Atlantic Star
JF-Expert Member
- Feb 22, 2023
- 539
- 1,696
......shida nyingine ni kwamba channels zinasitisha mikataba, kila baada ya miezi miwili utasikia channel fulani itakuwa closed ifikapo siku fulani.....Na bado, cha maana hakuna wamebaki na EPL tu.
Nilikuwa siikubali Azam ila nitahamia, kama ni EPL nitastream live basi.
kupitia compact unaweza kutazama epl na baadhi ya mechi kubwacompaq ina nini? Natumiaga shangwe
Hapa utakua umepuyanga kidogo boss..kwenye nchi 50 barani Afrika.
mkuu wangu mungu anakuonaDu! ujinga huu waliofanya DSTV ni zaidi ya ule ujinga wa Magufuli kuwakamia wafanyabiashara hadi wakafunga biashara na kupelekea uchumi kudorora. Na baada ya uchumi kudorora akaamua kukimbilia kukopa matrioni ya pesa hivyo kuiingiza nchi kwenye mzigo mkubwa wa madeni unaotuumiza vichwa hadi sasa. Mungu anamuona.
DSTV kwa ujio wa Streaming wanapoteza wateja kila kukicha Afrika kote.2024 Netflix na Amazon Prime wanaanza Services zao South Africa ambako ndo base kubwa ya DSTV kwa Afrika nzima.DSTV Wana miaka 3 mbele kabla Awajafungasha vilago na kutoka kwenye ulimwengu wa Pay TV.Either na yeye aanzishe Streaming Services na aje na Bei nzuri vinginevyo atoboiVifurushi vya DStv zilipanda Kwa Africa nzima sio Tanzania Tu hii imetokana na kupanda Kwa Dola hata hivyo wao wenyewe DStv wapo mbioni kubadilisha Makato ...
Toka December wameanza kutoa ofa mbalimbali za vifurushi
Kwa maelezo yako ni kweli DStv anatakiwa kujipanga upya..DSTV kwa ujio wa Streaming wanapoteza wateja kila kukicha Afrika kote.2024 Netflix na Amazon Prime wanaanza Services zao South Africa ambako ndo base kubwa ya DSTV kwa Afrika nzima.DSTV Wana miaka 3 mbele kabla Awajafungasha vilago na kutoka kwenye ulimwengu wa Pay TV.Either na yeye aanzishe Streaming Services na aje na Bei nzuri vinginevyo atoboi
Sio bure bwana wewe...nacho maanishi nikwmba mie nilipie compact plis alafu wao wani upgrade kwemda premium as long as nitaendelea kulipia compact plus pasipo kuikatisha. Hii waweke kwa all subscribers with more than 10 years connectionSasa bure lifetime utalipia nini tena
Dstv S.A itakufa na ndiko walipokuwa na wateja wengi. Unaambiwa watu wanahamia kwenye TV mtandao sasa hivi.Kampuni ya Multichoice inayomiliki visimbuzi maarufu vya DSTV imelamba hasara ya Tshs bilioni 122 kwa miezi sita iliyoishia Septemba mwaka jana sababu kuu ikiwa kupungua kwa wateja wake huku Afrika kusini pekee ikipoteza wateja zaidi ya laki nne.
Multichoice imedai kutekeleza malengo yake yote iliyoyapanga lakini mazingira inayofanyia kazi yametawaliwa na kukatika katika kwa umeme, presha kwenye gharama za kuishi na kushuka kwa thamani ya pesa katika nchi walizopo dhidi ya dola.
Mwaka huu channel maarufu ya michezo ya supersport itashindwa kuonesha michuano ya Afcon inayotarajiwa kuanza January 13 nchini Ivory Coast. Mwezi uliopita shirikisho la mpira wa miguu Afrika liliingia mkataba wa haki za matangazo kwa miaka miwili na kampuni kutoka nchini Togo ya New World TV iliyoanzishwa mwaka 2015.
Ni mwanzo wa mwisho wa utawala wa DSTV kusini mwa Afrika? Bado DSTV ni moja ya nguli wa kurusha matangazo barani Afrika huku kampuni zake mbili za DSTV na GoTV zikiwa na visimbusi milioni 23 vilivyo hai kwenye nchi 50 barani Afrika.
Mungu Aepushie Mbali AmeenHata Azam litawakuta jambo sio muda
Ni kweli kabisa! Dstv ni wapuuzi wanaweka gharama kubwa!Watu hawana hela hivyo wanapunguza matumizi yasiyo ya lazima.
Kabisa hiyo ni mbinu maana kama hujapata faida hulipi Kodi! Dstv wanapata super profitHizo story huja watu wanapokuwa wameshatengeneza njia za kukwepa kodi
Mumbwa wewe!Du! ujinga huu waliofanya DSTV ni zaidi ya ule ujinga wa Magufuli kuwakamia wafanyabiashara hadi wakafunga biashara na kupelekea uchumi kudorora. Na baada ya uchumi kudorora akaamua kukimbilia kukopa matrioni ya pesa hivyo kuiingiza nchi kwenye mzigo mkubwa wa madeni unaotuumiza vichwa hadi sasa. Mungu anamuona.
Wewe kiazi kweli. Kwa hiyo hata kama hayupo kwani alipokufa alikufa na madeni yake?Mumbwa wewe!
Huyo Magufuli bado yupo?
Serikali mbona inakopa mara 5 zaidi ya Magufuli na maisha yanazidi kuwa magumu?
Au unazani wote ni mazuzu km wewe.
Tupe mfano wa hayo matrilioni aliyokopa Magufuli mimi nikueleze matrilioni aliyokopa Samia.