Dr. Mwakyembe Vs. TAKUKURU



Jile.
Heshima yako mzee.
Mwizi ni mwizi tu.Aliyeiba kuku na yule aliyeiba ng'ombe wote ni wezi.Kinachokuja kuwatofautisha ni baada ya hukumu kutolewa.

Sina neno lingine lenye uwezo wa kuwakilisha mwizi wa kuku na mwizi wa ngo'ombe

Kulingana na post yako basi Mwakyembe ni Fisadi mtoto na Lowasa na RA ni mafisadi wakubwa.
Lakini baado maana yake iko palepale kwamba wote ni wezi na wanaiba pesa za wananchi.

Kwa kukusaidia, Ninakuomba utafute thread za Mwanakijiji au nakala yake moja aliandika kwenye gazeti la mwanahalisi jinsi anavyowaelezea hawa wanaojiita wapiganaji.Hakuna kitu hapo.Zote ni mbio za kukimbilia madaraka.wnatamani kutuua kwa ajili ya kukimbilia vyeo.
Kwanini alikuwa anaogopa kwenda tangu mwanzo?Hana usafi wowote huyu bwana zaidi ya njaa kumsumbua.
 
mi namuona muoga na mjinga kabisa maana mbwembwe zote zile za kuwatunishia misuli PCCB leo anakubali kuhojiwa...hana maana kabisa kabisa

Acha chuki zisizokuwa na msingi. Mwakyembe ni wale wanasiasa ambao ni daring, jasiri asiye na woga anayetetea maslahi ya taifa lake. Labda upate nafasi ya kuongea naye ana kwa ana utabadili mawazo yako. What is PCCB si chombo tu cha Serikali kama vyombo vingine?
 
ulikuwa mtaji wa kisiasa
Kama haukuwa mtaji wa kisiasa kwa nini kuna mambo ambayo hakupenda kuyatoa kwenye ripoti ya Kamati teule ya Bunge? Aliyaacha kwa manufaa ya nani?
 

Hivi mambo ya umeme wa upepo ameamua kuuacha au namna gani, maana haku-declare interest wakati akiwa kwenye Kamati Teule ya Bunge!
 
Tupe source ya hiyo information. Kama huna basi utakuwa kwenye pay roll ya rostam
 
Ana ujasiri kama ule wa mama Simba..
 
Sasa ukilipwa posho mbili au tatu na vyombo vya serikali kwa hundi za serikali, Rushwa iko wapi hapo??? PCCB mandate yao ni ipi???

Ili si suala la administration tu, Waziri mkuu angetoa mwongozo kuwa kuanzia sasa serikali na mshirika ya umma yatalipa posho moja tu, sio suala la rushwa ili.

PCCB fanyeni kazi yenu, mkitaka kujua rushwa nendeni Tanesco, polisi, BOT, mahakamani, nk
 

Moelex, hapo unapowaelekeza ni maua tu, mizizi iko huku
watendaji wa mitaa
polisi post
vyuoni
tawala za mikoa
mahospitali
mpirani
gesti
kwenye kulipa bili za maji na umeme

halafu zikitoka huko ndio zinakua maana watu wanaanza kuona tangu wanazaliwa... kama tunataka kupiga vita rushwa sustainably, basi tuanzie pia sio juu pekeyake
 
mi namuona muoga na mjinga kabisa maana mbwembwe zote zile za kuwatunishia misuli PCCB leo anakubali kuhojiwa...hana maana kabisa kabisa

wacha u-makamba. Jibu hoja. Kwanza mtoa mada hajaweka chanzo cha habari yake, pia hayuko bongo, tatu tusikurupukie hoja au mada. Hata kama kahojiwa sio sababu kuchonga
 
Hatimaye mpiganaji ameamua kutii Sheria ya Nchi ambayo ameshiriki mwenyewe kuitunga? Halafu siku hizi haongei sana kwa kuwa kitu kilichompatia umaarufu, Richmond, kimewekwa kapuni, kwa hiyo mtaji wa kisiasa ume-expire?

Hii ya Buchanan is too low na sina uhakika kama imetoka kwenye oblongata yake mwenyewe,nahisi kuna msela wa kijiweni kaiba password ya Buchanan"the greatest thinker"na kuandika upupu kama huu!

