BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Serikali imeanza uchunguzi wa ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi uliofanywa na Serikali ya Rais John Magufuli, kupitia alichoita, “Sheria ya Plea Bargain," Raia Mwema imeelezwa. Taarifa kutoka serikalini na baadhi ya watu walioswekwa magerezani na kutolewa kwa utaratibu huo, zinaeleza kuwa uchunguzi dhidi ya "mradi huo," unafanywa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Baadhi ya waathirika ambao hawakupenda kutajwa majina yao gazetini, walithibitisha kuitwa na kufika mbele ya jopo la uchunguzi, katika mikoa mbalimbali nchini. Waathirika hao wanadai kwamba dhana nzima ya plea bargain, iligubikwa na ubabe na kuendeshwa kwa kuangalia kipato cha mtu, badala ya kosa analodaiwa mhusika kulitenda.
Mmoja wa washukiwa waliofanya plea bargain na ambaye alifika mbele ya kamati, alitolea mfano wa kesi yao, iliyokuwa na washitakiwa watatu, kwamba kila mmoja alitoa kiwango cha fedha tofauti na mwenzake.
Alisema: "Mmoja aliambiwa alipe Tsh. milioni 5, mwingine akaambiwa alipe Tsh. milioni 700, lakini mwingine akatozwa Tsh. bilioni moja. Hakukuwa na fomula ya malipo. "Uamuzi ulitegemea wamekuta kiasi gani kwenye akaunti na uwezo ulionao. Yaani si sheria, kiasi utakacholipa kitatokana na utashi wa wenye mamlaka," alisema.
Aliongeza: "Namshukuru sana Rais Samia kwa kuliona hili na kulifanyia kazi. Kuna watu wameugua kwa kupoteza mali zao kwenye jambo hili. Wengine wamekufa na wengine kuhama nchi, kutokana na madhila waliyopata."
Hatua ya serikali ya Rais Samia, kuagiza kufanyika uchunguzi wa uhalali wa jambo hilo na jinsi lilivyoendeshwa, ilitokana na malalamiko kadhaa kutoka kwa wananchi, wakiituhumu Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kuchukua mali zao kinyume na sheria.
Haijaweza kufahamika mara moja, ni kiasi gani cha fedha kilichokusanywa wakati wa utawala wa Magufuli, ngapi ziliingia kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina na kiasi gani kililiwa. Hata hivyo, madai kuwa mamilioni ya shilingi yaliyotolewa yaliishia mikononi mwa wajanja wachache na hata baadhi ya nyumba hazijafikishwa serikalini huku nyingine zikimilikishwa kwa watu binafsi "ndilo gumzo la mjini."
Mchakato wote wa plea bargain, unadaiwa kusimamiwa na kuratibiwa na aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga Alisema: "Mfumo mzima ulikuwa hivyo, maelekezo yalitoka juu na kwamba masharti yalikuwa lazima uonekane una makosa. "Tunashukuru Mama (Samia) alipoingia, aliekeza watu wote walioshitakiwa kwa makosa haya na hakukuwa na ushahidi, waachwe huru.
Hakukuwa tena na plea bargain ya aina ile."
Mtoa taarifa hakutaja kwa rnajina waliohama nchi, baada ya kubambikizwa kesi za uhujumu uchumi. Lakini gazeti hili, linaweza kumtaja mfanyabiashara maarufu, Yusuf Manji, aliyekimbilia Marekani na mwandishi wa habari, Erick Kabendera aliye Uingereza. Manji aliyekuwa akilimiki kampuni mbalimbali, alifikishwa mahakamani Februari 2017, alituhumiwa kwa makosa mbalimbali, ikiwamo kutumia dawa za kulevya aina ya heroine na uhujumu uchumi.
Kabendera alituhumiwa kwa makosa matatu ya uhujumu uchumi ikiwamo kujihusisha na genge la uhalifu, kukwepa kodi na utakasishaji fedha alilazimika kuingia 'makubaliano na DPP, kukiri kosa na kumwomba msamaha Rais Magufuli, ili "kupata uhuru wake."
Makosa yote matatu aliyokuwa akituhumiwa nayo, hayana dhamana kwa sheria za Tanzania. Kabendera alikamatwa na Polisi na Uhamiaji, Julai 29, 2019, akidaiwa kuchunguzwa kuhusu uraia wake. Baadaye mawakili wake walitoa taarifa, wakisema Kabendera atashitakiwa kwa kuhusika na ripoti iliyochapishwa katika jarida la The Economist la Uingereza, lakini mahakamani kibao kikageuka na kuwa kesi ya uhujumu uchumi.
Septemba 2019, Bunge lilipitisha muswada wa maboresho ya sheria mbalimbali, ikiwemo ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ambapo mapatano baina ya watuhumiwa na rnwendesha mashitaka yalipitishwa na kusainiwa na Magufuli.
Plea bargain inasimamiwa na vifungu vya 194A hadi 194H vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) ya mwaka 1985, Sura ya 20 na makubaliano yaliyofikiwa yatawekwa katika Kumbukumbu za Mahakama. Kanuni za sheria ya plea bargain, zilisainiwa na Jaji Mkuu Februari 5, 2022. Lakini mamia ya raia wa Tanzania na wa kigeni, walielekezwa kupitia utaratibu huo na DPP tangu mwaka 2019.
Sheria inaeleza katika makubaliano hayo, mshukiwa anaweza kukiri tuhuma au sehemu ya tuhuma dhidi yake, lli kupata afueni fulani ikiwamo kuondolewa baadhi ya mashitaka, ama kupunguziwa muda au aina ya dhabu. Aidha, mshukiwa atatakiwa kula kiapo cha kukubaliana na makubaliano hayo, atapoteza haki ya kukata rufaa, isipokuwa kuhusu urefu au uhalali wa hukumu atakayopewa.
Hata hivyo, wakati utaratibu huo unatumiwa na DPP, Peter Madeleka mmoja wa mawakili mashuhuri nchini, alisema wakati hayo yakifanywa kanuni za plea bargain, zilikuwa hazijaanza kutumika.
"Plea bargain, inasimamiwa na sheria. Wakati Mganga anatekeleza yote haya, kanuni za plea bargain zilikuwa hazijatungwa. Watu "Walianza kukamatwa mwaka 2017 na kutozwa mamilioni ya fedha mwaka 2019, kanun1 zikitungwa mwaka 2021 alisisitiza.
Aliongeza: "Kwa hiyo, vitu vyote vilivyofanyika kabla ya kanuni kutungwa, ni batili. Hili nimekuwa nikilisema siku zote, kwamba haya yaliyofanywa ni haramu tupu." Kuhusu fedha kupelekwa akaunti ya DDP, Madeleka arnbaye aliwekwa gerezani kwa tuhuma za uhujumu uchumi, alieleza kuwa fedha zinapaswa kuhifadhiwa kwenye akaunti ya Msajili wa Hazina.
"Mwenye mamlaka ya kukusanya na kushikilia mali ya Serikali, ni Msajili wa Haz-ina. Sheria ya plea bargain, haimtaji kokote DDP. Kwa hiyo, hilo la kukusanya fedha za watu na kuweka kwenye akaunti yake iliyko. BoT, nalo ni haramu, alieleza.
RAIA MWEMA