mzee alpha
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 711
- 264
Dr. John Pombe Magufuli ametangazwa rasmi kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya 5 baada ya kuongoza kwa kupata kura 58.46%.
![]()
Lubuva: Kwa kuwa mheshimiwa Dr. Magufuli, John Pombe Joseph wa CCM amepata kura nyingi zaidi kuliko mgombea mwingine yeyote, kwa niaba ya tume ya taifa ya uchaguzi na kwa mujibu wa vifungu vya 35(e), 35(f) na 81(b) vya sheria ya taifa ya uchaguzi sura 343.
Ninatangaza rasmi matokeo ya uchaguzi ya urais wa mwaka 2015 kwamba
Asanteni kwa kunisikiliza
- Mheshimiwa Magufuli John Pombe Joseph amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
- Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu amechaguliwa kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Hongera rais mteule sasa kazi tu tunataraji utawatumikia watz wote kama ulivyoahidi bila kujali itikadi zao.na hongera lowasa na ukawa yako umeleta ushindani wa kweli hadi wastaafu wakashiriki kwenye kampeni na nyie ni washindi mmeongeza % zenu za ushindi kubalini matokeo rudini mkajipange tujenge tz yetu