amepublish. Kwa Tanzania, nimeambiwa hilo suala halifuatiliwi kabisa, ilimradi iitwe international journal, basi mtu atasubmit hizo published articles kwa promotion.

Nitafurahi kuona journals ambazo Kitila Mkumbo kapublish maandiko yake aliyoyatumia kuseek promotion to associate professorship.

Ni hayo tu.
 
Last edited by a moderator:
Hivi unajua kuwa Chelsea Clinton ana PhD kutoka Oxford? Sijawahi kuona popote pale akijitambulisha kama Dr.Chelsea Clinton...

Sasa subiri Ridhiwani apewe hata hiyo ya heshima....

ha ha haaaa
 
Kila alifanyalo wataka kuambiwa....!! Sabattical ..hahaha
 
Kama habari tayari umeisoma kilichokuleta humu kwenye huu uzi nini!? Au ni kiherehere?

hao Ndio wafuasi wa CDM, ukiwa sio CDM basi wewe ni adui kwao. Wanafanya siasa kama vita.
 
Kama atakuwa amepandishwa atakuwa siyo professor bali ni associate professor. Utofautishe hivi vitu. Huwezi kutoka dr kuwa professor moja kwa moja. Kuna cheo hapo katikati ambacho nimekitaja hapo juu. Ukome kudanganya umma

Acha wivu, jamaa kapiga hatua.
 
It's gorgeous! so, far amefanya kazi nzuri kitaaluma (mtazamo ni wangu). Nimesoma machapisho yake hapo juu and to be frank I'm impressed by the knowledge he has contributed to his field of study. I think, asihukumiwe kwa imperfection because it is equally true that we all have perfection fetishes. Muhimu kwake, na wengine ni kuhakikisha jamii inanufaika na elimu aliyonayo.
 
Ndugu yangu Kijazi ili upewe Uprof lazima utimize vigezo vinavyokulika kitaalum na kimataifa. Unapompima Profesa let say Mwandosya kwa vigezo vya kisiasa sio sawa.

Unapompima Profesa Lipumba let say kwa kumlingansha Zito Zuberi Kabwe sijui unatumia mizania gani. Profesa Lipumba ni Resource ( chimbuko la marifa) wakati Zito Zuberi Kabwe ni mpiga debe na anafaa kuwa mtendaji.

Kwenye siasa kuna mambo mengi ya hovyo. Wakati mwingine ukiwa mtaalam unapotaka kutumia taaluma yako unazuiwa kwa misingi ya kisiasa hasa katika nchi zisizoendelea kama za kwetu. Mwanasiasa anaheshimika kuliko mtaalam. Wenzetu Mhandisi aliyesimamia kujengwa kwa daraja jina lake huandikwa penye daraja kama ishara ya kumheshima Mhadisi kwetu hapa linaandikwa jina la Mwanasasa aliyelifungua. Kufungua ni muhimu kuliko kujenga.

Kitendo hiki kimewakatisha tama wataalam wengi pengine maovu tunayoyaona yanatokana na wataalam kuingia uwoga wa kupatilizwa na wasiasa. Ukitaka kujua umuhimu wa wasomi nenda chuoni usiende Bungeni. Pale unakuta mtu kama Sugu anasema uwingi wa takwimu sio hoja kwa sababu tukipima malaria au UKIMWI tunachua tone la damu na sio debe zima. Mtu kama huyu akikubalika anaweza kuwa Rais wa nchi kama Afrika Kusini Zuma hajasoma.

Unapotaka kumpima Profesa Mkumbo usimpime kwa ugomvi wake Freeman Mbowe, Uprofesa haupatikani jukwaani, haupimwi na watu wa mitaani unapimwa na Maprofesa ni evidence based.
Haya basi twende huko kwenye huo unaouita Usomi, wamefanya nini?
 


anzania yetu ina mambo dunia nzima hakuna
hata ma engineer nao lazima waitwe
'mheshimiwa engineer Stella Manyanya'

sisi ni zaidi ya Banana Republic.' labda tujiite 'Maandazi Republic'
 
Hivi unajua kuwa Chelsea Clinton ana PhD kutoka Oxford? Sijawahi kuona popote pale akijitambulisha kama Dr.Chelsea Clinton...

Sasa subiri Ridhiwani apewe hata hiyo ya heshima....


Dr Jakaya Kikwete
Dr Reginald Mengi
Dr John Nchimbi
Dr Maji marefu...
 
Mbona na Dr. Slaa ni professor lakini ajitambi, mbona Mwlm Nyerere alikuwa Prof. lakini alikufa akiitwa mwalimu acha usamba u-prof ni jina tu kama la majimarefu ua professor J

Naona hata babayako ni profesa ila hataki tu kujionyesha
 
Ukiwavuruga tu chadema unapata u prof kitilia kafanya alichofanya chadema sasa prof chezea cc wewe
 
Mnyonge mnyongeni haki mpeni yaani kila kitu kupinga hangekuwa bado yuko chadema haya yote mngesema duh ukawa nouma
 

Hapo umenikuna sana hata mimi ningependa kuona Journal ambalo Huyu Bw.Sospeter Muhongo amepublish, anajiita yeye ni Bingwa wa Jiolojia Afrika, kwa maana nina bifu naye sana huyu Mzee!

Halafu i
sitoshe hilo uliloandika naamini ni kweli tupu, kwa kuwa huwa ninashangaa hawa wanaojiita Maprofesa huwa wanaafanya huo utafiti na kuandika saa ngapi? Mbona tuko nao mitaani kila siku tunapiga ulabu mpaka naite kali?
Nijuavyo mimi kuwa researcher siyo mchezo kuna watu wanalala maabara lkn hawa Maprofesa wa kwetu kutwa wapo baa na kuzengea vibarmaid siwataji tu majina kwa kuwasitri, sasa hizo impact factor wanazifikisha saa ngapi au ni magenius?!

 
Saivi anaitwa prof kufata mkumbo

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 

Umesahau 'Senior lecturer' kabla ya associate professor.

Na pia, kwa UDSM, at least zamani (sina hakika kwa sasa) mtu kuwa full professor wala haikuhitaji PhD.

Kama unaweza, angalia prospectus za miaka ya 70, 80, na 90. Wamba dia Wamba hakuwa na PhD na alikuwa full professor!

Lakini tukizungumzia elimu tu, mtu mwenye PhD ana elimu kubwa kuliko full professor mwenye Master's.

Vile vile, wapo ma-PhD ambao hawana Master's. Yaani wana Bachelor's halafu wakaenda moja kwa moja kwenye PhD. Namjua mmoja alifanya hivyo lakini sitamtaja humu kwa sababu za privacy lakini mnaweza ku-guess na mkapatia....hahahahaaa
 

Mfumo huu una msingi gani?

Au ni wetu tu tumeutunga wenyewe?

Najaribu kuangalia kimataifa zaidi, katika dunia ya leo ya kimataifa.

Nisije kurudi bongo, nikajiunga na chuo, nikamuita mwalimu "professor" kwa kujua mwalimu wa chuo kikuu ni professor, nikawa nimeharibu.

Au ni katika zile habari za kuukuza uprofesa tu uonekane kama.unatoka galaxy ya mbali?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…