""Inakupasa kusema kila siku hata ama hamna la maana la kulisema kwa tija ya wananchi?Walahi sikujua kama inatakiwa iwe hivyo!"
 
Kama haukuwa mtaji wa kisiasa kwa nini kuna mambo ambayo hakupenda kuyatoa kwenye ripoti ya Kamati teule ya Bunge? Aliyaacha kwa manufaa ya nani?

Buchanan,
Kwani nawewe pia unataka kupingana na Metcalf's Law?, daktari yule alijua kwamba aliyoyaacha yatakuwa chachu ya mijadala humu na kwingineko na kesho utakujaona ndio kwanza yameanza kunoga Richmond bado mbichi mkuu.
 

Niliwaona Mwakyembe na Mpendazoe siku ya Jumapili pale City garden, labda walikuwa wanajiandaa kuhojiwa.

Wametimiza wajibu wao, sasa tuone PCCB watafanya nini na uchunguzi wanaoufanya.
 
Wanasiasa ni vigeugeu:

SPIKA wa Bunge Samuel Sitta amemtetea Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe kwamba, ana haki ya kutokubali kwenda katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhojiwa kwa kuwa sheria na kanuni za Bunge hazimlazimishi.
 
Mwakyembe ni FISADI wa kuchoka.

Kama Rostam Azzi asingelimzidi KETE na AKILI na kutaka kuuiba mradi wa umeme wa UPEPO, amini amini nakuambia, leo hii Mwakyembe angelikuwa kama Amos Makala akirusha karate na magumi kumtetea RA na EL.

Ki-homeboy aka Fisadi baba aka RA alipoona dili safi namna hii, akawazunguka na kuwaacha kwenye mataa. Ndiyo kisa wanachukiana hadi leo. Vinginevyo angelikuwa katulia kama maji mtungini akitafuna posho mbilimbili na kumalizia sasa hivi mradi wa umeme wa upepo. Na MGAWO huu wa sasa, ahh mwana wane, angelikuwa anazila tu za umeme na za ubunge na za POSHOs.

Alivyozidisha maneno miezi kadhaa nyuma, kiRA kikamlima kwenye magazeti. Jamaa akachanganyikiwa kabisa. Akawa akiitisha maandamano na mikutano ili AJIOSHE. Bahati mbaya akapambana na Balile akawa anachekacheka tu kama nani vile?? Ule utulivu wake woote ghafla ukageuka. Mara wanataka wamuuwe kwa ajali mara wanataka wamuuwe kwa kisu na simu za Ericsson na huku vijana wake wakiteka mtu na kumfungua kwa Mwakyembe. Kuhaha kwake kulikuwa kama msichana Bikra siku ya ndoa. Kaenda TAKURURU karudi mwepesiiii!!!! Ngoja tusubiri SHUKA jeupe tuone lina rangi gani!!!!!!!!!!!
 

Mafisadi Mkapa, Rostam, Idrissa Rashid, Chenge, Manji, Subhash Patel na wao watahojiwa lini na PCCB kuhusiana na ufisadi wao!? Au hawa wako above the law?
 
mi namuona muoga na mjinga kabisa maana mbwembwe zote zile za kuwatunishia misuli PCCB leo anakubali kuhojiwa...hana maana kabisa kabisa
je wewe kama wewe ulitaribu uthubutu alo utenda japo punje ya ulezi? Sifia panapostahili .ok mungu atakutoa huko gizini ulipo akulete kwenye mwanga ili upambanue cheupe na cheusi.
 
watu kwa kweli wana matatizo; tatizo halikuwa Mwakyembe kuhojiwa na TAKUKURU; tatizo lilikuwa huwezi kuwa subpoena wabunge wakiwa kwenye kikao ni kinyume na Katiba! Alipoingia AG mpya aliwatumia ujumbe kina TAKUKURU kuwa hawawezi kufanya hivyo na ndio HOsea akakimbia Dodoma maana kingemuungulia na ndio sababu wao kusitisha uchunguzi wao hadi kikao kilipoisha.

Nje ya kikao cha Bunge unaweza kumuita mbunge kumhoji kirahisi tu!
 


Una uhakika hilo lilikuwa tatizo, kweli? Ndicho walichomaanisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…