Dr. Mwele Malecela: Asiyekuumba, kukuumbua hawezi

Dr. Mwele Malecela: Asiyekuumba, kukuumbua hawezi

Dr. Mwele ungekaa kimya mama!, ukishambuliwa ukatulia mimi huwa naona inakuwa bora zaidi kuliko kujibu...anyway watu tunatofautiana malezi!
Mkuu mbona kama hapa na wewe hujakaa kimya? Unajua kwann umeongea? Umekereka na majibu yake. Ulitaka anyamaze.

Sasa Imagine wewe ambaye haikuhusu umeongea kwa sababu amefanya kile usichopenda, Je yeye ambaye inamuhusu moja kwa moja kwa kufanyiwa kile asichopenda?

Ukishambuliwa instict zinakutuma ujitetee. Ni Mara chache sana, kwanza si Mara chache lazima utajitetea tu kwa rafiki, au kwa ndugu au rohoni kwako. Lakini utajitetea.

Kama Ile tweet ililenga kumjibu mh, basi ni vizuri maana Mh atajua ni nn huyu mama anawaza juu ya makosa anayoamini mama ameyafanya. Kama hili kosa kalifanya kweli basi raisi ameshajua kuwa huyu mtu hajajutia pamoja na mm kumuadhibu.

Mfano angetweet ' Watz mnisamehe, Raisi wangu nisamehe mjadala ungekuwaje?
 
Hata hili la Ebola kutangazwa tangwa huko nje mkuu naona mkuu kahisi fyokofyoko ilikoanzia huenda kwa huyu huyu ndo kaamua kupitishia zika
 
Pamoja na hayo, haimaanishi kuwa sisi tusiokuwepo hatumtazami...wote tuna mtazama na kumsikiliza lakini ni dhahiri shahili kwamba hatuwezi kumchukulia sawa

Hata hivyo, inabidi aelewe kwamba kama kiongozi wa nchi asimamapo jukwaani ajue nchi nzima inamtazama, bara na hata dunia nzima! Akilijua hilo atachambua maneno ya kuongea!

Maana kuna maneno anaongea kwa kudhani anasikilizwa na wale wanakijiji tu waliopo uwanjani ambao wengi wao uelewa wao wa mambo yanayoendelea duniani sio mkubwa kama hawa wengine wa duniani wanaomtazama
He is too local,too unprofessional,he is so incompetent ataanzaje kwanza kuchagua maneno , wewe hushangaii mambo ya ccm hoyee yamekujaje kwenye jukwaa la kimataifa?Hivi Rungu nae aliposimama kuongea alitaja chama chake au yeye huko Zambia hana chama?
 
Huyo mwanamke alitangaza jambo hadharani pasipo kuongea kwanza na bosi wake ambaye ni waziri wa afya anayefanya kazi chini ya rais wa nchi.

Ukiwa msomi sana unajikuta katika hatari ya kuwa ni kiburi cha elimu yako, unasahau kuwa unaweza kuwa na elimu kumzidi bosi wako lakini unafanya kazi kwa muongozo wake. Wasomi wa kiafrika wanao udhaifu huo.

So ndio tayari alishamuadhibu KWA kumuondoa kwenye wadhifa wake alionao, sasa KWA nini bado anaendelea kumfuata fuata NA kumsakama????????

Unajua, hata ktk maisha ya kawaida ya wanandoa , mume unapoamua kumuacha mke NA kisha unamfukuza nyumbani kwako unatakiwa kumuacha moja KWA moja ili awe huru kuendelea NA hamsini zake. Usimuonee wivu pale atakapoolewa tena NA mwanaume mwingine NA kuwa na maisha mazuri zaidi NA Yale aliyokuwa akiishi kwako.
 
Binafsi naamini Raisi naye anapenda kuanzisha Mijadala isiyo na tija.

Kwani ni lazima kusema kila Jambo linalomfurahisha au kumkera Sana?

