Dua zenu zimekubaliwa: Kenya haitaagiza tena chakula kutoka Tanzania 2023

Dua zenu zimekubaliwa: Kenya haitaagiza tena chakula kutoka Tanzania 2023

Yaan mtu kama siyo mkulima bhana unaeza ongea vyovyote lakin fikiria uyo mkulima unamfungia mipaka ili akuuzie chakula bei powaaa na ndo tegemeo la kipato ccha

Ruto akiwa makamo wa Rais alihusishwa na njama ya Kenya kusitisha manunuzi ya mahindi kutoka Tanzania.

Hiyo ilitokana na Ruto kufadhili mashamba makubwa ya mahindi nchini DRC ambapo inadaiwa kuwa alijipanga kutoa huduma hiyo kuanzia miaka ya 2020 lakini mpango ukabuma.

Kuna wakati mahindi yetu yalikataliwa kuingia Kenya kwa sababu yameathiriwa na sumu kuvu. Hivi sasa yuko kiti kirefu, inawezekana Amerika kusini inapakaziwa tu, karibu zaidi kama siyo Tanzania basi ni DRC.
Mahindi yatatoka Zambia no more
Congo hakuna kilimo tunawa uzia pale kasumba resa viazi mviringo,dagaa,maharage,karanga,vitunguu,Michele,kwa Bei za Doral Tena za juu jiandaeni kuwatafutia soko wakulima wenu
 
Tujenge viwanda, uchumi wa kutegemea kuuza mazao umepitwa na wakati
Hadi Marekani wenyewe wanauza mahindi ghafi, sio unga
Mahindi ni rahisi na salama kusafirisha kuliko unga, pia kuhifadhi mahindi ni rahisi na salama kuliko unga

Mahindi yanazalisha vitu vingi tofauti na unga, kuna pumba, makande, popcorn, sembe na dona
Ndio maana biashara hufanyika ya mahindi zaidi kuliko products za mahindi
Ndio maana wafanyabishara wanachagua kununua mahindi zaidi kuliko
 
Kwa watu wenye akili na wenye uchungu na uchumi wa nchi hii, ni jambo la kuhuzunisha Sana kupoteza soko kubwa namna hii,
Tulipaswa kuongeza nguvu kwenye kilimo Cha umwagiliaji tuzalishe mara 3 , Kwa mwaka Ili kukidhi soko la chakula kenya na kulishikilia Kwa nguvu zote,
Pia kutafuta na masoko mengine kama Ethiopia Sudan somalia nk.
Cha kusikitisha Kuna watu wenye fikra za kipumbavu kabisa watafurahia na kutamani kufungwa mipaka yote,
Hutupaswi kuwapa nafasi hata kidogo
 
Naona hujafikiri vizuri hatukatai biashara lakini huwezi uza kwa jirani wakati kwako hakitoshi utakuwa punguwani.
Hizi ni fikra duni za kufikiria familia Yako , hapa tunaongelea kilimo biashara Kwa manufaa ya taifa na kuongeza kipato Cha taifa,
Demand ikiwa kubwa hiyo ni fursa ya kuongezeka uzalishaji,
Sio kufunga soko huo ni utaahira
 
Hizi ni fikra duni za kufikiria familia Yako , hapa tunaongelea kilimo biashara Kwa manufaa ya taifa na kuongeza kipato Cha taifa,
Demand ikiwa kubwa hiyo ni fursa ya kuongezeka uzalishaji,
Sio kufunga soko huo ni utaahira
Sasa kama uzalishaji hautoshelezi soko la ndani utauzaje chote nje ya nchi? Kuna kitu kinaitwa protectionism hata mataifa yaliyoendelea yanafanya ili kulinda usalama wa ndani. Soma soma uelimike..
 
Ni kosa kubwa sana la kiuchumi kulipoteza soko la nafaka la Kenya.

Soko hutafutwa, na likipatikana hulindwa. Watanzania kama kweli tuna akili, hatukustahili kabisa kulalamika kama nafaka zetu zilikiwa zinatoka nje ya mipaka ya nchi yetu. Hiyo ilikuwa ni fursa nzuri sana kiuchumi. Ulikuwa ni wakati wa kuzidisha uzalishaji kwa nguvu zote.

Kwa mvua zinavyoendelea **** uwezekano wa kuwa na mahindi mengi mwakani. Ikiwa hivyo, utakuwa ni mwaka wa kuwaua wakulima.
Kwanini nafaka? kwanini tusiuze product kutoka viwandani?

Yaani tuuze packed rise na sembe na unga wa lishe

Uoni tunapoteza ajira nyingi?
 
View attachment 2449797

Kenya wamepanga kuagiza tani 900,000 za mahindi na tani 600,000 za mchele kutoka nchi kwa njia ya meli kutoka nchi za Amerika

Shehena hiyo ya mchele na mahindi ni kwa ajili ya kufidia upungufu wa chakula kwa mwaka 2023 kwa kuwa uzalishaji wa ndani ni mdogo

Hii ni habari njema kwa wale waliokuwa wakitaka serikali ifunge mipaka ili tusiuze chakula nje, bei ishuke ndani

Naona Kenya wameamua kufanya biashara na nchi zinazojielewa, zenye uhakika wa uzalishaji

Sio kufanya biashara na nchi ya wavivu na walalamishi wasiotaka kulima ili kujitosheleza kwa chakula chake wenyewe, inakuwa ni biashara isiyokuwa ya uhakika

Na kwa kukosekana kwa soko la Kenya, kilimo sasa kitakuwa ni zaidi ya biashara kichaa, wataendelea kulima losers waliokosa ishu ya kufanya mjini, ila sidhani kama kuna mtu mwenye mtaji serious ataenda kuwekeza kwenye bidhaa isiyokuwa na soko la uhakika
Wapi waliposema hawataagiza kutoka Tanzania?
 
Wameagiza tani 900,000 kufidia uzalishaji wa ndani
Hizo tani laki 9 plus mahindi watakayovuna wao, unafikiri watahitaji mahindi yenu tena?
Umejibu swali langu? Kwani wameaema hizo Tani 900,000 zitatoka Ulaya pekee au?

Hata Tanzania Ni ng'ambo
Screenshot_20221218-172156.png
Screenshot_20221218-171933.png
 
Back
Top Bottom