Elections 2015 Dr. Pombe Magufuli, Rais mteule wa Tanzania awamu ya 5

Elections 2015 Dr. Pombe Magufuli, Rais mteule wa Tanzania awamu ya 5

Hongera sana Dr. John Pombe Magufuli....

Pole pia kwa mzigo mzito unaokukabili maana kuongoza nchi masikini ni mzigo mzito!!!
 
Bila shaka, ni manung'uniko kila kona, hasa kufuatia utabiri wa January Makamba kwamba Magufuli lazima atanganzwe leo.

Kumekuwepo ujuma za wazi, hasa ushahidi wa Matokeo ya kule Bumbuli, ambayo yalikuwa dhahiri kabisa kwamba mchezo fulani ulichezwa.

Hii inatuacha kutafakari kwamba: je, Magufuli ni Rais wa NEC au wa Watanzania?
daaa!!!!! xxxxx ndo TZ Hiyo
 
CCM wanatufanya watanzania wajinga!

sasa hivi ni mwendo wa kula kwa urefu wa kamba yako...hakuna kulemba maana imeshajidhihiri kuwa baadhi ya watanzania wengi ni wajinga na hawajitambui....mikoa ya kati singida,dodoma, tabora na shinyanga ambako ukipita barabara ukavuta hewa , hewa inanuka umasikini lakini bado wao ndo wamewapa kura nyingi...kule mwanza nimeshawaambia kuanzia leo nimewawekea vikwazo vya kiuchumi kwa miaka mitano..sitaki kusikia simu ya mtu akiniomba msaada wowote...manyugus!
 
nakupa pole, wastarabu tunakula bia na nyama taratibu, sio mda wa kelele za mabodaboda.
 
Misingi ikiharibika mwenye haki atasimama WAP?? Mungu ni wa haki pia Hukumu! Hajapita kwa haki! Kiti kitamtapikaa!

Lile mlilosema chaguo la Mungu liko wapi?? Mungu huwa anashindwa??
 
haina msisimko
haina mashiko
haina hisia.
kuna tofauti kubwa sana ya mapokeo ya kutangazwa kwa urais na ulinganifu wa matokeo ya kutangazwa kwa rais kwa mwaka 2005 na 2010

Halafu nasikia ataapishwa kesho....
Sijui ni kweli na Kama ni hivyo mbona haraka namna hiyo au ni kwa sababu ya.......................!!! Naogopa kusema
 
Haya bwana, kwenye anga zangu nikisikia mtu ana lalama maisha magumu namkata kidevu

Mkuu tatizo siyo wananchi angalia na upande wa pili wa shilingi kuibiwa kwa kura!
 
Hongera sana John Pombe Magufuli
Tuijenge nchi yetu kwa umoja wetu
Mungu Ibariki Tanzania
 
Hakika toka moyoni mwangu, Magufuli si rais wangu bali ni rais wa ccm. Ila kwa katiba iliyopo atanitawala kilazima. My heart to cdm and ukawa, shall remain.

Hiyo ndiyo demokrasia. Shangilia kwanza jaribu tena 2020. Tunakupenda. Tujenge nchi yetu.
 
Baada ya matokeo kutangazwa watu wengi wananiuliza wapi yalipo maduka yanayouza sumu kali sana,sijui wanataka kufanya nini nazo. Lakini wanaonekana kama vile watu waliokata tamaa, wenye huzuni, na wasio na raha. Wanatembea njiani na kuongea peke yao wakiwa wanakunywa viroba.

Mwenye taarifa ya maduka ya sumu waambieni wayafunge angalau miezi 3 ili upepo upite kwanza.
 
Back
Top Bottom