Dstv wapandisha bei ya vifurushi kuanzia Septemba 1 mwaka huu

Mambo ya pricing haya mtu hawezi kuona hii ni 20000 bali ataona 19900 toka 19000 bomba, 29900 bali ni 30000 toka 29000 family nk vifurushi vya dstv wanabadilika kila wakati sijui ni vigezo gani wanatizamia,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MM tv yangu ni smartphone
 
Mkuu nimepata Canal Dish na be yao ni laki 300k nimeshawishika kuinunua maana hii Dstv Gharama inanishida kabsa, vip ushawahi kuitumia au kupata changamoto yeyote? Maana nimeona ina sehemu ya HDMI bila shaka ina channel za HD.
Canal ni Equivalent ya Dstv kwa Nchi zinazoongea Kifaransa. Ipo fresh, sijaitumia Nyumbani ila Vibanda umiza nimeiona sana, changamoto yake ni signal, fanyia utafiti eneo uliopo.

Na kama wanavyosema wadau 300k ni kubwa yanapatikana around 100k mpaka 200k, search humu ndani wapo wauzaji.
 

Hapa Shop nimeambiwa mwisho 250k kuiseti 20k so inaenda kwenye 270k. Hii dstv nimechoka kwa gharama japo sifanyii biashara ni kuweka ndani kwa ajili ya burudani yangu binafsi.
Haya maswala ya kulipia 44k EPL Kwa Dstv na 84k nimechoka aisee
 
Mkuu Canal+ kwa sasa wameongeza coverage yao,ili mradi umpate fundi mwenye uzoefu nayo kuifunga.
 
Ni vizuri kama wangeshusha gharama zao ili ziwe chini sana halafu wateja wangekuwa wengi sana.
Kama Dstv huko South Afrika gharama ziko chini sana, kwanini Tanzania ishindikane?
Unajua kuna vitu huwa havimake sense ila wahusika wanakuwa wanapambana na mazingira fulani yanayowakwamisha kufanya maamuzi mazuri.

Unaweza kuta jamaa kuna makodi ya kipuuzi wanapewa na tozo za ajabu za TCRA kiasi kwamba wakishusha bei wanajikuta wanakula hasara.

Mazingira ya sasa kibiashara yamekaa tofauti sana.

Nashindwa kusema mazingira ni mabaya au mazuri ila ninachojua ni kuwa mazingira kwasasa si kama kipindi cha mzee baba mkwere ambapo watu walikuwa na deal za mamilioni kwa siku.

Mtu analipa king'amuzi package ya premium kwa mwaka.......ila kwa sasa mmmmmmhmn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…