Duka linapitia changamoto ya kukosa wateja. Mbinu ipi nitumie?

Duka linapitia changamoto ya kukosa wateja. Mbinu ipi nitumie?

stivii

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Posts
222
Reaction score
143
Mwenza wangu nilimpa mtaji afungue biashara kwa kuwa anapenda sana urembo akaona afungue biashara ya duka la urembo, cosmetic na mavazi.

Lakini anapitia changamoto ya kukosa wateja inaweza ipite siku mteja asiingie kabisa dukani. Siku akiuza basi ni bidhaa chache tu. Duka lipo Mikocheni lina miezi miwili. Anauza nguo, viatu vya kike, perfume, jewellery na vitu vya namna hiyo.

Mwenye uzoefu na hii biashara anisaidie mawazo maana naona wife anapata stress mno kuwa business itakufa. Tumejaribu kuwa anatangaza online ila page haijachangamka ata tukiboost wateja hatuwaoni.

Mawazo yenu wadau.
 
Hilo duka lina mtaji kama kiasi gani?

Kama linazidi 5M bora uviuze kwa bei ya jumla kwa wenye maduka makubwa then umfungulie biashara ya duka la vitu vya jumla, kama pesa itabaki kidogo weka na mitungi ya gesi na baadae mtaji ukikua weka huduma za mpesa

Kama fremu haipo sehemu ya makazi mengi ya watu tafuta sehemu nyingine iliyochangamka
 
Kwanza kila kitu kinahitaji sacrifice,ajitoe haswaaa na bahati mbaya inakuja kama ameingia kwenye biashara kwa kuhisi tu kua inalipa,miezi miwili bado ni michache sana kuanza kuwa na hofu, kuna muda ROI(Return on investment) kuipata inachukua muda na itambidi awe na moyo mkuu na dhabiti haswaaaaa.

Mwisho: "Fortune favor the brave"
 
Ulizingatia location? Status ya wateja eneo hilo? Ni kweli wateja wanahitaji huduma kama hiyo sehemu hiyo?

Ngoja wabobezi wa marketing waje waongezee maswali.

NB: Biashara huwa hainyanyuki kwa muda mfupi kama unavyofikiria. Wote hawa tunaowaona wamefanikiwa walishasota sana
 
Naenda moja kwa moja kujibu swali lako

Swali mnalopaswa kujiuliza mmeanzisha biashara kwa lengo ngani?

Wateja wako ni kinani?

Location ya biashara yako imekaaje?

Washindani wako unawafahamu?

Ubora wa bidhaa zako zikoje?

Bei ya bidhaa zako zinafanana na za washindani wako?

Customer care na customer service unazitoa ni kwa ajili yako binafsi au mteja wako aridhike?

Kwa hayo maswali ukiyajibu kwa ufanisi changamoto ya wateja kwenye biashara yako itakuwa imefikia tamati,hakuna mchawi hapo kwa maelekezo zaidi njoo dm.
 
Nilifungua duka dogo la Ujenzi, wiki tatu za mwanzo mauzo yalikuwa 1m hadi 1.5 kwa siku nikashukuru Muumba, aisee baada ya miezi 4 duka likawa linauza elfu therathini hadi elfu kumi kwa siku. Vitu vimejaa ila watena wanalipita tu kama hawalioni.

Wengi watasema ni bei ya bidhaa zetu, ubora, Lugha kwa wateja, upangaji wa vitu dukani nk - vyote hivi vilizingatiwa kwa umakini mkubwa, kuna wakati tukashusha vitu vyote kwa 500 hadi 1000 compared na wenzetu ila kitu kikagoma.

Nikaamua kulifunga, nikasema mali za kuamika na wanadamu wanaziona zina changamoto zake.
 
Lugha ya biashara yaani customer care iwe ya kiwango cha juu.

Mteja afike shop uko bize na simu unategemea nini.

Wadada hawa walivyo na visirani, mara afungue duka saa saba mara asifungue kabisa nani ataenda hapo.

Bidhaa pia ziwe toleo jipya.

