TANZIA Dr. Sengondo Mvungi afariki Dunia

TANZIA Dr. Sengondo Mvungi afariki Dunia

RIP Dr, nakumbuka mwaka 2005 nilikuwa naye mahali! nimeshtuka sana!
 
chadema ndio wanaotakiwa kujibu issue ya dr kupigwa mapanga sha,wao ndo watakuw wahusika wakuu wa hili tukio!huu ni mwendelezo wa ile muvi ya kuteka watu na kuwatesa kama walivyofnya ulimboka

wee mshenzi kabisa, watu tunaomboleza hapa unaleta mzaa hapa, tena ITIKAVU inakufaha ngoja, RIP DR S.A.MVUNGI
 
Watu muhimu kama huyu wangehamishwa City centre kuna usalama sio mwituni. Wahindi sio wajinga kukaa jijini.
It sounds like there is a substance in yr comment!
Mbezi Msakuzi Lipelanya kwa Mzee wa Irambo na Ujumbe wa Tume ya Katiba wapi na wapi!

Kituo cha polisi immediate kiko wapi kama siyo Mbezi mwisho!

Binadamu wote ni sawa, lakini mwisho wa Siku lazima tukubali kuwa kuna majukumu mazito na Risky, tena ya Kitaifa kama haya ya Dr Mvungi, ona sasa yanatucost.
 
Ulimboka alilipwa hela anyamaze.huyu kwani kuna mkono wa Ccm?
 
Poleni wanafamilia. Poleni watanzania! RIP Dr. Mvungi MUNGU amekupenda zaidi!
 
Dah Dr Mvungi! Dah
Hakuishi kuona alichopigania! hakuona mageuzi aliyoyatamani. Dah!
 
Bila shaka Ccm ndo watakuwa wa kwanza salamu za rambi rambi! Tusisahau pia kuwa Ccm ni mabingwa wa kuhudhuria misiba ya watu maarufu.

Lakini je wanaweza kujinasua na kifo hiki? Kama mjumbe wa tume ya katiba anauwa na vibaka itakuwaje kwa raia wa kawaida? Wajumbe wa tume wamekuwa wakilindwa muda wote imekuwaje kwa Mvungi? Au ni baada ya kupendekeza serikali tatu?

Lakini uvamizi huu tunautofautishaje na wa Kibanda au Ulimboka? Je tunakumbuka maneno aliyosema Mbatia bungeni? Kwa nini haridhiki kwamba ule ni uvamizi wa majambazi kawaida?

Tutarajie mkanda wa mkenya mwingine kuhusishwa au mara hii atakamatwa mchina, maana juzi tuliona wa pembe za ndovu msishangae kuona wa mauaji!
Mkuu umethubutu,Hongera
 
Comedian wa Jeshi la Polisi alishasema eti kofia ya CHADEMA ilipatikana kwenye crime scene
 
Rip. Dr ni uzembe na udhaifu wa selikali yetu umetufikisha hapa
 
Ndugu maneno yako yanatia uchungu zaidi.

Nadhani sasa Dr Mvungi amepumzika.

Majeraha ya upanga yangeendelea kumtesa muda mrefu.

Amelinganisha kati ya kubaki na kwenda, akaona itafaa zaidi akienda.

Nadhani amemhurumia sana mkewe akijua kuwa angeumia sana kumuuguza maisha yote na familia nzima ingekuwa katika maumivu.

Atakuwa pia ameona haifai kuonana na wauaji wake katika dunia hii, pia ameona roho yake inasita kusalimiana na waliomtuma muuaji na kuonana nao uso kwa uso.

Binafsi namuunga mkono. Ni bora tu ameenda.
Duniani huku kuna mateso na taabu. More you live more you expose yourself to trouble and agony.

Mateso yamekwisha.

Kwanini kusumbua watu bana!...hata ningepona hapa hospitali ni lazima ningekuja kufa siku ingine, sasa kwanini kuwaliza watu multiple times.

Hata hivyo nimeweka kumbukumbu yangu ya kutosha. Kama ni wa kuelewa wameelewa...tofauti na hivyo wasingekaa waelewe hadi dahari.

Kutafuta mno ukweli na haki kuna gharama yake, huenda labda ndio nalipia.

My Promotion to Glory...No more trouble!
 
Very humble;genious; mwalimu wangu first yr UDSM constitutional law;one week before kuvamiwa alitupa Mada nzuri sana kuhusiana na Rasimu ya Katiba na Serikali Tatu-Mkutano ulioandaliwa na NACONGO..Mwenyezi Mungu ampe pumziko la amani;poleni sana familia,n special condolences to Dr Natujwa Mvungi;inaumiza sana kupoteza mzazi katika hali kama hii..Mungu awape uvumilivu
 
Damu yako Dr Mvungi hakika haitapotea bure kwani wale wote walohusika watajulikana mapema na malipo yatakuwa hapahapa duniani?. RIP DR Mvungi. Poleni sana wanafamilia wa Dr.
 
chadema ndio wanaotakiwa kujibu issue ya dr kupigwa mapanga sha,wao ndo watakuw wahusika wakuu wa hili tukio!huu ni mwendelezo wa ile muvi ya kuteka watu na kuwatesa kama walivyofnya ulimboka

Sometimes uwe unaweka uharoo wako pembeni,hii sredi inahusu late Dr.Mvungi hayo mambo ya siasa za majitaka weka pembeni.

Dr. Mvungi alikuwa kichwa ndio maana wauaji wamechukua laptop yake kuyapoteza madini aliyoshusha kwenye mchakato wa katiba mpya!!
 
Back
Top Bottom