Ndio tatizo letu watanzania, kuendekeza ushabiki wa simba yanga, Chadema na CCM hata kwenye ishu nyeti. Ukubwa wa nchi hauna impact kwenye ubora wa kivita. Israel ni taifa dogo sana, angalia anavyosumbua mataifa makubwa ya kiarabu duniani. Angalia Israel inaingia mara ngapi kwa Iran, angalia population yao na iran.
Vita sio ukubwa wa nchi, vita ni mbinu za kimedani, ubora wa silaha, ari ya wanajeshi na intelejensia imara. Ikiwa jeshi lako, lipo wazi kila mtu anajua una nini, mpo wangapi na wapi, basi kukupiga ni jambo la kawaida tu.
Nasisitiza, sio rahisi kuwapiga Rwanda kwa kukurupuka mnaweza kuunguzwa na moto msioujua umetoka wapi.