Elections 2015 Dr. Pombe Magufuli, Rais mteule wa Tanzania awamu ya 5

Elections 2015 Dr. Pombe Magufuli, Rais mteule wa Tanzania awamu ya 5

Ivi tukijumlishaa kura zilizo aribika nchi nzima atupati elfu 10 au 20...
 
Nimepita pita sehemu kadhaa na kukuta watu wakitizam Tv live kutangazwa kuteuliwa Raisi Mpya wa awamu ya tano Wa Tanzania... lakini ukiwatizama wamenyong'onyea sana kama wanaumwa...

Naomba ufanye kazi sasa kama ulivyoahidi... CCM Oyee
Mimi huku niliko ni shangwe tu...

Watu wanaimba 'Lowassa.....Tumemkataa'
 
Bila shaka, ni manung'uniko kila kona, hasa kufuatia utabiri wa January Makamba kwamba Magufuli lazima atanganzwe leo.

Kumekuwepo ujuma za wazi, hasa ushahidi wa Matokeo ya kule Bumbuli, ambayo yalikuwa dhahiri kabisa kwamba mchezo fulani ulichezwa.

Hii inatuacha kutafakari kwamba: je, Magufuli ni Rais wa NEC au wa Watanzania?
Kwahiyo kumbe NEC wamepangiwa ratiba na Makamba??Bavicha mna mambo.
 
Hatimae baada ya kufikia matakwa yao, JF sasa inapatikana bila wasiwasi,
 
Taratibu watanzania wataelewa kuwa kuacha chama kimoja kudumu madarakani ni hasara kimaendeleo. Chama inabidi kiwe na hofu ya kudondoka madarakani ndio kitafananya maendeleo na kuogopa kufanya ufisadi. Lakini kwa kuipa ushindi ccm ni kuwaondolea hofu ya kufanya ufisadi. Subiri siku si nyingi hela zitaaanza kuibwa bila aibu. Mgema akisifiwa tembo hulitia maji. My heart to cdm shall remains.
 
naamini demokrasia bado ,kinacho niuma sana tena sana ni kwamba kiongozi anatufikisha alipotufikisha
mama mtoa maamuzi ya nchi
mtoto mtoa maamuzi ya nchi lakini bado watanzania wenzangu bado wanamwamini n kupata wasaa kumshangilia wakati anatuletea mtu wa aina hiyo hiyo
MUNGU ATUSAIDIE SANA
ILA TUSIKATE TAMAA KWANI KUFANYA HIVYO NI KURUHUSU WATOTO WETU NAO WAWE WATUMWA WA NCHI YAO
 
Nimepita pita sehemu kadhaa na kukuta watu wakitizam Tv live kutangazwa kuteuliwa Raisi Mpya wa awamu ya tano Wa Tanzania... lakini ukiwatizama wamenyong'onyea sana kama wanaumwa...

Naomba ufanye kazi sasa kama ulivyoahidi... CCM Oyee

peke yakohushangilii watu huku full shangwe
 
ukitazama pande zote mbili CCM na chama tawala na matokeo ni wazi kuwa wapinzani walikuwa na nafasi ya kuiondoa CCM madarakani mwaka huu.

ccm ingeondoka madarakani kutokana na mambo ambayo asilimia kubwa ya watendaji inaowatumia wamekuwa wakitumia uongozi kujinufaisha. na katika kufanya hivyo wengi wamekuwa wakifanya mambo haya waziwazi au wananchi wakiangalia rasilimali zao na wanachikipata kuona kama haviendani.

huu ulikuwa mtaji mkubwa sana kwa vyama vya upinzani kwa sasa kutokana na hali ya wananchi wengi kutambua au kusikia mambo haya na kuchukia serikali hii.

lakini wapinzani walijichanganya kwa kutochanganya karata zao vizuri na wao kujikuta wakionekana kuwa na mapungufu pia.

