Kigogo
JF-Expert Member
- Dec 14, 2007
- 20,508
- 6,183
Na mwandishi wetu.
Emanuel Sukariguzi
Habari kutoka Dodoma zinasema kuwa dalili zote zinaonyesha kuwa makubaliano ya ndani kabisa ya CCM ni kumpitisha Dr Shein.
Shein ambae alikuwa amezingirwa na wapinga maendeleo yake huku akishutumiwa na kukandamizwa kwa sababu mbali mbali ikiwemo ile ya kuonekana kuwa ni mpemba.Hali iliyowafanya wapenda maendeleo wa Zanzibar akiwemo Dr Salmini Amour kutoikubali na kulazimika kuhamia upande wa Shein katika kumuunga mkono.
Pia hali iliyokuwa imezingira wakutanaji wa mkutano huo ni kule kuhudhuriwa na wakuu wa walioshiririki Mapinduzi ya kumuondoa mkoloni mwarabu ,Mheshimiwa Moyo na Mheshimiwa Natepe ,waliosikika wakieneza umoja wa kulaani sumu ya upemba na uunguja kwa kuwataka wapiga kura kutokumchagua yeyote yule anaeonekana ni mwenye kupandikiza chuki za aina hio.
[FONT=ArialMT, sans-serif]Minong'ono ya ndani inadai sababu kubwa ya kutaka Dk. Shein ateuliwe kugombea nafasi hiyo, kwanza ni kudumisha umoja na mshikamano visiwani na pili kutaka kuendeleza yale ambayo tayari yamefanyika[/FONT].
Habari ambazo zimepatikana kutoka ndani ni kuwa tayari uhakika wa ushindi wa Shein umeshahakikishwa iliyobaki ni utekelezaji tu.
Shein bwana naye kazidi uzezeta bana...we mtu hata mkwara hawezi kupiga sa rais gani wa ivo..apewe bilal tu kieleweke