Pre GE2025 Dr. Slaa: Ni dhahiri Milioni 150 zilizotolewa na Rais Samia zimeingia kwa sura ya kampeni, anayebisha abishe!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sasa hapo anaomba kura? Kwa akili yako mpaka 2025 hao wachaga watakumbuka km kanisa lao lilichangiwa 150,000,000/=. Kiukweli hiyo michango ni mikubwa, hao washauri wake wamshauri km anawasikiliza. Kweli hizo ni pesa za umma kuichangia kundi moja tena likanisa la kijijini ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Hivi kwanini Rais achangie ktk vitu km hivyo? Huko ni kujishusha hadhi yake, sisi tunashindwa kati ya kuchangia km Samia na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
 
Dkt slaa wivu na choyo hataki kukubali jema afanyalo mwengine!
 
Slaa ameongea kitu sahihi kabisa, lakini Yuko kiunafiki zaidi. Kipindi Cha dhalimu Magu akiwa kwenye ulaji, alikalia kimya tabia hizohizo kisa alikuwa kwenye mlo. Hoja yake ni sahihi sana, ila Hana uhalali wowote wa kuiongea.
 
Slaa ameongea kitu sahihi kabisa, lakini Yuko kiunafiki zaidi. Kipindi Cha dhalimu Magu akiwa kwenye ulaji, alikalia kimya tabia hizohizo kisa alikuwa kwenye mlo. Hoja yake ni sahihi sana, ila Hana uhalali wowote wa kuiongea.
Hapa tunaangalia Hoja siyo mtoa Hoja!
 
Dk. Slaa anazeeka vibaya.
 
Yaani Slaa anawaza kula tu, mtu hawezi kuishi kwa mkate tu....anaona wivu Mwenyezi Mungu kuchangiwa fedha kwa ujenzi wa nyumba yake, tena padri....
 
Jamaa mdini sana huyu. Anatisha kwa udini
 
Siasa bhn! Huyu mwamba kipindi cha jiwe alikuwa anakula kwahiyo alikuwa haongei... Akiongea ss anasifia aliempa msosi na kuponda kule kwingne
Kanuni za uongozi wa pamoja za "collective responsibility" zinamkataza mtu aliye sehemu ya serikali kuikosoa serikali hiyo hadharani wakati bado akiwa sehemu ya serikali hiyo.

Na inawezekana alikuwa anaikosoa serikali ndani ya serikali kwa kufuata vikao, kama inavyotakiwa na kanuni za "collective responsibility".

Sasa ametoka serikalini, hafungwi tena na kanuni hizo, anaruhusiwa kuisema serikali hadharani. Anaisema.

Pia, hujajibu hoja, umemshambulia mtoa hoja.

Hii ni logical fallacy, ad hominem.

Mara nyingi hufanywa na watu wasio na hoja kujibu hoja.
 
Chadema nao wanalipa Kodi, hela yote ya Million 150 inayosemwa ya mama Samia ni mchango kutoka kwa Watanzania wote, kodi zetu na tozo lukuki mnazotutoza
Toeni ruzuku mnazozipata mana nazo pia ni kodi za watanzania
 

Kila anachofanya mwanasiasa anafanya kwa sura ya kampeni, hata Mbowe huo uchangishaji ameufanya kwa sura ya kampeni.

Wanasiasa maisha yao yote yanaangalia uchaguzi.
 
Kwa mujibu wa Mbowe, fedha zile zimetoka kwa familia ya rais Samia....

Harambee tunachangisha mtu yeyote bila kuangalia status yake.

Waziri Mkuu amechangia
Tundu Lissu amechangia
Halima Mdee amechangia
Bulaya amechangia
Mbunge wa Hai amechangia
Na wengineo!

Mama akitoa pesa kununua magoli yale ya Simba na Yanga hatuoni shida, leo amechangia ujenzi wa kanisa tayari maneno yameanza!

Acheni Nongwa!
 
Wakati amejiuzulu Chadema alikuwa bado hajawa sehemu ya serikali, mbona alitapika nyongo kweli kweli pale Serena hotel dhidi ya Chadema na baada ya hapo akapewa ubalozi.Huoni kwamba ilikuwa ni Campaign dhidi ya Chadema na Lowasa ambaye ni KKKT na leo tena anajitokeza kushambulia mchango uliotolewa na Rais kwa vile haukwenda RC ambako huwa hakosoi chochote.Alichosema ni kweli lakini huyu mzee ni mnafiki wa kupitiliza,mdini na mbinafsi ambaye hata leo akipewa cheo iwe Chadema ama CCM ananyamaza kimya.Lissu Ndiye mwenye haiba ya kusimamia anachikiamini lakini kwa huyu Dr. Slaa hapana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…