Dubai wakumbwa na mafuriko baada ya mvua kubwa kunyesha

Natoa Pole kwa Jamaa zangu pale Sharjah, Deira Union , Al sabkha, Gold Souq Gate no 2& 3, Silver Touch, Al madina , Al coniche, Al yazia Plaza, swahili Restaurant, Bila kusahau wapambanaji wote Pale Dubai Mall
 
Nimeona Black BMW inaoga na kunywa vikombe vya kutosha
Mkuu hiyo siyo BM
Natoa Pole kwa Jamaa zangu pale Sharjah, Deira Union , Al sabkha, Gold Souq Gate no 2& 3, Silver Touch, Al madina , Al coniche, Al yazia Plaza, swahili Restaurant, Bila kusahau wapambanaji wote Pale Dubai Mall
Mbona umenisahau mimi ninayeishi na kumiliki jumba langu la usd 50 m palm jumeirah?

RRONDO
 
D
Dubai sio mara ya kwanza kukumbwa na mafuriko baada torrential rains kupiga kwa siku mbili tatu mfululizo. Mwaka 2020 yalitokea makubwa kama haya na cha kukumbuka ni kwamba maji huwa yanahamishwa kwa muda tu, baada ya miaka kadhaa water courses always claims their ways
 
Mkuu hiyo siyo BM

Mbona umenisahau mimi ninayeishi na kumiliki jumba langu la usd 50 m palm jumeirah?

RRONDO
Nisamehe mkuu Maghayo kwa Kukusahau.
Ila nyie pale Palm tayari mlikwishajipata mnaishi pepo yenu . Kimbembe ni huku uswekeni kwa Wa Pakstani , Wafilipino, Nepal na Wahindi , wa nigeria, Waganda.
Mwenyezi MUNGU awanusuru.
 
Nisamehe mkuu Maghayo kwa Kukusahau.
Ila nyie pale Palm tayari mlikwishajipata mnaishi pepo yenu . Kimbembe ni huku uswekeni kwa Wa Pakstani , Wafilipino, Nepal na Wahindi , wa nigeria, Waganda.
Mwenyezi MUNGU awanusuru.
Heshima kwako mkuu nimecheka balaa. Pitia hapo kwa mangi agizia chochote ntalipa baadaye.
 
Shida ni hili bwawa la nyerere, walijenga bila kushirikisha wataalam. R.I.P JPM
 
Hivi ford bronco zipo bongo kweli?
Sijui ila . Juzi kati nimeona Ford Super duty. Pale mitaa ya Kalakata Airport.

Ila pia kuna hii gari inaitwa Honda Pilot.
Nalo limesimama kulia bata kibongo.
 
Dubai yakumbwa na mafuriko, safari za ndege zasimama

Mvua kubwa imeendelea kupiga katika mji wa Dubai na nchini Oman, na kusababisha mafuriko ambayo yamepelekea maafa na kusimamisha safari za ndege katika uwanja wa ndege wa Dubai ambao ni wa pili kwa shughuli za safari za ndege duniani.

Uwanja huo wa Kimataifa umetahadharisha kuhusu "hali ya hatari" na kuwashauri baadhi ya abiria kutofika katika maeneo ya uwanja huo kutokana na kujaa maji.

Jana Jumatano, April 17, 2024 , takribani safari 300 za ndege kwenda na kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai ambao ni kitovu cha kuunganisha safari za ndege kwa takribani kila bara - ziliahairishwa au kucheleweshwa.

Uwanja huo ambao mwaka jana ulihudumia zaidi ya abiria milioni 80, ukiwa wa pili kwa ukubwa baada ya Uwanja wa Atlanta nchini Marekani, ulionya kwamba inaweza kuchukua "muda" hali kurejea katika ukawaida wake.

Emirates, shirika kubwa la ndege la kimataifa lenye makao yake makuu mjini Dubai, jana lilizuia abiria waliokuwa wakisafiri kutokea katika jijini hilo kuingia kwenye ndege zake hadi leo April 18, 2024 kama hali itakuwa nzuri.

Mamlaka ya hali ya hewa nchini humo ilitahadharisha kuwa mvua nyingi zikiwa zimeambatana na radi na upepo mkali zitaendelea kupiga na kuonya watu wa maeneo ya mabondeni kuchukua tahadhari.

Kaskazini mwa Dubai mwanaume mmoja alikufa baada ya gari lake kusombwa na mafuriko.

Huko Oman, waokoaji walipata mwili wa msichana katika eneo la Saham, na kufanya idadi ya vifo nchini humo kufikia 19 tangu Jumapili.
 
Wanatamani kusema CCM ndo imepeleka mafuriko Dubenga sema nafsi inawasuta wataonekana Vinega.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…