Duka la "Plea Bargain" lafungwa, Waliochukuliwa fedha zao waitwa kuhojiwa, uchunguzi waanza

Duka la "Plea Bargain" lafungwa, Waliochukuliwa fedha zao waitwa kuhojiwa, uchunguzi waanza

Udhaifu wa sheria zetu hizi, yaani mtu mmoja anaifanya taasisi ya Rais kama mali ya mama yake na anaangaliwa tu

Kama Bunge lingekuwa na meno na sheria zinafuatwa angetolewa kwa kutokuwa na Imani nae na shtaka juu

Ila kwa nchi masikini na viongozi masikini wa akili na mali na busara basi hakuna namna kila anaekuja anaamua kufanya anavyoamka nayo na hakuna wa kumzuia akisema kesho wote tunakimbia Tutakimbia tu
Uko sahihi 100%. Nakumbuka kumsikia mwenyewe Rais Magufuli akitamka, yeyote ambaye atapuuza kwenda kwenye plea bargain, Shauri yake atakaa ndani hata miaka 20, kwa hiyo unaweza kuona wengi walijua nini kingewakuta wangebisha. Kwa ujumla ni ukatili wa kiwango cha juu sana, wenzetu walipitia. Udhaifu wa bunge na mahakama ni janga kubwa kwa utawala wa sheria. Naweza kusema mtu kama Kikwete hana sifa ya maana ya kukumbukwa kwenye utawala wake, kwani kwa sehemu kubwa alichangia sana mateso hayo ni kama alikuwa akifurahi, na alisikika akisema mlisema mimi mpole, Sasa nimewaletea tingatinga. Binafsi namuona kama msaliti tu, hata hizo nafasi za kimataifa hazimstahili hata kidogo.
 
Back
Top Bottom