Duka la Dawa Muhimu za Binadamu (Pharmacy): Utaratibu wa Kufuata na Mtaji wa Kuanzisha Biashara

Mfamasia gani bongo saivi utamlipa hayo mamilioni!mtaani graduate wamejaa hawana kazi
 
Mfamasia gani bongo saivi utamlipa hayo mamilioni!mtaani graduate wamejaa hawana kazi
Unaongea kitu ambacho hukijui, tuulize sisi ambao tupo kwenye hili game kuhusu kuwapata wafamasia wenye degree!
 
Kwenye huo uzi wako mwenyewe maswali ya msingi ya wadau umeyakimbia tangu 2019 mpk leo.
 
Hio ndio pont ya msingi.Safi sana.
 
Uko very honest and positive sana thank you very much again
 
Huyo mphamasia anatakiwa alipwe mwisho wa mwezi. Tuseme 1m
Efd mashine laki4
Cheti cha dispensary???

Ngoja nione itakuaje huko mbele
Nashukuru

Sent using Jamii Forums mobile app
Haiko hivyo ushauri anza hiyo biashara story za kumpa mphamasia 1.5m sijui laki 8 ni ngonjera unampa hata laki 2 kulingana na mauzopia mnaweza mkaingia mkataba ama partnership unamlipa % fulani ya faida

Phamacy zipo za jumla na rejareja so kwa visenti vyako utakuwa na pharmacy ya rejareja natumaini unatambua tofauti ya DLDM na pharmacy.

Unaweza kuanza na DLDM baadae uka upgrade kuwa pharmacy muhimu uwe forecast. Industry ya Dawa ni ngumu kama zilivyo biashara zingine na usipokuwa makini hii ni ngumu sana ina mambo mengi na ujanja kama biashara zingine.

Uzoefu ni 30% ya mtaji mtu ambaye tayari anamiliki Duka la Dawa muhimu kwa pesa yako anaweza kufanya kazi ya 24m hizo display cases nunua materials fundi akutengenezee. Anza na displays 4
Kubwa moja upana 6ft na urefu 6ft kila ngazi iwe na 33cm ni nzuri zaidi

Counter display 6ft by 3ft but ngazi ziwe pana 33cm
Na mbili ndogo za ukutani 3ft by 3ft .
Kununua Dawa nako ni Shida nyingine tegemea na distributors muhimu kuwa na taarifa sahihi na uwe na muda wa usimamizi by the way kupata pesa za kurun vizuri daily sales inabid iwe kuanzia 100k na ukianza vibaya miezi 6 ya mwanzo tayari unakuwa ushafilisika.

Pharmacy rejareja na DLDM huitaji EFD mashine unalipia tu mapato
Leseni ni 200k kwa 100k vingine utajifunzia mbele kwa mbele wauzaji malipo ni 150-200k including meals and transport wazoefu ni wazuri na ni wezi wabobezi wanacheza na logbook na sales book too.

Kugundua tofauti ni kazi kupata muuzaji mwaminifu na mchangamfu anaependa anachokifanya pia ni mtaji hasa kwa wanaoanza. Kwa sasa usipende kuzijua changamoto sana ukijua ya ndani zaidi hutofanya biashara yeyote
 

Umeshauri vizuri na kiuzoefu
 
Aiseeee naambiwaga phamarcy zinalipa sana kumbe nazo zinachangamoto zake za kutosha.
 
Habari zenu ndugu zangu. Mimi nimejipigapiga nimepata Tsh 20M. Nataka nifungue duka la Pharmacy. Vipi pesa itatosha au nimebugi. Ushauri wa kushiba tafadhali
 
Ni kubwa mno aisee ni mtaji mkubwa sana kwa ufunguaji wa pharmacy.
Kwa hiyo pesa anafungu pharmacy na kanoa keupe juu hiyo ni pesa toshelevu kabisa

Labda kama anataka ndio lwe more expensive pharmacy hapo mtaani kwake na mjinga yeyote asilete
fyokofyoko pia akifungua asinisahau
hata ka kazi kakufagia.
 
Habari zenu ndugu zangu. Mimi nimejipigapiga nimepata Tsh 20M. Nataka nifungue duka la Pharmacy. Vipi pesa itatosha au nimebugi. Ushauri wa kushiba tafadhali
Inaweza kutosha au isitoshe kufungua famasi pia itategemeana unapata wapi mfamasia kama utakuwa wamlipa jiandae si chini ya laki 7 kwa mwezi hapo bado wale assistance au tecnicians wengine, ili uwe na famasi wahitaji store iwe na AC na vigezo vinginevyo plus duka lenye AC na vigezo vingine ambavyo watu wa pharmacy council watakupa, usisahau ghalama kubwa iko kwenye kufata mzigo utahitaji pengine mzigo wa zaidi ya mill 10 bila shaka utahitaji usafir maalumu wa dawa zako toka kwa supplier kuja ofisin kwako dawa nyingi za pharmacy hazihitaji joto, vumbi wala maji hivyo utahitaji gari maalumu zinazohurusiwa hutobeba tu kwenye sijui canter yenye turubai.... All the best
 
Asante xana mkuu
 
Habari Wakuu

Baada ya kufanya research kidogo nimegundua maduka ya Pharmacy yameongezeka sana na yanazidi kufunguliwa, nahisi hii biashara ina faida nzuri japo sijapata mtu wa kunieleza kiundani sababu wanaoifanya wengi wanakuwa wasiri.

Je,
1. Ni kweli hii biashara inalipa?
2. Ni vigezo gani unatakiwa kutimiza ili uifanye?
3. Gharama zake zikoje ukiachana na kodi ya pango?
4. Kwa duka la Rejereja unatakiwa angalau uwe na mtaji wa kuanzia shilingi ngapi?, kwa jumla je?
5.Changamoto zake ni zipi?

Mwenye majibu angalau hata ya swali moja naomba anieleze.
Natakungliza Shukurani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…