Duh! Rais Samia amkataa mama mnyonge aliyetaka kumlilia kama Magufuli. Nenda kakae…

Duh! Rais Samia amkataa mama mnyonge aliyetaka kumlilia kama Magufuli. Nenda kakae…

Juzi tu katuambia watumishi wa umma tusipeleke malalamiko kwa Rais kama tume ya maadili ya utumishi wa umma ilishatoa maamuzi kuhusu kesi zetu. Ila katiba inatuambia tuna haki ya kukata rufaa kwa Rais kama tunahisi haki haikutendek. Leo tena yanajirudia kwa wananchiwa kawaida.
Mama hataki kusikia shida za waliomchagua. Yupo sahihi kabisa kwamba hatakiwi kuwa jalala la kila shida, ila anatakiwa ku strengthen istitutions zake zote kabla hajakataa kusililiza shida za wapiga kura. Atuletee katiba mpya, then yeye akae pembeni aache katiba ichukue mkondo wake. Kwa sasa hawezi kuepuka shida zetu sababu katiba inampa mamlaka makubwa ya kuwa msemaji wa mwisho kuhusu maslahi yetu.
kwani Kuna sheria yoyote imevunjwa?
 
==========

Mama mmoja amesikika akimuomba Msheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassani kuwa anaomba atendewe haki, mama huyo amerudia mara 3 kusema anaomba atendewe haki, Lakini Rais Samia alimjibu kuwa hawa hapa wapo umeshatuandikia litanifikia nenda kakae. Rais Samia Aliendelea kusema kuwa ona yanajitokeza hata hapa. Hivyo kusisitiza mahakama zitende haki kwa kuangalia utu wa mtu.

Huyu ni katili haswa
 
Kama hizo delegation of power, specialization of labor zingekuwa zinafanya kazi kwa weledi hao watu wasingekuwa wanafika kuanika mabango kwenye hafla na hotuba za raisi
Hapo sasa ndiyo pa kufanyia kazi lakini siyo kazi ya Rais wa Nchi yenye watu 60 Milioni kumjibu Mtanzania mmoja mmoja.

Ule UJINGA wa Magufuli tumeuzika naye Chato March 2021
 
Wanawake siku zote ni watu wa Jazba, nimegundua Mama samia ni mtu wa Jazba zaidi waenga walisema tabia haina dawa

Wasaidizi wake wamekua ni msaada mkubwa sana kwa Wananchi mfano Kassim Majaliwa , ukimuona shida ngumu na za kudhulumiwa zinaisha kama Maghufuli

Nadhani ndio maana JPM alitaka mh Majaliwa ndio aje kua Raisi

Kwahiyo mlishajipangia vyeo kama nchi yenu vile
 
Ule ujinga wa maigizo hatutaki,safi Sana Rais..

Haiwezekani kila mwenye tatizo amtafute Rais.
Nikweli unalosema ila haijawahi kukutokea ukapitia changamoto,wajanja wanawapiga makofi ya nyani watu wote hadi RC.na Mahakama.....Utaenda wapi? Nchi hii dhulma ni waziwazi, inawezekana nikweli JPM kulikuwa na kasoro hizo,ila Kuna machozi ya watu wengi na hakuna pa kupata haki yao
 
Alishaandika hoja yake na Rais kasema ataenda kuitazama na kuifanyia kazi, Sasa ulitaka amjibuje? Siyo Kila kitu kinapaswa kutolewa majibu ya papo kwa hapo vinginevyo itakuwa ni ukurupukaji. By the way Rais kamjibu kwa upole yeye akaendelea kung'ang'ania ndo maana kaamua kwa Mara ya pili kukaza sauti "KAA CHINI". Sijaona kosa la Rais
Mjomba hayajakusibu
 
Azibaye masikio yake asisikie kilio cha masikini,yeye naye atalia,lakini hatasikiwa. MITHALI 21:13
 
This is TZ, mkuu! Kitendo cha yeye kukimbikilia kwa Rais tayari kimeshawachukiza wale wadogo wote. Akiwarudia watamuambia apeleke shida zake kwa Rais. Kwa maneno mengine, if her situation was bad, it’s going to be worse!
Dawa ni katiba mpya, hakuna nchi inayojielewa ambayo Rais anatatua migogoro ya mashamba na ndoa kwa mwananchi mmoja mmoja.
 
that's right

na hicho ndicho Samia anakiamini kwa dhati kutoka moyoni, she wishes kwamba serikali ingeweza kutoa hukumu za kesi.

