DSTV yalamba hasara ya bilioni 122, gharama za vifurushi zawakimbizia wateja 486,000

Kitendo cha kifurushi cha compact kupanda toka 55k hadi 60k huku kukiwa hakuna huduma zilizoongezwa kilitukimbiza wengi.
Nililipia mwezi wa tano mwaka jana walipopandisha tu mpaka leo king'amuzi hata sijui kama kipo maana sijalipia tena. Mimi nanunua tu bundle basi maana kulipia king'amuzi ni hasara tupu.
 
Katika sababu walizoziweka wamesahau sababu moja ambayo ni ukuaji wa matumizi ya internet...

Ukishakuwa na internet ya kasi na yenye gharama nafuu, DSTV inakuwa kama option B...
 
Nadhani wametusikia
Screenshot_20240107-165042.jpg
 
Jibu ni moja tu.

  • Ujio wa Smart TVs
  • Watu kuwa na uelewa kuhusu FTA na IPTV. (Huko nibure kuanzia mpira mechizote hadi muvi, bure daima hadi kifo).
Naomba kuielewa hii mkuu.
FTA na IPTV ndio kitu gani hiki?
 
Kampuni ya Multichoice inayomiliki visimbuzi maarufu vya DSTV imelamba hasara ya Tshs bilioni 122 kwa miezi sita iliyoishia Septemba mwaka jana sababu kuu ikiwa kupungua kwa wateja wake huku Afrika kusini pekee ikipoteza wateja zaidi ya laki nne.

Multichoice imedai kutekeleza malengo yake yote iliyoyapanga lakini mazingira inayofanyia kazi yametawaliwa na kukatika katika kwa umeme, presha kwenye gharama za kuishi na kushuka kwa thamani ya pesa katika nchi walizopo dhidi ya dola.

Mwaka huu channel maarufu ya michezo ya supersport itashindwa kuonesha michuano ya Afcon inayotarajiwa kuanza January 13 nchini Ivory Coast. Mwezi uliopita shirikisho la mpira wa miguu Afrika liliingia mkataba wa haki za matangazo kwa miaka miwili na kampuni kutoka nchini Togo ya New World TV iliyoanzishwa mwaka 2015.

Ni mwanzo wa mwisho wa utawala wa DSTV kusini mwa Afrika? Bado DSTV ni moja ya nguli wa kurusha matangazo barani Afrika huku kampuni zake mbili za DSTV na GoTV zikiwa na visimbusi milioni 23 vilivyo hai kwenye nchi 50 barani Afrika.
MultiChoice(DSTV) Malawi mwaka jana ilipoona inafilisika iliamua kufunga biashara lakini mamlaka ya mawasiliano ya Malawi ikawakubalia kwa sharti wanunue vifaa vyao vyote toka kwa wananchi ambao wanavyo kwa sababu havitakuwa na matumizi kwao, wakashindwa na kuendelea na biashara. Hapa Tanzania ingekuwa poa tu, watanzania wasikivu tu.
 
DSTV kwa ujio wa Streaming wanapoteza wateja kila kukicha Afrika kote.2024 Netflix na Amazon Prime wanaanza Services zao South Africa ambako ndo base kubwa ya DSTV kwa Afrika nzima.DSTV Wana miaka 3 mbele kabla Awajafungasha vilago na kutoka kwenye ulimwengu wa Pay TV.Either na yeye aanzishe Streaming Services na aje na Bei nzuri vinginevyo atoboi

Streaming service multichoice wanayo ndo ile inaitwa SHOWMAX Sema watu hawashoboki nayo kivile kama netflix.
 
DSTV kwa ujio wa Streaming wanapoteza wateja kila kukicha Afrika kote.2024 Netflix na Amazon Prime wanaanza Services zao South Africa ambako ndo base kubwa ya DSTV kwa Afrika nzima.DSTV Wana miaka 3 mbele kabla Awajafungasha vilago na kutoka kwenye ulimwengu wa Pay TV.Either na yeye aanzishe Streaming Services na aje na Bei nzuri vinginevyo atoboi
DSTV tayari wana streaming service kitambo sana zaidi ya miaka Nane sasa labda hujui tu..

