Duh! Rais Samia amkataa mama mnyonge aliyetaka kumlilia kama Magufuli. Nenda kakae…


Hakuna Rais hapo!
 
Mama kaupiga mwingi hivo yeye anaamini tu kuwa yeye hayo ya wengine hayamhusu .
 
Umenena vyema! Ila kuna kundi kila madahaifu ya Rais wanapiga mapambio! Yaani Rais anaonesha hadharani hawezi kujali masrahi ya mwananchi wa chini Wasaidizi wake si ndo itakuwa balaa!
Ndio lumumba buku 7 hao yani hata siku kiongozi akijinyea watasema ni mfumo wake wa tumbo unafanya kazi vizuri tu ni hali ya kawaida mtu kujisaidia😅
 
Hii nchi itakapofikia watu wanaviziana na kuuana ndipo ambapo serikali itastuka😜 na kugundua kuwa kumbe inatakiwa iwajibike kwa matatizo ya wananchi
 
Hawa jamaa ni wajinga sana! Rais analipwa na kulishwa na kodi za watanzania! Sasa yupo hapo kwa ajili ya tumbo lake au watanzania! Rais akikosea lazima asemwe yeye ni nani?
Mbona JPM mlikuwa mnamuona mdogo wake mungu, na waliomkosoa walikiona cha mtema kuni, wengine wakapotezwa wengine wamebaki kuwa walemavu mpaka leo...au JPM alikuwa halipwi mshahara na wananchi? Maana mzee alikuwa anaona wengine wote kama ng'ombe tu isipokuwa yeye!

Mama is doing good, mwacheni aijenge nchi, msemeni anapokosea ili mambo yaende saw a sawa
 
Wananchi milioni 50 wanaishi huko vichochoroni, Rais akiwasikiliza wote hatafanya kazi nyingine.Jawabu la Miungu watu wa vichochoroni ni KATIBA MPYA.
Raisi hawezi sikiliza watu zaidi ya 3 kwenye hotuba. Hio inajulikana kabisa sema tu raisi wetu wa sasa amedhihiri kuwa hana time na wanyonge 😂
 
Yani hapo kwa tafsiri tu huyo mama haki ndio ishapotea aandike maumivu tu😅!

Sababu kuu ni kwamba hao wanaotakiwa kumsaidia wote wanamuona msumbufu sababu hela ya kuhonga hana na sio mtu wa maana. Ubaya haya yanafanyikaga kwa coordination sababu viongozi wa level zote wana mawasiliano na taarifa juu ya huyo mtu isipokuwa raisi mwenyewe.

Kwahio raisi kuli forward kwa watu wa chini yake still haitasaidia. Ni sawa na utume barua ya maombi halafu secretary aitupe kwenye dustbin. Usitegemee boss atakaa aione labda kwa neema za Mungu!
 
Hii Safi, inaondoa unafiki nafiki... mama afuate taratibu atasikilizwa, sio kusubiri barabarani na mabango, mahindi au jogoo.
Hizo taratibu za kibongo tena kwa awamu hii ya kula kwa urefu wa kamba yako mwenye mda na wewe kama huna pesa ya hongo ni nani? Huyo mtu amechoshwa na kuzungushwa.
 
Kama hizo delegation of power, specialization of labor zingekuwa zinafanya kazi kwa weledi hao watu wasingekuwa wanafika kuanika mabango kwenye hafla na hotuba za raisi
 
Wako wangapi wenye shida kama hizo sasa.. Au Rais awe anatenga muda katika ratiba zake wa kufika kila wilaya kusikiliza matatizo yaliyoshindikana na watendaji wake? Liko practical kweli hilo?
 
Wako wangapi wenye shida kama hizo sasa.. Au Rais awe anatenga muda katika ratiba zake wa kufika kila wilaya kusikiliza matatizo yaliyoshindikana na watendaji wake? Liko practical kweli hilo?
Akiskiliza watatu haina shida
 
Au mi nimeelewa vibaya... Ujue kuna baadhi ya watu kuongea kiswahili kwao.. Ili waeleweke.. Wanabadili maneno ya kiingereza kwenda kiswahili... Na hadhira anayoongea nayo, anaitafsiri kama ni wale "laymen" kabisa... Kwa hiyo anaiangalia hadhira, anaiona inamtegemea yeye kama "mtatuzi" wa mwisho wa shida zote za wananchi, wakati kuna masuala ya haki yanayotolewa maamuzi mahakamani. Nadhani hiyo statement isimhukumu Rais.. Ni kule kutafsiri neno "unfortunately" ambako kumesababisha hiyo sintofahamu...
 
Ule ujinga wa maigizo hatutaki,safi Sana Rais..

Haiwezekani kila mwenye tatizo amtafute Rais.
ukifikiria kwa kutumia nguvu kidogo tu utaelewa. Hakuna mwenye akili ambae atakaa na shida yake amsubiri raisi apite ndo amueleze.
Ukiona mama kamfata raisi kuelezea shida yake uwe na hakika hajapata msaada katika ngazi alizopita huko chini ndo mana anaona msaada wake utatoka kwa raisi.
Hukumbuki wakati wa Yesu? sio kama hapakua na waganga wa kutibu watu ila kwanini wagonjwa walikua wanamuandama Yesu? ni kwasabab hawakupata uponyaji kwa hao waganga.
Ukiona huyo mama kafanya ujinga omba yakukute ndo utapata akili
 
Reactions: nao
Mtoto Mwenye Hekima na busara ,aliyelelewa vema na mwenye maadili,hawezi kumkatisha Mzazi au mkubwa wake wakati anaposema.
 
Alishaandika hoja yake na Rais kasema ataenda kuitazama na kuifanyia kazi, Sasa ulitaka amjibuje? Siyo Kila kitu kinapaswa kutolewa majibu ya papo kwa hapo vinginevyo itakuwa ni ukurupukaji. By the way Rais kamjibu kwa upole yeye akaendelea kung'ang'ania ndo maana kaamua kwa Mara ya pili kukaza sauti "KAA CHINI". Sijaona kosa la Rais
 
Raisi hawezi sikiliza watu zaidi ya 3 kwenye hotuba. Hio inajulikana kabisa sema tu raisi wetu wa sasa amedhihiri kuwa hana time na wanyonge 😂
Kukubali kuitwa mnyonge ni kuidhalilisha nafsi yako. Mungu aliumba binadamu mkamilifu mwenye nguvu za mwili na ubongo. Yeyote akizitumia akili zake na nguvu zake vizuri ana uwezo wa kupiga hatua kiuchumi na kijamii. Usikubali kuitwa Mnyonge, utapata LAANA kama aliyoondoka nayo Mwendazake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…