kwanza kwa kuwa na mgombea ambaye amewafunga midomo wapinzani kuzungumzia mambo mabaya yanayotendwa na serikali. ikumbukwe kuibua mambo mabaya yanayofanywa na serikali na kuwatetea wananchi ndio sera zilizokipa chama cha demokrasia na maendeleo umaarufu. baada ya chama hiki kupata wabunge wachache na wakaanza kila siku wanaibuka na hoja tofauti bungeni na kuwasha moto wananchi walikikubali chama hiki na kikaanza kuwa maarufu.

kwa bahati mbaya chama hiki cha demokrasia na maendeleo hakikujitafakari na kujikuta kikichagua kubaki na kundi fulani la vijana hasa baada ya kuingia kwenye sera za hoja za nguvu kwa kutumia maandamano na maneno makali.

kwa wakati huo chama cha mapinduzi kilikuwa kimegundua siri ya chama hiki kidogo kukua na walipoitupa njia hiyo iliyowapa umaarufu, ccm waliiokota na kuzunguka nchi nzima kwa hoja zilezile wakiongea kana kwamba serikali si yao. mbinu hii ilikirudisha chama cha mapinduzi ulingoni tena na kurudi katika chati za kuvitishia vyama vidogo katika ushindi wa knock out.

kwenye kampeni ccm walichagua karata zao vizuri kwa maana mgombea alikuwa yeye binafsi anakubalika na wakaja na hoja zinazolenga matatizo ya wananchi.

wapinzani wakajichanga tena kwa kuja na timu isiyoshirikiana yaani kama ni mpira wanasema timu inategemea uwezo binafsi wa wachezaji. hii ni kutokana na mgombea waliyemsimamisha kuwa maarufu yeye kama yeye lakini hapatani na hoja na sera za chama ambazo wamezisimamia mda mrefu. mbali na mtizamo wa hoja za mgombea ikawa mgombea anashindwa kutawala jukwaa, hali yake ya kiafya yote haya yalisababisha kampeni za upinzani kutokuwa na hoja bali kubakia na kauli mbiu za mabadiliko.

kama mgombea wa ukawa angekuwa na nguvu kama mbowe, akawa anajua kuongea kama sumaye, akawa anataswila kama ya jaji warioba kwenye jamii, akawa na mvuto kwenye jamii kama wa kwake mwenyewe na wakajenga hoja na sio kauli mbiu ilikuwa ni wazi ccm kilikuwa mashakani kurudi.

mwaka 2020 ni vyama vyote kujiandaa kurekebisha makosa yanayowagarimu.

lakini kwa sasa tatizo letu kubwa ni katiba kwa maana bila ya watanzania kuona kupitwa wakati kwa katiba yetu kunaitikisa nchi yetu vibaya mno na mitikisiko hii tusipoitafutia ufumbuzi haraka itatubomoa.

katiba mpya ni muhimu kuweka kuweka misingi yetu ya kuchaguana, ni muhimu kuweka mifumo ya kusimamiana kwa lengo la kutoa haki na usawa, kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuweka nidhamu kwa kila anayeishi ndani ya ardhi yetu.

hili ni jambo ambalo raisi ajaye angelipa kipaumbele namba moja na hilo ndilo litamfanya kutimiza yale anayolenga kuwafanyia watanzania.
 
Haki huinua taifa

Mungu ibariki Tanzania na usimame upande wa haki!
Msemo huu wa maandiko Matakatifu una maana kubwa mno!
 
Mwaka 2005 Ushindi 80%

Mwaka 2010 Ushindi 68%

Mwaka 2015 Ushindi 58%

Mwaka 2020 Ushindi .....

Ngoja kwanza tujenge taifa. 2020 UKAWA itakuwa imekufa jumla kwa mziki wa Magufuli na mamvi naye atakuwa monduli hivyo ccm itapiga reverse 90% kwa kazi tu.
 
Back
Top Bottom