Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Status
Not open for further replies.
......leo nitakula na kushiba.....nitalala na kupata usingizi maana ninaye mgombea urais wa kumchagua! kama wapinzania wa kweli (maana wapo vibaraka wa CCM) watakomaa wasiibiwe kura, wabunge wa upinzani naamini wataongezeka mwakani.
 
Hii kwangu siyo habari ya kujivunia maana nafahamu kabisa umuhimu wa Slaa kuwa Bungeni umepotea. Nadhani lengo lake ni kupumzika ubunge kwa muda.

Ukombozi wetu ungeanzia Bungeni kwa CUF na CHADEMA kuingiza wabunge wengi. Ina maana nguvu yao kubwa ingeelekezwa kwenye Ubunge. Sasa tena turufu yetu inajitoa!

Ni vigumu kuingiza wabunge wengi bila kuwa na mgombea uraisi atakayefanya kazi ya ziada ya kuwanadi wagombea kwenye ubunge. Dr Wilbrod kazi yake ya ukatibu ni mtendaji mkuu wa chama hivyo si kweli kuwa atakuwa kijiweni kama hatashinda. Vile vile maamuzi mengine ndani ya Bunge yanahitaji msimamo wa chama hivyo Dr Slaa ataendelea kutoa mchango wake bungeni akiwa nje ya pazia (Indirect)
 
Woooow..what a good news!...Huyu Mkuu hata ukimtazama sura yake anapoongea jambo unaona kwamba anamaanisha!...Ni nafasi ya pekee kwa watanzania kuona mabadiliko makuu katika uongozi wa nchi na kupata matarajio mapya ya maisha!

Nitawahi kwenye foleni siku hiyo!
 
Baraza kuu la CHADEMA litakapomuidhinisha Dr Slaa kugombea Urais limpe pia uenyekiti wa chama hicho ili kumwongezea nguvu.
 
Nimeamini kuwa CHADEMA ni chama makini sana.
Hawapeani maaraka bali wanaweka maslahi ya nchi kwanza.

Sasa tuache porojo za kupongezana, TUINGIE KAZINI kuelezea watanzania wenzetu kwa nini CHADEMA ni chama makini kwa ushindi oktoba.
Tuwaelimishe wake zetu, tuwaelimishe vijana wetu pamoja na wavuja jasho wa nchi hii kuhusu umuhimu wa kuwapa watanzania wenzetu CHADEMA nafasi ya kutekeleza ilani yao kwa kuliongoza taifa kiuchumi kwa miaka 5 ijayo na ikiwezekana milele.
 
Nipo huku Mkoani Lindi wilaya ya Kilwa.
Kila sehemu nnayopita naona vikundi vya watu wanadiscuss juu ya uteuzi wa Dr. Slaa.
Kwa mbaali naanza kupata picha ya mabadiliko.
lakini sijui kwani watanzania hawatabiriki, wakishapesha kofia na khanga basi wanabadili mawazo.
 
wakuu ndiyo natoka misituni - nafungua internet - siamini hii habari hebu niperuzi maana ina tumaini jipya - kwangu hii ni breaking news.... DR slaa kuwania urais 2010 kupitia CHADEMA - safi saaaaanaaaa.....
 
Very gud challenge for rulling party. I support Dr.Slaa since then, and that is a great news all over.

Hii inataraji kuongeza wabunge pinzani mjengoni na kuongeza ugumu wa rulling party kuiba kura, kwa sasa
najua wanatayarisha kura zaidi za wizi mbali ya zile walizopanga kuiba, as washaona bumps kadhaa mbele.

Ujinga na umaskini ndio mjaji wa rulling party, so don't be party of them. Value u'r vote for voting for change.

May God Bless TZ.
 
Lipumba wa CUF na Mtamegwa wa TLP fanyeni kile Watanzania wanachotarajia mfanye leo. Sio tu mtakuwa mmejiwekea historia ya aina yake bali mtakumbukwa daima dumu
 
Tumsubiri mbeba matusi wa ccm (makamba) aanze kutapika mamneno machafu dhidi ya mgombea wetu. sisi tunamsubiri kwenye kura tu!
 