Suala la Dk. Mwele lilishapita na hakutakiwa kulizungumzia tena kwa kuliunganisha na taasisi za kimataifa ambazo kesho na kesho kutwa tutahitaji msaada wao pale ambapo magonjwa ya mlipuko yatakapo tokea.

Jana nimeona BBC NEWS habari kubwa ilikuwa ni Raisi kumpongeza Ofisa aliye charaza wanafunzi viboko.

Huu nao pia ni mjadala mkubwa ambao ameuanzisha na hauna tija. Chanzo cha mjadala huu ni hotuba yake aliyoitoa Jana.

Mh. Raisi ajitahidi kuwa na kifua cha kuifadhi mambo hata kama yanamfurahisha au kumsikitisha.
Kikubwa ni mshahara kwani kazi ya sasa inamlipa vizuri kuliko hiyo kazi ya awali ya masimango na hofu ya kutokuongea ukweli, hata sasa tetesi za Ebola huko mipakani zipo lakini waziri wa Afya kwa kuhofia kukosa watalii kaamua kukanusha kwa nguvu kubwa kulinda kibarua chake
 
So ndio tayari alishamuadhibu KWA kumuondoa kwenye wadhifa wake alionao, sasa KWA nini bado anaendelea kumfuata fuata NA kumsakama????????

Unajua, hata ktk maisha ya kawaida ya wanandoa , mume unapoamua kumuacha mke NA kisha unamfukuza nyumbani kwako unatakiwa kumuacha moja KWA moja ili awe huru kuendelea NA hamsini zake. Usimuonee wivu pale atakapoolewa tena NA mwanaume mwingine NA kuwa na maisha mazuri zaidi NA Yale aliyokuwa akiishi kwako.

Naungo mkono hoja yako kwa 100%
 
Binafsi naamini Raisi naye anapenda kuanzisha Mijadala isiyo na tija.

Kwani ni lazima kusema kila Jambo linalomfurahisha au kumkera Sana?

Suala la Dk. Mwele lilishapita na hakutakiwa kulizungumzia tena kwa kuliunganisha na taasisi za kimataifa ambazo kesho na kesho kutwa tutahitaji msaada wao pale ambapo magonjwa ya mlipuko yatakapo tokea.

Jana nimeona BBC NEWS habari kubwa ilikuwa ni Raisi kumpongeza Ofisa aliye charaza wanafunzi viboko.

Huu nao pia ni mjadala mkubwa ambao ameuanzisha na hauna tija. Chanzo cha mjadala huu ni hotuba yake aliyoitoa Jana.

Mh. Raisi ajitahidi kuwa na kifua cha kuifadhi mambo hata kama yanamfurahisha au kumsikitisha.
21 Kwa ajili ya mambo matatu nchi hutetemeka, Naam, kwa ajili ya manne haiwezi kuvumilia.
Mithali 30 :21

22 Mtumwa apatapo kuwa mfalme; Mpumbavu ashibapo chakula;
Mithali 30 :22
 
Si kama dengue tu zimekuja zimeondoka...
Umesema vyema mkuu, hawa wakina tajiri mpole naona uwezo wao wa kufikiri haujasambaa vya kutosha. Wao kazi ni kushangilia kila afanyalo mr. Jiwe. Ni shida, nabaki najiuliza kwa akili hizi za mkubwa ajambi, hii nchi tutatoboa kweli??
 
Alishasema anapenda Shilawadu unafikri kichwani mwake kajaza nini ?
Binafsi naamini Raisi naye anapenda kuanzisha Mijadala isiyo na tija.

Kwani ni lazima kusema kila Jambo linalomfurahisha au kumkera Sana?

Suala la Dk. Mwele lilishapita na hakutakiwa kulizungumzia tena kwa kuliunganisha na taasisi za kimataifa ambazo kesho na kesho kutwa tutahitaji msaada wao pale ambapo magonjwa ya mlipuko yatakapo tokea.

