Felixonfellix
JF-Expert Member
- Feb 16, 2010
- 1,672
- 183
Huzuni sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Samahani sana sikujua kama it has already been posted, nimeomba mode waiondoe, waweza pia tafadhali.
Kpifo hichi ni ngumu kikitenganisha na serikali! Dk Mvungi, profesa Mwaikusa, vifo vyao ni vya kuuliwa na majambazi... Tutakukumbuka Dk Mvungi..
Hizi habari za msiba ni za kuhuzunisha mno!
Alafu badala ya Kova kusema laptop ipo wapi yeye anatwambia gongo! Badala ya kutuonesha wahusika walokamatwa wanauza sura zao wenyewe!
Anayeua kwa upanga naye atauliwa kwa upanga
Hii sentensi ni ya masiba ama ulevi wa chama. Dr, M alikuwa mtumishi wa Umma na mwanachama wa NCCR M. Acheni kupotosha kuhusu laptop. Ofisi ndipo mahali SALAMA kuhifadhi kila jambo muhimu lililopangwa na hii TUME YA KATIBA. Tume haikuwa na mtu mmoja tu Dr, pekee, kila lililo nyeti lipo Ofisi ya tume. Kama mtu nduguye ndo amehusika na ushenzi huu ndo tayari wamekamatwa na hii eti CCM, CDM majina haya Kova hajatamka bali vimeonyeshwa vifaa tu. Tusubiri uchunguzi ukamilike ndipo tuambiwe kama waliokamatwa ni wahuni wa ktk vyama ama wa mitaani tu ama wa kununuliw!!! Kuhusu uhalifu kupanuka Serikali itambue kuwa sasa ifanye uchunguzi wa kina ijiridhishe ni kwa jinsi gani wahalifu wanapata ajira ndani ya Serikali na maeneo mengine nyeti. Pili lililo kuu Askari wanaposhiriki Opareshe ya aina ye yote ili zaidi uvunjaji wa SHERIA za NCHI HURU TZ, baada ya kupambana na wahuni wahalifu, na pindi wanapo umia ama kufa eti wanasiasa wanaunda TUME kuwatetea wahalifu sababu ni ndugu zao. Askari mwema mtoto wa mkulima anaburuzwa mahakamani eti muuwaji.
Raia tunapiga kelele pindi tukio kama hili la Dr M linapotokea zidi ya Serikali lakini hatupigi kelele pale wanapo undiwa TUME.ASKARI. TUKUBALI KUWA tuna TANZANIA POLICE FORCE na siyo TANZANIA POLICE SERVICE. WANASIASA NI AIBU KUBWA JESHI LETU LENYE UWEZO TULIOUONA KTK NCHI TANO KUSINI NA SASA KASKAZINI NA JUZI TU TUMEONA DRC. WAACHWE VIJANA WAREJESHE NIDHAMU KWA GHARAMA YEYOTE ILE. MAMBO KAMA HAYA HAYATATOKEA TENA
KUNA NCHI MOJA EAC MADUKA UTAYAKUTA WAZI HADI USIKU WA MANANE. Wanasiasa acheni mapezi kudanganya watu mm naamini mnacho penda kwangu ni kura tu. Siasa imejipa nguvu zaidi ya Sheria za Nchi. Mh Waziri Mkuu ukiona unatukanwa kusukwasukwa ni kuwa kazi unaiweza lakini ukiona mswahili anakusifu tu kila jambo mjuwe kuwa huyo Jangili. Tuna Jeshi la kutosha lipewa majukumu linaweza kukomesha maovu ya aina ye yote. Kichwa kilicho potea kukipata kingine ni baada ya miaka 40. SERIKALI ITAFAKARI SASA
Duh! Hujafa hujaumbika. Binadamu tumekuwa wakatili na wakuogopwa zaidi ya simba na fisi. Damu iliyomwagika na roho iliyotoka itawamaliza wengi. Pumzika kwa amani Dr. Mvungi