Binafsi naamini Raisi naye anapenda kuanzisha Mijadala isiyo na tija.
Kwani ni lazima kusema kila Jambo linalomfurahisha au kumkera Sana?
Suala la Dk. Mwele lilishapita na hakutakiwa kulizungumzia tena kwa kuliunganisha na taasisi za kimataifa ambazo kesho na kesho kutwa tutahitaji msaada wao pale ambapo magonjwa ya mlipuko yatakapo tokea.
Jana nimeona BBC NEWS habari kubwa ilikuwa ni Raisi kumpongeza Ofisa aliye charaza wanafunzi viboko.
Huu nao pia ni mjadala mkubwa ambao ameuanzisha na hauna tija. Chanzo cha mjadala huu ni hotuba yake aliyoitoa Jana.
Mh. Raisi ajitahidi kuwa na kifua cha kuifadhi mambo hata kama yanamfurahisha au kumsikitisha.