Rais amekosea kutomsikiliza ila mwenye shida amekosea zaidi kulazimisha kukatisha hotuba.
Mama Samia anatoa hutuba unamkatisha ili useme shida yako. Why usumsubiri amalize hotuba yake kwanza?
Rais amekosea kutomsikiliza ila mwenye shida amekosea zaidi kulazimisha kukatisha hotuba.
Mama Samia anatoa hutuba unamkatisha ili useme shida yako. Why usumsubiri amalize hotuba yake kwanza?
Kwani kuna ubaya hupi,?hata angelimkabidhi kwa Waziri wa sheria au wasaidizi wake,kwani alikuwa anaambiwa atoe ukumu? Samia anausaidizi wowote kwa Watanganyika wa hali ya chini,labda kwa Mafisadi,ana roho mbayaHayo mambo si ya kukurupuka ovyo, Magufuli alikuwa anapenda kukurupuka ndio maana yule mama wa Tanga alimdanganya kudhulumiwa mirathi ya mumewe kumbe yeye ndio tapeli.
Mama Samia yuko sahihi swala unakuta lilishaenda mahakamani au watendaji wanalifanyia kazi mtu sababu tu kaona raisi kaja anataka kubururuza taratibu ziheshimiwe si kwamba Mama Samia hatalifuatilia ila kitakachofuata kama huyo mama alionewa wahusika wajiandaeKila utawala na mambo yake
Tukubali kubadilika
Ule ujinga wa maigizo hatutaki,safi Sana Rais..
Haiwezekani kila mwenye tatizo amtafute Rais.
Naunga mkono.Kila jambo ulishughulikie wewe kisa ni rais. Utapata matatizo ya moyo kwa binadamu wasio na shukrani hata kidogo.
JPM alikuwa anataka kushughulika na kila tatizo, amefariki na ni kama wema wake ulipotea bure tu, anatukanwa na wengi humu jukwaani.
Alishaanza kuugua kipindi kampeni zinaendelea.Naunga mkono.
Magufuli asingegombea urais 2015 leo angekuwa bado anaishi.
Angeweza kuongea kiupole kidogo kuliko alivyofanya…
Magufuli aliwahi kuongea kiupole liniAngeweza kuongea kiupole kidogo kuliko alivyofanya…
Usiongee mambo usiyoyajua! Suala la Msingi Ni Moyo wa Mtu kuguswa na mambo ya watu wengine! Magufuli ukiachana na hao Waliokuwa wanam-face directly amesaidia watu wengi sana kimya kimya walioonewa. Sasa huyu ambaye hakurupuki ameshamsaidia nani?Hayo mambo si ya kukurupuka ovyo, Magufuli alikuwa anapenda kukurupuka ndio maana yule mama wa Tanga alimdanganya kudhulumiwa mirathi ya mumewe kumbe yeye ndio tapeli.
Kwa hili maza nakupa tano, utasikiliza wangapi? mtindo huu wa marehemu haukuwa mzuri, tuna watendaji kibao kila ngazi, kuna wawakilishi wa Rais kibao - kama kweli wananchi wana matatizo hadi wanataka kumwona Rais pekee yake basi tukubali watanzania kwamba tuna mfumo mbovu wa utawala - na sisi tunaodai KATIBA MPYA nikweli tuna hoja ya msingi.
Unakosea, kila anayekwenda kinyume na mama kwenye baadhi ya vitu ni sukuma gang? Watu walimkosoa mpaka Jiwe, sembuse mama?Rais anaongea then mtu anamkatisha na watu wanaona jibu alilopewa huyo mama hakustahili..wtf..sukumer gang tulieni.
Ni kweli, ila humu kuna watu wachache mno ukilinganisha na majority ya Watanzania wanaomkubali! Humu ndimo wapinzani wengi walimojificha, so hakuna maajabu kumtusi Jiwe.Kila jambo ulishughulikie wewe kisa ni rais. Utapata matatizo ya moyo kwa binadamu wasio na shukrani hata kidogo.
JPM alikuwa anataka kushughulika na kila tatizo, amefariki na ni kama wema wake ulipotea bure tu, anatukanwa na wengi humu jukwaani.
Si alisema kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake!
==========
Mama mmoja amesikika akimuomba Msheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassani kuwa anaomba atendewe haki, mama huyo amerudia mara 3 kusema anaomba atendewe haki, Lakini Rais Samia alimjibu kuwa hawa hapa wapo umeshatuandikia litanifikia nenda kakae. Rais Samia Aliendelea kusema kuwa ona yanajitokeza hata hapa. Hivyo kusisitiza mahakama zitende haki kwa kuangalia utu wa mtu.
Sukuma gang achezi malalamiko, huyo mama aende kwenye vyombo husikaHiyo mama hata ukimuona ni mtu wa kuhitaji msaada! Acheni ujinga!
Hii kesi inafanana na ya Barthimayo Kipofu aliyekuwa anapiga Kelele kumlilia Yesu huku watu wakimnyamazisha asiwapigie Kelele. Sote tunajua Yesu alifanyaje? Jambo la msingi Ni shida za unaowaongoza na sio kila Mara kuangalia kama utaratibu umefuatwa ama la.Huyo mwenye shida ni mnyonge asiejua hata huo utaratibu wa kusubiri. Yeye anachojua ni kupaza sauti tu kuomba msaada.
Angemsikikiza ili ajue atakapo kwenda kuona alichoandika alinganishe na maneno mubashara kutoka kwa muhusika.
Usipende kurahisisha mambo hujui mtu anamaumivu ya kuonewa kiasigani.
Kila mtu anayeona huko kwingine hatendewi haki akimfuata rais inakuwa fujo. KATIBA MPYA ndio jawabu.Watu wako desperate. Ukiona hivyo ujue huko kwingine wanaona kama vile hawapati haki zao.
Una uhakika gani kama yeye ndiye mwenye haki? Umekwisha sikiliza pande zote mbili au umejigeuza mahakama Kangaroo ?Kwa jibu hilo alilopewa huyo mlalamikaji asitarajie chochote cha maana hapo.. Haki yake ndo ishapotea hivyo