Wasomali wengi madhehebu yao ni ya Waislamu poa kama hawa wa kule Markaz Gongolamboto hapa Dar.
Alshababu wanasema kwasababu Wasomali wanafuata mafundisho ya Abdukadir Jailani kwamba na wao ni Makafiri.
Alshababu ni dhehebu la Salafi kutoka Saudi Arabia.
Zingatia sana hapo kwenye Red
Moja ya misingi ya madhehebu ya kisalafi ambayo ni mwiba dhidi ya MAGAIDI (sisi masalafi huwa tunawaita makhawaariji) ni kuwavumilia watawala pale wanapokosea na kuwapa nasaha na ushauri na kuwakosoa kwa upole na usiri kama vile Allaah alipowapa utume Musa na Kaka yake Haruna kwenda kwa firauni ambaye alikuwa mtawala muovu wa Misri kipindi hicho aliwaambia wakazumgumze nae kwa maneno laini.
{ ٱذۡهَبَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ }"
[Surah Ṭā-Hā: 43]
Nendeni kwa Firauni. Hakika yeye amepindukia mipaka.
{ فَقُولَا لَهُۥ قَوۡلٗا لَّيِّنٗا لَّعَلَّهُۥ يَتَذَكَّرُ أَوۡ يَخۡشَىٰ }
[Surah Ṭā-Hā: 44]
Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa."
Huo ndio mwongozo wa uislamu tangu enzi za Nabii Musa na Firauni hadi kitakaposimama kiyama.
Uislamu unaharamisha uchochezi, uasi na mapinduzi dhidi ya watawala hata kama wamekosea bali uislamu unataka watawala wapewe nasaha, kwa upole ,na kwa usiri siyo kutaja makosa ya watawala kwenye mimbari za misikiti au mbele ya vyombo vya habari.
Sasa Alqaida na ndugu zao hawalitaki hilo na ndio maana MTAWALA AKIKOSEA KIDOGO TAYARI WANAMUITA KAFIRI NA KUANZA MANENO YA UCHOCHEZI NA KUHAMASISHA MAPINDUZI DHIDI YAKE kwahiyo Ugaidi na usalafi ni vitu viwili tafauti sana.