DRAFT ONLINE: Sisco vs Mkulima

Nazani nilijitaidi kuelezea kwamba mkataba huu Kwa Ronaldo utakua mgumu Kwa mkulima..kama upo playok utakua umeona sana game mkulima vs ashkelon zinavyokua..baada ya Ronaldo kumshtukia mkulima anasema live mkikutana kwamba ukicheza nae ckuzote usiishambulie kwakua iyo ni program..
Kma unamjua Sisco yeye hua ni offensive sana anajua kusaka ata ingerudiwa Leo Sisco vs mkulima bado atafungwa tuu..

Kwa wanaomfaham cr7 wanajua uwezo wake wa kuepuka mabao magumu..Kuna game kama tege ya 3 ivi nusu cr7 aende na maji adi mkulima akatoa kasmile icon akijua goli ila alichomoka..
Huu mkataba mgumu sana Kwa mkulima..

Cr7 anasema wadau waweke mzgo wakutosha kama wanataka aende kisu kisu na mkulima..aingie chimbo kwenye chat playok Ile saa 10 baada ya game ya mwisho akakumbusha tena mzigo uwe wa kutosha[emoji28][emoji28]
 
Miaka ya 2000 , KWENYE Madraft mafundi walikuwa MANGWELELE, SHABAN KATOTO,BEDUI ,KINA MAREHEMU MCHAFU

Ronaldo ndiye alianza kuwafunga na kutoa dhana ya kuwa wakubwa pia wanaweza kufungwa
Kweli kabisa hao wote wakali na wanaweza kufungwa Noel CR7 NDULI ISSA SiSKO hawa ndio mabingwa ispokuwa huyu mkulima mm sio shabiki ake siwezi shabikia kitu nisichokiona hata siku moja live wakati uwezekano wake kutokea live katika benchi upo na yeye hataki
 
Miaka ya 2000 , KWENYE Madraft mafundi walikuwa MANGWELELE, SHABAN KATOTO,BEDUI ,KINA MAREHEMU MCHAFU

Ronaldo ndiye alianza kuwafunga na kutoa dhana ya kuwa wakubwa pia wanaweza kufungwa
Ronaldo aliingia kweny game kibabe sana kwasababu kijiti Cha ubingwa kilitoka Kwa mangwelele kikaingia Kwa Shaban katoto..wakiamini Shaban katoto hafungiki..siku akapata chance nae ndo apo jina la Ronaldo likajulikana.. alishinda 3-0..Kila game baada ya apo katoto anatafuta sare..
Ndo maana adi leo katoto hamkubali cr7 yy yupo na kina noel..
Ila kwangu one among of consistent player ni nduli..nduli ndio mtu mbaya sana kimya kimya alikua akiingia kweny nyavu za katoto enzi zake,,kaingia sana Kwa cr7,,ila Sasa anapata shida Kwa Sisco kwasababu wanadiscuss wote mabao..
 
That's why hataki kujionyesha
True chukua simu mbili weka gemu ya draft moja ili na jingine kama dalmax kisha omba mechi na mtu akianza yeye kucheza na wewe cheza hivyo hivyo kete aliyo sukuma kwenye dalmax kisha dalmax itacheza kete itakayo chezwa na dalmax na wewe icheze hiyo hiyo hivyo huyo mpinzani wako atakuwa anacheza na kompyuta akijidanganya anacheza na wewe.
 
Ninacho kuambieni ni cha kweli huyo mkulima usikute hata draft ajui kucheza ila anatumia programu za simu au komputa za draft ila mimi aniwezi hata akitumia hiyo mbinu nimecheza madraft magumu yote ya kompyuta
Nataka nikujaribu twende tanzania draft online tucheze mm natumia dalmax ww usitumie nione ukitoka salama aisee nitakukubali na nitakuwa mwanafunzi wako
 
Scars umeona zile sare alipokuwa anasakwa mkulima na katoa sare wakati sie wengine tunapanga pale goli yaan kama kaniacha hoi mkulima aisee yule jamaa ni mtu hatari
Mkulima SiO mtu ni zombi aka robot! Mara waseme ni program anatumia ila Ukweli kashindikana kwasasa na hataki sura Wala jina lake halisi lijulikane na matula Tula wote wenye majina bongo!

Hakuna stori ya mkulima kufungwa na matula Tula wote wa manyanya kina Mangwelele Sisco Ronaldo sijui meno ya kenge au Mamba msomali na wengine!

Mashabiki wake tupo wengi inafaa ajitokeze ajulikane avishwe taji na kuua stori za matula Tula wa manyanya wenye majina makubwa Huku draft hawajui!

Mi namuandaa bingwa mpya wa draft dogo mbishi sana simtaji kwa Sasa! Ila Yuko Chanika! Nataka kuanza kudhamini mapambano yake!

Mangwelele ni senior ninamfahamu ila sijaona akicheza zaidi ya Kufundisha matula wenzake wa manyanya ambao huwatumia jamaa Zangu flani madraft yaliyorekodiwa namna ya kukabili Kila kete anayoanza nayo mpinzani. Ukweli matula Tula wa manyanya wako mbali kwenye kopi za draft we unaenda kucheza nao kawaida wao wanacheza kwa kopi Kila kete utakayosukuma wao wanajua kete ya kujibu wamekariri mabao yote kichwani matula Tula wa manyanya ni kiboko huwafungi hata uje umeroga!
Ila mkulima ni kiboko yao matula wote tz!
 
That's why jana tumeshangaa kweli kashindwaje mkulima kushinda michezo 24 kwa ronaldo au nae kiwango chake kimeshafika mwisho au watu washamujulia maana ndani ya siku 2 waliwapiga Noel 3 na sisco 2
 
Yah Nduli Ni timu moja na Sisco ,

Juzi kapigwa Fainal mbili Zote na Sisco
 
Dalmax mbona Linapigwa SUTI kila Siku na linakuwa 100%
 
Ninacho kuambieni ni cha kweli huyo mkulima usikute hata draft ajui kucheza ila anatumia programu za simu au komputa za draft ila mimi aniwezi hata akitumia hiyo mbinu nimecheza madraft magumu yote ya kompyuta
Sasa anatumia program Gan hiyo,

Maana Kama Dalmax watu wanalibutua hata Sare halipati
 
Wewe Ni mdau mkubwa wa Draft
 
Zuga

Scars

Taarifa ya Makubaliano

Baada ya majadiliano Mazito kati ya Tajiri Java, Mtu kati, na Viongozi wa Cr7 na hatimae wamefika makubaliano,, Iko hivi viongozi wa cr7 hawajaikataa mechi ya Dogo Sisco bali walitaka matakwa yao yatimizwe moja ya sharti lao kubwa ni zawadi iongezwe kidogo ambalo kwa Hakika Boss Java amekubali ombi lao na amejazia kishungi kutoka zawadi ya 250k hadi 300k.

Vile vile Mgawanyo wa hiyo zawadi ni kama Ifuatavyo ; winner 200k na looser ni 100k,, Boss Java amesema Afya tu kwake sio kesi kikubwa watu wapate burudani ya kutosha .

Viongozi wa Cr7 wamekiri sasa Cr7 yupo teyari kupambana na Sisco na ikiwezekana Viongozi wa watu huru nao wathibitishe ili Tangazo la mechi lianze kutembea,, Ikumbukwe tu Cr7 amejizolea umaarufu mkubwa baada ya kumzuia MKULIMA ngoma 24.

Naomba kuwasilisha ,,,,,,,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…