Jana nimeona BBC NEWS habari kubwa ilikuwa ni Raisi kumpongeza Ofisa aliye charaza wanafunzi viboko.

Huu nao pia ni mjadala mkubwa ambao ameuanzisha na hauna tija. Chanzo cha mjadala huu ni hotuba yake aliyoitoa Jana.

Mh. Raisi ajitahidi kuwa na kifua cha kuifadhi mambo hata kama yanamfurahisha au kumsikitisha.
 
Dr Mwele twambie Zika iko wapi?

ZIKA ilizikwa na Magufuli…!
Mtanzania leo hii akifa na ugonjwa wa ZIKA ataambiwa kafa kwa ugonjwa USIOJULIKANA…!
Kwa awamu hii EBOLA=ZIKA=UGONJWA USOJULIKANA!
Ni sawa tu na kusema WATU WASIOJULIKANA…! Si jambo la ajabu kusikia Mhe.Tundu Lissu aliposema tuna Rais wa ajabu sana na baada ya muda mfupi WATU WASOJULIKANA WAKAMTWANGA RISASI mchana kweupe na hawajajulikana mpaka mtondogoo…!
 
Like yangu ni ya 122, sijaona likes nyingi kiasi hichi[emoji2089][emoji2089][emoji41]
Binafsi naamini Raisi naye anapenda kuanzisha Mijadala isiyo na tija.

Kwani ni lazima kusema kila Jambo linalomfurahisha au kumkera Sana?

Suala la Dk. Mwele lilishapita na hakutakiwa kulizungumzia tena kwa kuliunganisha na taasisi za kimataifa ambazo kesho na kesho kutwa tutahitaji msaada wao pale ambapo magonjwa ya mlipuko yatakapo tokea.

Jana nimeona BBC NEWS habari kubwa ilikuwa ni Raisi kumpongeza Ofisa aliye charaza wanafunzi viboko.

Huu nao pia ni mjadala mkubwa ambao ameuanzisha na hauna tija. Chanzo cha mjadala huu ni hotuba yake aliyoitoa Jana.

Mh. Raisi ajitahidi kuwa na kifua cha kuifadhi mambo hata kama yanamfurahisha au kumsikitisha.
 
Uko sahihi mkuu lakn kwa hulka za wanadamu huwa ni ngumu mno kushinda hali kama ile, muda mwingine tunaumizwa ama kufurahishwa na ishara ya haya ni mtu akiumizwa analia, anaweza pia kupigana hata ngumi yote hii ni ishara ya disscontent lakn pia akiwa na furaha atacheka, kutabasamu ama hata kuimba wimbo wenye kuonyesha hali ile, kwa mh Rais na tukio alilolitenda Dr Mwele bado inajimuktadhanisha na maelezo yangu haya na ukweli hakuna ugonjwa wa ZIKA uliokuja kutukia sasa swali tulitakiwa kujiuliza je zika aliizika dr mwele? Kwanini hakukuwa na hata dalili baada ya taarifa yake hyo na kutumbuliwa kwake? Kwanini Rais asionyeshe hasra zake kwa alichokifanya huyo mtumishi wa umma?

Muda mwingine tunashabikia ujinga tu lakn ukwel wa habar hii tulipaswa kujiuliza swali hili tu kwamba huu ugonjwa ulikuwepo kweli? Kwann ulipotea?
Hivi ugonjwa wa ZIKA upoje na ueneaji wake upoje na unachukua muda gani kuenea kwa watu wengi kiasi cha kuonekana kutisha?
 
Ipo Havard University
Inakosekanaje Google sasa kwa mfano?! Hata kwenye repository ya London School of Hygiene and Tropical Diseases ipo! Ila tukitafuta za wanaoongea sana hata Google hazipo! Ukim-google japo ni PhD holder unakutana na picha za matukio tu, no machapisho no dissertation! Aibu hii!!
 
Back
Top Bottom