Ieleweke kuwa, Kikwete, Slaa na Lipumba et all, bado SI WAGOMBEA bali WATEULE wa vyama vya siasa. Tume ya Uchaguzi itawathibitisha tarehe 19 August 2010.

Tanzania ina majimbo 239 ya uchaguzi, itatakiwa msajili wa vyama vya siasa akusanye taarifa za kukubalika kwao kutoka kanda za Tume hiyo ambazo zipo Arusha, Mbeya, Mwanza na Dar es Salaam. Mtwara na Lindi wana mwakilishi wao. Vyama vya siasa na wagombea watatakiwa kuwasilisha mapato na matumizi ya vyama hivyo kwa DED au kwenye ofisi za kanda ili chama kiweze kukubaliwa kuwa mgombea wake anaweza kushiriki uchaguzi kwakuwa chama kinajiweza kifedha. Mpaka sasa BADO!

Ieleweke kuwa msajili wa vyama anaweza kutibua hali ya hewa endapo mgombea hatothibitika kuweza kutekeleza sharti hili, na mbaya zaidi endapo tume ya uchaguzi itakuwa imeondoa uhalali wa mgombea itatakiwa msajili amfungulie kesi na chama kitakuwa kimepoteza nafasi ya kugombea nafasi ya urais/ubunge. Siku 180 baada ya uchaguzi itatakiwa mgombea ambaye ameshinda nafasi aidha ya ubunge au urais atatakiwa kuwasilisha ripoti ya mapato na matumizi ya kampeni zake ili iweze kuwekwa bayana gharama zilizotumika kwa mujibu wa sheria ya matumizi /gharama wakati wa Uchaguzi.
 
Nimeongea na Tendwa na anadai mwaka 2005 alichukua hatua ambazo baadae ziliungwa mkono na NEC, anasema hawahawa NEC wanaweza kulishughulikia suala la CCM kuanza kuweka mabango barabarani. Anakiri ni kosa kubwa, anasema hata vyama vya siasa vimelalamikia TOT kuanza kusambaza nyimbo zake zinazosema TUWASHIKE TUWACHANECHANE TUWATUPE.

Anakiri ni kweli kuwa haikubaliki kabisa kimsingi na anasema kuwa hoja ina-valid, na analichukulia hatua kwa kuwasiliana na Tume ya Uchaguzi. Anasema kauli za kuchanachana si za kiungwana na wapinzani wamelipigia kelele sana. Anasema CCM wao wanadai ndiyo siasa lakini yeye anadai ni kuwa si uungwana hata chembe.

Amesisitiza kuwa Slaa ni mteule wa CHADEMA lakini si mgombea rasmi, same for JK
 
Invisible,
Ungemuuliza haya yanayofanywa na CCM ikiwemo kutambulishana hadharani kule Jangwani, Pemba na kwingineko yangefanywa na CHADEMA, CUF, TLP angeendelea kunong'ona na kulalama akiwa ofisini? Nilidhani anayo MAMLAKA ya KIKATIBA kuyasimamia haya kumbe ni hadi awasiliane na NEC!?
 
Tendwa tumeshamzoea na hizi porojo!! hili litaisha hivi hivi!
 
Wera weraa weraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa safi CHADEMA JUUUUUUUUUUUUUUU, KURA YA NDIO KWA DR. SLAAA mpe kura yako leo kesho akuondoleee ufisadi WERAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
 
Invisible,
Ungemuuliza haya yanayofanywa na CCM ikiwemo kutambulishana hadharani kule Jangwani, Pemba na kwingineko yangefanywa na CHADEMA, CUF, TLP angeendelea kunong'ona na kulalama akiwa ofisini? Nilidhani anayo MAMLAKA ya KIKATIBA kuyasimamia haya kumbe ni hadi awasiliane na NEC!?
Nimebahatika kumwuliza hivyo, akasema tumtumie maswali au tutume mwandishi wetu Ijumaa wiki hii ili ajibu maswali yote na ikibidi kama tuna mapendekezo atatoa ufafanuzi kwa mapana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom