Tanzania kama Taifa lipo katika wakati ?tata?, kiuchumi kamataifa, kimaadili, kimaendeleo na pia inakabiliwa na maadui wakubwa sana wanaolidhoofisha taifa na kuliangamiza kabisa. Rushwa imekuwa adui mkubwa sana,kuanzia ngazi za chini kabisa mpaka za juu kabisa za uongozi na huduma zakijamii, Rushwa sasa imekuwa ni sehemu halali ya kipato chao cha kawaida chawatu Fulani katika sekta tofauti tofauti za umma hata binafsi.
Ufisadi ni zao la Rushwa, tena kubwa kubwa, nalo katikakipindi cha miaka ya karibuni imeonekana kushamiri vibaya sana, na kupelekeamvutano mkali kati ya Bunge na Serikali, ufisadi umedhoofisha baadhi ya sektana huduma muhimu kwa umma wa waTanzania.
Usiri wa mikataba inayo ingia serikali kuhusu Rasilimali zetuwatanzania, imekuwa ni jadi mikataba kutowekwa wazi ili watanzania waione,waielewe na wahoji matokeo/manufaa ya hiyo mikataba kwa pande zote, hili nalolimeonekana ni tatizo jingine kubwa sana, ambalo Serikali isipo jipangalinaweza kuwa ndio bomu au ombwe katika serikali ya awamu ya Tano, Mzee mwinyi alisema, Kila kitabu kina zamazake.
Umoja wetu wa kitaifa umetikisika hasa katika mchakato mzimawa uchaguzi wa mwaka huu, kusema ukweli ukabila na ukanda vimeonekana wazi wazibila ya kificho.
Rais wetu Magufuli, unayo kazi kubwa sana mbele yako, ambayoinahitaji mtu alien a msimamo, mtu anayeheshimu kiapo/viapo vyake na mtu anayesema kwa vitendo, mimi naamini uwezo huo unao na wewe ndie Yule ajae, atakaewakomboa watanzania, katika nyakati hizi ngumu kiuchumi.
Endelea na msimamo wako uleule uliouonyesha tangu zamani,usilewe madaraka na zaidi ya yote timiza ahadi zako.
Hongera sana Rais Mteule Magufuli.