Pre GE2025 Dr Slaa: Kilichonitoa CHADEMA 2015 sasa hakipo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Slaa hakuwahi kurudi CCM, alichofanya ni kuachana na siasa lakini hakuwahi kupewa kadi wala kuvaa nguo za CCM wala hata kwenye makutano ya CCM hakuwahi kushiriki!
Lakini ana kadi ya CCM na yey mwenyewe alikiri hilo hadharani
 
Namkubali sana Dr Slaa, alivyoondoka chadema nilikereka sana... kama atarudi itakua undamaged sana..
 
Tulishindwa kivipi mkuu?
Aliye waondoa walinzi area D ni nani siku ya tukio, askari hupangiwa zamu Kwa mpangilio maalum, (duty roster), nani aliwapangia zamu siku ya tukio

duty roster -orodha ya majukumu

Swali fikirishi je Dr Silaa anaweza kuingilia majukumu ya polisi kuhusu duty roster kwa kuwaondoa walinzi kwenye lindo?
 
Lakini ana kadi ya CCM na yey mwenyewe alikiri hilo hadharani
Kama ana kadi ya CCM aliipata miaka mingi sana kabla haijaingia chadema , kadi kama hiyo hata Mbowe anayo!
Watu wengi waliokuwa CCM kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi walipoingia vyama vya upinzani kadi za CCM walibakia nazo!.
 
Inachanganya
Lissu alisema "...aliyeshauri Chadema 2015 imchukue Llowasa ni W. Slaa"
Swali: Kama Slaa ndiye aliyeshauri? Vipi amkimbie?
Exactly, kwa kauli Lissu aliuambia umma kuwa Slaa ndiye aliyeshauri wamchukue Lowassa ila kibao kikageuka baada ya 'madame' Mushumbusi kumkasirikia kwa move hiyo ya kumkosesha uwezekano wa kuwa first lady. Things changed drastically na Slaa akapiga U-turn 180Β° kutokana na pressure ya madame Mushumbusi.
 
Mushumbusi balaa. Siku anaona picha ya Lowassa ndani ya ofisi za Chadema usiku Slaa aliporudi nyumbani hakufunguliwa geti. Yule maza kweli mhaya!
 
Huyu mzee hata afya yake haimruhusu kufanya Siasa.
Kwanini hataki kupumzika,
Anatakiwa akae alee wajukuu sasa abaki mshauri tu.
Wamemuachia kwasababu ni mzigo hata kumfunga.ye atadai hawamuwezi
 
Dr Slaa amechangia kukuza viongozi wengi CDM na kuwajenga kina Zitto, Mnyika, Lema, Mdee nk nk!

Sasa akijenge chama Kwa JASHO na Damu ,iweje tena akihujumu?

Waliohujumu chama wamekataliwa kwenye uchaguzi uliopita.

Dr Slaa ni victor!
Chawa wa Mwendakuzimu na msaliti aliyesaliti na kupambana kukihujumu chama katikati ya mapambano ni mtu asiyefaa, imagine mtu wa aina yake aliyegeuka akawa chawa wa Jiwe kama ndiye angekuwa mwenyekiti wa chama kwa sasa kingeshajifia yaani hafai hata kwa kurumangia. Bora hata Lowassa alivyorudi CCM hakuwasagia kunguni CHADEMA aliendelea tu na maisha yake mengine, once a traitor always a traitor.
 
Karibu tena CHADEMA Dr.Slaa mpigania HAKI za Wananchi.🫑
 
100%βœ“
πŸ‘πŸ‘
I second your analysis big time.
 
Inaonesha ni mchanga sana siasani. Siasa haipo hivyo unavyodhani ndugu, siasa ni watu na yeyote yule anayekuletea watu kwa wakati sahihi unampokea.
 
Kumbe wewe ulikimbilia kuni quote kwenye comment namba 2 bila kuelewa nilichoandika.

Niliandika kwamba Dr Slaa alisema kuwa kwa habari za ndani alizokuwa nazo ni kwamba ni Chadema wenyewe ndio walimpiga Lissu risasi na kumuangushia jumba bovu raisi Magufuli.

Sasa mtu wa aina hiyo kwa mujibu wa kile alichoongea ni kwamba ana taarifa nyingi kuhusu tukio lile. Hivyo anaweza kwenda polisi kuwataja hao waliopanga mikakati ya kumpiga Lissu risasi ili kumuangushia jumba bovu Magufuli. Na kama anaona hawezi kwenda polisi basi atoe taarifa hizo kwa Lissu mwenyewe ambae ni kiongozi wa chama ili aweze kuwachukulia hatua wahusika.

Na hapo kwenye swali lako fikirishi, labda linakufikirisha wewe mwenyewe. Kwa sababu kama kuwataja wahusika ni kuingilia kazi ya polisi, basi tayari alikuwa ashaingilia kazi hiyo kitambo kwa kukimbilia kusema kuwa Chadema inahusika na shambulizi la Lissu kabla hata ya polisi wenyewe kutoa ripoti ya waliomshambulia Lissu.
 
Inaonesha ni mchanga sana siasani. Siasa haipo hivyo ubavyodhani ndugu, siasa ni watu na yeyote yule anayekuletea watu kwa wakati sahihi unampokea.
Wewe ndio mchanga mno katika mambo ya siasa nchini na duniani kwa ujumla. Siasa ni kama biashara, kuna faida na hasara. Sasa hauwezi kulazimisha kufanya biashara ambayo unaona kabisa itakupa hasara hapo baadae.

Nafikiri kilichotokea kwa Lowassa, Sumaye na Lazaro Nyalandu haukukiona kwa sababu ulikuwa bado mdogo haujaijua siasa vizuri. Hao walijifanya kuhamia Chadema hivi hivi kama anavyojifanya kuhamia Dr Slaa. Chadema nao bila kujua ikakimbilia kuwapokea bila kujua mikakati iliyokuwa imepangwa na CCM kupitia wanasiasa hao.

Jamaa waliingia wakakivuruga chama baada ya kumaliza wakarudi kule kule walipotoka na lundo kubwa la madiwani na wanasiasa kadhaa wa chama. So na huyu ana lenga kufanya hivyo hivyo. Ajiunge halaf asipopitishwa kugombea uraisi akurupuke tena na kundi lake kurudi CCM huku wakikishtutumu chama kwa kutosimamia demokrasia vizuri nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…