Elections 2010 Dr. Shein aibuka kidedea; kuiwakilisha CCM urais Zanzibar 2010

Elections 2010 Dr. Shein aibuka kidedea; kuiwakilisha CCM urais Zanzibar 2010

Kama Kawaida na mazoea, Wabara wamewachagulia wazanzibar mgombea, so Sad to them but that is politics
 
Kwa nini rais wa Zanzibar anachaguliwa toka Dodoma na sio Baraza la Mapinduzi?

Hili ni swali muhimu sana, maana wajumbe wa NEC almost three quarters wanatoka bara, kwa hiyo mgombea yeyote anayeungwa mkono na wajumbe wa bara lazima ashinde. It is very very unfair mgombea uRais wa SMZ kuteuliwa na NEC yote. Hilo ni kosa kubwa, uteuzi wa mgombea wa Zenji wangewaachia wa-Zanzibari wenyewe wateuwane.
 
BREAKING NEWS!! NI DR SHEIN

NI DR MOHAMMED SHEIN, amechaguliwa kuwa mgombea Urais Zanzibar. Amepata kura 117, Bilal 54, Nahodha 33

Kwa hisani ya mjengwa

Yaani BILAL amekuwa kama GAIDI, hatakiwi kuwa raisi ZnZ???///
Kusema UKWELI hili la sisi wabara kuwachagulia rais wazenj halifai hata kidogo. kwanza linawafanya hata wazanzibar wenyewe wamchukie rais wao.

CUF siwapendi, lakin bora maalim kuliko hhuyu mtumwa wa MAFISADI Dr Shein
 
Another puppet from SMT...come on Zanzibaris let all join hand to vote for Maalim Seif Sharrif Hamad that to do away withi this insect puppet like called Dr.Sheni
 
Kuna jamaa wa Bilal wameamua kuondoka usiku huu wanadai wanaondoka kwenda kuanza smear campaign against Shein anyway nadhani haya ni maneno ya mkosaji. In short sasa nadhani ni wakati muafaka tukaona uadilifu wa huyu mzee kama kweli muadilifu au ni just another puppet of CCM. Nampongeza sana yeye na familia yake.

Mkuu ushindi wa huyu jamaa ni message kubwa sana kwa makundi ndani ya CCM kuelekea 2015. Makundi hayalipi kama ililipa kwa JK basi bahati ya mwenzako usiilalie mlango wazi. JK anamchagua Dr. Amani Karume kuwa mgombea mwenza mchezo unaishia hapo. Ila itategemea na upepo wa mpaka mwisho wa mwezi huu, kama uteuzi huu utaonekana ni tishio kuelekea uchaguzi mkuu basi hamkani JK akamteua Dr Bilal kama mgombea mwenza.
 
yes but hapo ndipo wale mamluki ndani ya CCM wajue hicho ni chama cha mafisadi
 
Haya ,nashangaa wakati niliwapa matokeo tokea juzi kuwa piga ua Shein ni Chaguo la CCM wapenda amani ,na leo pia niliwapa za kuibuka kidedea kwa Shein,nawaambia tena kuwa Shein hana haja ya Uraisi wa Zanzibar ,ila ameonekana ni mtu wa kupenda amani mpole na hana choyo.

Kwa ufupi ameridhika, ila kuiweka amani Zanzibar huyu ndie ambae anafaa kuwepo, kwa maana kubwa kabisa ,inajulikana na wengine mnazo data kuwa kwa Zanzibar CCM haishindi hata wakiweka malaika

Jamani mtambue kuwa wanachotaka waZanzibar ni kubadili uongozi kichama na sio mtu , wanahitaji uongozi wa Chama kingine kuendesha serikali.
 
good news kwa kushinda Shein, sio BILAL tu kaanguka! wameanguka Janjaweed na wote waliokuwa tayari kuturudisha kwenye jino kwa jino.
Looking foward to to see free and fair election October 2010.
 
Katika hizo kura zote Wazanzibara wangapi?

Maana ilielekea kama wanzaznibara wanamtaka Bilali...Au ndo porojo za Urojo?

Sasa tutaona kama Bilali ana guts za kuwang'oa CCM Zanzibar kwa sababu kama ana wafuasi bai akagombee maana kuna vyama chungu nzima. Sio lazima CCM.

Shein ali[okuwa makamu wa rais jimbo lake la pemba lilichukuliwa na CUF which means aliibiwa Kura maana Zanzibar hawana Umalaya wa kisiasa, Kama mtu CUF ni CUF na kama CCM atapigia kura hata nguruwe wa CCM lakini sio mwana CUF.

Nangojea vumbi...
 
There are currently 250 users browsing this thread. (65 members and 185 guests)
 
Kwa wana CCM haya si matokeo mazuri sana kwa sababu yamezua mpasuko kati yao, mtu anaweza kuvumilia mara mbili but si mara tatu, hii ni mara ya tatu Bilal anafanyiwa Hila na Wabara. kwa upande wa Upinzani ni jukumu lao sasa kuhakikisha wanatumia mwanya huu kufanya kweli, si kwa kale margin kadogo tulikozoea, bali sasa wawapite CCM kwa kura nyingi tena watakazozipata kutoka kwa wafuasi wa Bilal.

CCM wanaweza kuepuka hili angalau kwa kumteua Bilal kuwa mgombea Mwenza, je ikiwa hivyo huyu si ndo naye atataka Urais 2015?
 
Wale wote (vijana wa zamani) tuliokamatwa PH 333 (Nuclear Physics) na Dr. Bilal pale Mlimani tumelipiziwa kisasi! te he he he.........
 
Hureeeeeeeeeeeeeeeeeee! Dr. Sheni kachukua nchi ya zenj.

Mimi niko nilikuwa ndani humu. Nawaambia mnaniona **** na kuniita malevi. Haya sasa, mlevi nani sasa?!
 
Kuna jambi hili la namna ya kumpata mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM, naamini inafaa liangaliwe upya.

Sasa hivi, rais wa Zanzibar sio Makamu wa Kwanza wa rais na hahusiani kwa namna yoyote na serikali ya muungano. Ni sahihi kwa CC na NEC kuhusika kwenye mchakato wa kumpata, lakini maamuzi ya mwisho wangeachiwa wenyewe. Haileti mantiki yoyote kwa mjumbe toka Kigoma kuhusika kumchagua mtu ambaye wala hata msaidia kwa lolote.

Wasipoliangalia hilo, ipo siku litawagharimu.
 
NI DR MOHAMMED SHEIN, amechaguliwa kuwa mgombea Urais Zanzibar. Amepata kura 117, Bilal 54, Nahodha 33

Kwa matokeo haya, ata Bilal angegombea na Nahodha bado angekuwa na shughuli pevu sana.
 
Ningependa mtu alete matokeo ya kura yalivyotokea Zanzibar ? Kama yupoe ,ngoja nichekelee ,nikisubiri vitisho vya wale ambao waliahidi ahadi lukuki kama mgombea wao akishindwa ,watafanya kweli ? Pili CUF haihitaji hata mmoja kati ya walioshindwa si wao si wafuasi wao,kama wanao 😛ound:
 
Haya ,nashangaa wakati niliwapa matokeo tokea juzi kuwa piga ua Shein ni Chaguo la CCM wapenda amani ,na leo pia niliwapa za kuibuka kidedea kwa Shein,nawaambia tena kuwa Shein hana haja ya Uraisi wa Zanzibar ,ila ameonekana ni mtu wa kupenda amani mpole na hana choyo.

Kwa ufupi ameridhika, ila kuiweka amani Zanzibar huyu ndie ambae anafaa kuwepo, kwa maana kubwa kabisa ,inajulikana na wengine mnazo data kuwa kwa Zanzibar CCM haishindi hata wakiweka malaika

Jamani mtambue kuwa wanachotaka waZanzibar ni kubadili uongozi kichama na sio mtu , wanahitaji uongozi wa Chama kingine kuendesha serikali.
...kaka Mwiba si vema kuwafananisha na Watu na Malaika Kiutendaji ...hata kwa lolote...Waache Malaika wamtumikie ALLAH pekee.
 
Ningeshangaa kuona matokeo tofauti. Bilal alipokuwa elimu ya juu enzi za Mwisho mambo yake yalikuwa si haba, na naamini ilikuwa ndio sababu kubwa ya Mkapa kutumia kila aliloweza kumzuia asipewe uraisi na Salmini Komandoo wa mchamba wima.
 
Back
Top Bottom