Yaani huyu mzee Slaa na mwenzake Lipumba sio watu wa kuwaamini kabisa. Hao ni wazee wa kuchomoa betri dakika za jioni kabisa. Na Mungu alivyo fundi sasa hivi sio Lipumba au Slaa anayeweza kuzungumza kwenye vyombo vya habari halafu watanzania wakaacha shughuli zao wakae wawasikilize. Sitawashangaa CHADEMA wakimpokea tena ila nitawashangaa wakimpa uongozi. Huyo Mzee Slaa apokelewe tu kama mwanachama wa kawaida lakini asipewe hata uongozi wa tawi abaki mwananchama wa kawaida kabisa. Kwanza huko CHADEMA amesahau nini au ana jipya lipi. Na kama uongozi utampokea na kumpa uongozi basi itadhihirika wazi upeo wa uongozi na kuchanganua mambo ni mdogo kiasi gani.
Kauli zake tata juu ya CHADEMA zinamuhukumu, mara ndani ya CHADEMA kuna kundi la utekaji, msaidizi wangu alitekwa na watu ndani ya CHADEMA, nawashangaa wanaosema Mbowe sio gaidi, Inawezekana Lisu kashambuliwa na CHADEMA wenyewe n.k. Huyo mzee ni mtu mnafiki sana na anapenda sana visasi. Hebu fikiria yeye ndiye aliyemleta Lowasa CHADEMA according to Lisu halafu alipoona Lowasa kapewa nafasi ya kugombea uraisi akaondoka CHADEMA kwa hasira na kuanza kuitukana CHADEMA na Mzee Mbowe. Haya akaenda CCM akapewa ubalozi alipoondoolewa tu ubalozi akaanza kuitukana serikali, CCM na akaenda mbali zaidi kila siku kumzushia raisi mambo ya uongo. Yaani mara nyingi hata ukimsikiliza unaona kabisa ana chuki binafsi na Mbowe na raisi kitu ambacho kinamuondolewa sifa ya kuwa kiongozi mzuri kwani anaweza kabisa kujenga hoja bila ya kuingiza chuki binafsi.
Nafikiri watu waliopo karibu naye au hata watoto wake wangemshauri kwa umri aliofikia aachane kabisa na siasa amrudie Mungu afanye toba kwa usaliti wa kiapo cha upadri na kuwasaliti watanzania.
Ni mtizamo tu.