Dr. Mwele Malecela: Asiyekuumba, kukuumbua hawezi

Dr. Mwele Malecela: Asiyekuumba, kukuumbua hawezi

Waliomtuma wamempa kazi ! Una mfano wa mgonjwa wa Zika popote utuonyeshe !?
Ungekua na CV ya kueleweka ungeelewa tatizo elimu yako ya kuunga unga ndo maana unaona kazi za mashirika ya kimataifa unapewa tu kama uteuzi wa DED
 
Hivi barua ya kuomba msaada wa ebola si tuliandika kwenda kwa huyu????
 
Tena niliona kama Rais ameongea kwa uchungu sana aiseeee

Ni kama vile ilimuuma huyu dada kupewa kazi WHO. Probably alitaka baada ya kumfukuza asikie dada ame lost mbaya. Ila siku zote Mungu huwa hanywi chai [emoji4]. Baada ya kumfungia dirisha Mungu akamfungulia geti dada yetu, mambo yake mswano
 
Binafsi naamini Raisi naye anapenda kuanzisha Mijadala isiyo na tija.

Kwani ni lazima kusema kila Jambo linalomfurahisha au kumkera Sana?

Suala la Dk. Mwele lilishapita na hakutakiwa kulizungumzia tena kwa kuliunganisha na taasisi za kimataifa ambazo kesho na kesho kutwa tutahitaji msaada wao pale ambapo magonjwa ya mlipuko yatakapo tokea.

Jana nimeona BBC NEWS habari kubwa ilikuwa ni Raisi kumpongeza Ofisa aliye charaza wanafunzi viboko.

Huu nao pia ni mjadala mkubwa ambao ameuanzisha na hauna tija. Chanzo cha mjadala huu ni hotuba yake aliyoitoa Jana.

Mh. Raisi ajitahidi kuwa na kifua cha kuifadhi mambo hata kama yanamfurahisha au kumsikitisha.
jamaa ni jau
 
Kwa mtindo huu, je nitakuwa nakosea nikitabili kuwa siku moja huko mbele tutakuja kuambiwa Benno Ndullu nae alifukuzwa kazi kama gavana wa BOT kwa kufanya kazi kwa maelekezo ya mabeberu? Na sasa hao hao wamemtafutia kazi huko aliko!!!
Gavana Ndullu alistaafu mkuu.
 
Mabeberu wana mbinu nyingi tuna muunga mkono Rais tuko pamoja kupinga mikakati ya kibeberu
 
Waache tu. Kwanini watulazimishe kutoa taarifa za uongo. Accreditation ya vyombo vyetu vya kitafiti vitakuwa compromised kama tutaendelea kupelekwa namna hii. Lazima tujiamini.
Acha kuzungumza mambo usiyoyajua' unajua part wanayofanya, waliyokwisha fanya shirika la who kwenye maisha ya binadamu wa Tz?

Kama ilivyo serikali kuna uwezekano kukawa na viongozi ndani ya who wasio na maadili, hiyo haimaanishi shirika Zima ni useless kwetu.
 
...tofauti yako na hao wanao mtazama ni wewe kuwa haupo hapo !
Pamoja na hayo, haimaanishi kuwa sisi tusiokuwepo hatumtazami...wote tuna mtazama na kumsikiliza lakini ni dhahiri shahili kwamba hatuwezi kumchukulia sawa

Hata hivyo, inabidi aelewe kwamba kama kiongozi wa nchi asimamapo jukwaani ajue nchi nzima inamtazama, bara na hata dunia nzima! Akilijua hilo atachambua maneno ya kuongea!

Maana kuna maneno anaongea kwa kudhani anasikilizwa na wale wanakijiji tu waliopo uwanjani ambao wengi wao uelewa wao wa mambo yanayoendelea duniani sio mkubwa kama hawa wengine wa duniani wanaomtazama
 
Sasa Mbona rais wetu hakutaja jina la huo mteule Halafu amejitokeza Dr.Nywele inaonekana huyu mama sio mzuri ni agent wa mabeberu,Nafikiri hata Ebola ni yeye mwenyewe anatuzushia
 
Hata Mimi nashangaa sana.
Unajua siyo kitu kizuri KWA mwanaume kugombana au kuzozana NA mwanamke kulingana NA utamaduni wa kiafrika. Mwanamke mwingine ktk ugomvi Ka!a huu anaweza kukudhalilisha KWA umma, anaweza kusema kuwa "ulimtongoza kisha akakulkatalia" ndio maana unamsakama sana.
Huyo mwanamke alitangaza jambo hadharani pasipo kuongea kwanza na bosi wake ambaye ni waziri wa afya anayefanya kazi chini ya rais wa nchi.

Ukiwa msomi sana unajikuta katika hatari ya kuwa ni kiburi cha elimu yako, unasahau kuwa unaweza kuwa na elimu kumzidi bosi wako lakini unafanya kazi kwa muongozo wake. Wasomi wa kiafrika wanao udhaifu huo.
 
Hongera mkuu. Maneno ya busara sana haya.

Back
Top Bottom