Pre GE2025 Dr. Slaa: Ni dhahiri Milioni 150 zilizotolewa na Rais Samia zimeingia kwa sura ya kampeni, anayebisha abishe!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Halafu aliyezipokea na kutangaza ni Mbowe, kila kwenye fursa hakosi.
 
Huyu jamaa bana zile milioni 100 zilizotolewa kanisa katoliki babati mwezi wa 10 mwaka jana mbona hakusema? Au kwakua hizi zimepelekwa KKKT kwahiyo kimemuuma?
 
lakini mama samia ataingia peponi ni mkarimu sana sijawahi kuona Rais yoyote anaetoa pesa zake za mshahara na marupurupu kujenga barabara nchi nzima mahospitali nchi nzima shule nchi nzima na kutoa pesa za ujenzi wa kanisa na kutoa pesa kwa magoli na kujenga mwendo kasi kwa mshahara wake sijawahi kuona huyu ni mtu wa mbinguni, maana kila mradi unaojengwa utasikia asante mama kwa msaada wako au bila mama tusingepata hiki
 
mama sasa ana deal na kkt kaachana na wapigaji na wazinguaji na wanaojifanya wako juu ya sheria wakatoliki mama wakumbuke na wasabato
 
Mzee Dr Slaa ni muda wako wa kupumzika na kukaa kimya kama mwenzio Lowasa!! Hatutegemei jipya Toka kwako!! CCM waliokurubuni ukautosa upinzani wamekutumia na KUKUTUPA! Upandacho ndicho utakachovuna! Tulia uvune ulichopanda Mzee!! Pole Sana!
 
Yeye ali honvwa shilingi ngapi kuharibu uchaguzi?
 
Sawa na yeye atoe badala ya kulalamika.Mkono mtupu haulambwi.

Uzuri aliyezitangaza ni Mbowe 🔥🔥
 
Good uitishwe mdahalo wa wazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…