Elections 2010 Dr. Shein aibuka kidedea; kuiwakilisha CCM urais Zanzibar 2010

Elections 2010 Dr. Shein aibuka kidedea; kuiwakilisha CCM urais Zanzibar 2010

Future ya nini tena wakati atakuwa mstaafu, kwani future ya mstaafu ni nini. au mpaka afie ofisini? ameshakuwa rais kwa miaka kumi that is enough. Kwani future ya Salmini ilikuwa nini?

future ya madarakaaaaa, sio ya fedha bwana na pia ya kulinda maslahi yetu, unajua tunavyo fanya haya mambo tunakuwa na mipango ya muda mfupi na pia ya muda mrefu. dynasty huanza vipi ?
Salim hakuchanga karata zake vizuri au ule wakati hakumpa nafasi hiyo.
Ndio maana unaona sera zetu ukitoka kuwa mkurugenzi wa shirika au katibu mkuu wa wizara, unafuatia ubunge, halafu uwaziri, ukikosa huko ukuu wa mkoa, mwenyekiti wa bodi, ubalozi nk nk ili mradi mambo yazunguke kwenye kikundi chetu. na mikataba yetu na watoto wetu.
 
hapana mkuu nimesema kwamba shein ndio atakuwa "puppet",atafanya mambo kwa kuambiwa.
Katika siasa hakuna cha upuppet. Mtu akishapata madaraka anajiona juu ya kila mtu. Kwa hiyo sahau kwamba Shein atakuwa puppet wa yeyote yule.
 
Kama kungekuwa hakuna m(i)kono w(y)a mtu/watu katika maamuzi ya nani agombee nafasi ya Urais Zenj, basi mshindi according to Paul the octopus atakuwa ni Bilal, lakini kwa kuwa kutakuwa na mikono ya watu watakaopindisha maamuzi kwa sababu moja au nyingine basi Bilal ana kazi ngumu sana ya kuweza kuibuka kidedea.
 
Duh kazi kwa kweli ipo.mwaka huu tutaona mengi.tuendelee kuiombea nchi yetu, safari hii iangukie kwenye mikono salama.
 
hapana mkuu nimesema kwamba shein ndio atakuwa "puppet",atafanya mambo kwa kuambiwa.
Mtu pekee ambaye hatafanya mambo kwa kuambiwa ni Maalim Seif tu kama watakubali kumtangaza mshindi mwaka huu. Wengine wote watafanya mambo kwa kuambiwa kwa kuwa hawatachaguliwa na wananchi wa Zanzibar bali watasimikwa kwa nguvu za dola kwa njia ya wizi wa kura. Ukiisha wekwa kwa style hii wewe unakuwa huna sauti za wananchi nyuma yako bali wale waliokuweka. So whoever win today shall be royal to masters who will ensure his declaration as a winner in October.
 
hii kitu itakuja kueleweka usiku sana, watoto tutakuwa tumeshalala.
 
Hapo ndipo nilipowashangaa wengi sana ,makamo wa kwanza wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania ,wazuke akina Bilali na Pandu ,basi msubiri jawabu tu ,nawambia kuwa SHein anashinda tena kwa kura nyingi kama si zote ,ao wengine ndio wanaoingizwa kitanzini bila ya wenyewe kujua kama wanajua wangelijitoa na mapema ili kulinda kuwepo kwenye siasa.

kaka Mwiba nafikiri tukubaliane kitu kimoja kuwa kila mtu anahaki ya kugombea. sometimes usiemtarajia anaweza shinda. Pamoja na majungu ya hapa na pale huwezi ondoa Jina lako kienyeji. Even Kikwete wakati ule wanagombea na Mkapa hakutaraji kabisa kama angeweza kufika ile level ya kufanya kura zirudiwe na kuombwa amwachie Mkapa.so to me hao wanaogombea pia ni mtaji wao for future incase wakikosa wakati huu.

Siwapendi wanaokata TAMAA mapema. by the way, nafikiri hii attention tunayoifanya wadau on CCM ndio inayofanya CCM ishinde pia...We could concentrate to Build our oppossion parties ambao wamekubaliana kutokukubaliana.
 
Mkuu nadhani wamemaliza (ingawa wanadai wanaendelea kuhesabu) lakini wametoa taarifa kuwa watatangaza rasmi matokeo hayo saa 3 (mida ya Tanzania - almost 40min left)

With many thanks kwa taarifa
 
Matokeo rasmi yatajulikana SAA TATU za usiku kwa mida ya Tanzania.

Kuna kila dalili kuwa Shein atashinda tu!
Leo hakuna kulala mpaka kieleweke.tutaendelea kusubiri mkuu. sasa ni saa mbili karibia na nusu.Nimesikia kwenye taarifa ya habari ya ITV watapitisha jina kesho sasa sijui nini kinaendelea.
 
forum_new-48.png
Jukwaa la Siasa (358 Viewing)

forum_new-48.png
Uchaguzi Tanzania 2010 (407 Viewing)

Never ever happened before, kwa Jukwaa la Siasa kuzidiwa watazamaji na Jukwaa la Uchaguzi 2010 toka lianzishwe.
 
Never ever happened before, kwa Jukwaa la Siasa kuzidiwa watazamaji na Jukwaa la Uchaguzi 2010 toka lianzishwe.
Mkuu, ndo ujue jukwaa hili lina umuhimu kuelekea Uchaguzi ili liwe na habari za ki-uchaguzi zaidi... Stay tuned, dakika si nyingi moshi mweupe utaonekana Dodoma
 
According to Mjengwa Blog baada ta raundi ya kwanza Shamshi Vuai Nahodha ameondolewa wamebaki Dr Bilal na Dr Shein
 
Breaking news!
Dr Mohamed Gharib Bilal nje,Dr Ali Mohamed Shein MGOMBEA ZNZ.

Shein.jpg
Hapa ni Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM na Makamu wa Rais Dr. Ali Mohamed Shein na Waziri kiongozi wa SMZ Shamsi Vuai Nahodha wakisalimiana katika viwanja vya makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo asubuhi. (Picha kwa hisani ya Blog ya Michuzi)
 
Back
Top Bottom