Umegusia suala la Samia ku dissapoint wanawake, lakini si yeye tu, hata JPM nae alififisha mahakama. Marais wetu hawaamini mahakama. Ukipata muda nenda youtube tafuta clip ya Harmonize aliposimama nje ya airport DSM akieleza kwa saa nzima jinsi kesi yake na Diamond ilivyoamuliwa na Rais!

Eti watu wana namba za simu za marais mifukoni wakigombana wanawapigia simu marais waamue, mambo ya mikataba, mambo ya kibiasharana, ya kisheria, na marais na wanatoa maagizo kwa mawaziri!
Rais anashugulika na bifu za Wasafi na Konde boy![emoji1787]
 
Majukumu ya rais sio hayo yakuokoteza shida za wananchi mmoja mmoja.ndo maana nchi ina vyombo na wizara mbali mbali.kama mtu anashida na haitatuliwi ngazi ya chini xiko taratibu zakupeleka malalamiko yake ngazi ya juu.acheni kujitoa ufahamu kwa mambo madogo kama hayo kisa kuna limbukeni mmoja alikua anasikiliza matatizo ya watu kienyeji bila kuhimarisha taasisi zakutatua kero za wananchi.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Wewe ndo unajitoa ufahamu. Unajifanya hujawahi ona Samia anasikiliza kero ya mtu mmoja mmoja?

Sema Rais hana uwezo na mambo Magumu, anayaogopa hatari.

Kimsingi anakwepa jukumu lake la kuwahudumia wananchi.
 
Rais amekosea kutomsikiliza ila mwenye shida amekosea zaidi kulazimisha kukatisha hotuba.

Mama Samia anatoa hutuba unamkatisha ili useme shida yako. Why usumsubiri amalize hotuba yake kwanza?
Ndo usemi wake ukinizingua ntakuzingua
 
Juzi tu katuambia watumishi wa umma tusipeleke malalamiko kwa Rais kama tume ya maadili ya utumishi wa umma ilishatoa maamuzi kuhusu kesi zetu. Ila katiba inatuambia tuna haki ya kukata rufaa kwa Rais kama tunahisi haki haikutendek. Leo tena yanajirudia kwa wananchiwa kawaida.
Mama hataki kusikia shida za waliomchagua. Yupo sahihi kabisa kwamba hatakiwi kuwa jalala la kila shida, ila anatakiwa ku strengthen istitutions zake zote kabla hajakataa kusililiza shida za wapiga kura. Atuletee katiba mpya, then yeye akae pembeni aache katiba ichukue mkondo wake. Kwa sasa hawezi kuepuka shida zetu sababu katiba inampa mamlaka makubwa ya kuwa msemaji wa mwisho kuhusu maslahi yetu.
Hakika.

Kama wananchi wanakosa msaada kuanzia chini huko hadi kwa Rais basi tumekwisha.
 
Alishaandika hoja yake na Rais kasema ataenda kuitazama na kuifanyia kazi, Sasa ulitaka amjibuje? Siyo Kila kitu kinapaswa kutolewa majibu ya papo kwa hapo vinginevyo itakuwa ni ukurupukaji. By the way Rais kamjibu kwa upole yeye akaendelea kung'ang'ania ndo maana kaamua kwa Mara ya pili kukaza sauti "KAA CHINI". Sijaona kosa la Rais
Utalionaje kosa la Rais wakati kakutia limbwata?
 
Back
Top Bottom