WananPlatform wanaiita ShowMax, Wana DSTV Live Stream nk...
 
Kampuni ya Multichoice inayomiliki visimbuzi maarufu vya DSTV imelamba hasara ya Tshs bilioni 122 kwa miezi sita iliyoishia Septemba mwaka jana sababu kuu ikiwa kupungua kwa wateja wake huku Afrika kusini pekee ikipoteza wateja zaidi ya laki nne.

Multichoice imedai kutekeleza malengo yake yote iliyoyapanga lakini mazingira inayofanyia kazi yametawaliwa na kukatika katika kwa umeme, presha kwenye gharama za kuishi na kushuka kwa thamani ya pesa katika nchi walizopo dhidi ya dola.

Mwaka huu channel maarufu ya michezo ya supersport itashindwa kuonesha michuano ya Afcon inayotarajiwa kuanza January 13 nchini Ivory Coast. Mwezi uliopita shirikisho la mpira wa miguu Afrika liliingia mkataba wa haki za matangazo kwa miaka miwili na kampuni kutoka nchini Togo ya New World TV iliyoanzishwa mwaka 2015.

Ni mwanzo wa mwisho wa utawala wa DSTV kusini mwa Afrika? Bado DSTV ni moja ya nguli wa kurusha matangazo barani Afrika huku kampuni zake mbili za DSTV na GoTV zikiwa na visimbusi milioni 23 vilivyo hai kwenye nchi 50 barani Afrika.
Mungu ibariki DSTV
 
DSTV kwa ujio wa Streaming wanapoteza wateja kila kukicha Afrika kote.2024 Netflix na Amazon Prime wanaanza Services zao South Africa ambako ndo base kubwa ya DSTV kwa Afrika nzima.DSTV Wana miaka 3 mbele kabla Awajafungasha vilago na kutoka kwenye ulimwengu wa Pay TV.Either na yeye aanzishe Streaming Services na aje na Bei nzuri vinginevyo atoboi
Netflix ni nzuri zaid ya DSTV
 
Naomba kuielewa hii mkuu.
FTA na IPTV ndio kitu gani hiki?

FTA = Free To Air ( Hapo ukiwa na king'amuzi kinachoruhusu kupokea signals bila kulipia mfano " GTMEDIA RECEIVER DVB S2+T2" pamoja na kuwa na dish kubwa kuanzia ft 6 Cband utapata channels za bure kulingana na uelekeo wa satellite uliyotegeshea dish lako na zipo nyingi sana.)

IPTV = Internet Protocol Television ( Hapo ukiwa na uhakika wa internet iwe bure au kulipia bando bei rahisi tena ukipata fiber kama zuku na ttcl basi hapo mchawi anabaki kuwa Smart tv tu kuna apps za kustream channels za kimataifa tena zile kubwa kubwa kama zote bure.)
 
FTA = Free To Air ( Hapo ukiwa na king'amuzi kinachoruhusu kupokea signals bila kulipia mfano " GTMEDIA RECEIVER S2+T2" pamoja na kuwa na dish kubwa kuanzia ft 6 Cband utapata channels za bure kulingana na uelekeo wa satellite uliyotegeshea dish lako na zipo nyingi sana.)

IPTV = Internet Protocol Television ( Hapo ukiwa na uhakika wa internet iwe bure au kulipia bando bei rahisi tena ukipata fiber kama zuku na ttcl basi hapo mchawi anabaki kuwa Smart tv tu kuna apps za kustream channels za kimataifa tena zile kubwa kubwa kama zote bure.)
🙏🙏🙏
 
DStv
Ni nyumbani kwa F1 na MotoGP....

January hii tupo na Dakar rally
Mhh F1 iko premium! Mwanzo wa season wanaachia kidogo then wanarudisha premium. Kama wengi walivyosema inabidi washushe bei vinginevyo kila mwaka watapoteza wateja. Maisha yamekuw magumu.
 
Back
Top Bottom