Biashara inabidi uvumilie, miezi mitatu tu ndo kaanza kulia lia.
 
Sure mi nilifungua duka miezi mitatu ndio wateja wakalizoea duka ikawa full shangwe..
 
stivii Poleni sana yawezekana pale anapofanyia hiyo biashara akuzingatia anavyouza na jamii inayopazumbuka hapo .

Kiuhalisia kwa hapo mjini kati hiyo biashara inahitaji muda sana kujitangaza japo pia hapo mjini kati biashara ni ushindani sana tofauti na sehemu zingine unajikuta uko mwenyewe.

Hivyo aangalie sehemu yenye uhitaji wa hivyo vitu ili aweze kufanya biashara au ajipe muda huku akitangaza hiyo biashara.

Ila mkoani ni kutamu sana kwa hiyo biashara hasa vijijini kwa wakulima kwenye misimu hii ya mavuno .

Karibu mbeya tufanye wote hiyo biashara nimewekeza pia

Ushauri tu [emoji120][emoji120][emoji120]

TEKERI
 
Biashara imehamia mtandaoni, ajitangaze sana mtandaoni na awe anafanya delivery. Kama vipi a run ads campaign facebook na instagram awalipe wale wambea wa Insta pia watupie matangazo.
 
Kama ni miezi miwili hii.. Biashara hiyo haikua rahisi sana. Hata kwa sisi wa Kkoo jumla.
Nashauri awekeze muda mwingi kwenye marketing ya bidhaa zake dukani.
Nashauri kutokukata tamaa..
Nashauri muda wa baishara unakuja hivo kuweni na subira.
Miezi miwili ni michache sana kujua mtazamo wa biashara kama hiyo.
ASANTE.
 
Wateja wanakimbiaga bei mana ushindani ni mkali muuze bidhaa sawa na wenzenu mana biashara siku faida ni asilimia 10 ya bei ya bidhaa ukitaka faida nusu kwa nusu hiy haipo wateja watakuwa wanaishia kuuliza nakuondoka
 
Naenda moja kwa moja kujibu swali lako
Swali mnalopaswa kujiuliza mmeanzisha biashara kwa lengo ngani?
Wateja wako ni kinani?
Location ya biashara yako imekaaje?
Washindani wako unawafahamu?
Ubora wa bidhaa zako zikoje?
Bei ya bidhaa zako zinafanana na za washindani wako?
Customer care na customer service unazitoa ni kwa ajili yako binafsi au mteja wako aridhike?

Kwa hayo maswali ukiyajibu kwa ufanisi changamoto ya wateja kwenye biashara yako itakuwa imefikia tamati,hakuna mchawi hapo kwa maelekezo zaidi njoo dm.
Duka lipo mikocheni ni ushuani kidogo ila lipo barabarani tena pembeni kuna kituo cha bodadoda.

Washindani sio wengi hiyo biashara kuna duka lingine moja na bidhaaa alizoweka ni size ya kati sio bei kuuubwa za vile ila sio vitu cheap pia.

Kuhusu customer care ananisaidia sana ila sijui inapimwaje good customer service ila anahudumia vizuri tu wateja.
 
Mwambie aingie kwenye vipodozi

Atafute vile vinavyotrend mjini apige kampeni mitandaoni huko
Wateja wa hivyo watasaidia kununua na vingine
Okay sawa nimekuelewa.

Unaweza nitajia baadhi ya vipodozi anavyoweza kuweka vikavutia wateja ili kama hana nimwelekeze aviweke?
 
Lugha ya biashara yaani customer care iwe ya kiwango cha juu.

Mteja afike shop uko bize na simu unategemea nini.

Wadada hawa walivyo na visirani, mara afungue duka saa saba mara asifungue kabisa nani ataenda hapo.

Bidhaa pia ziwe toleo jipya.

Biashara inabidi uvumilie, miezi mitatu tu ndo kaanza kulia lia.
Kuhusu muda anajitahidi maana anafungua kila siku kuanzia saa 3 mpaka saa 2 usiku kasoro jumapili ndio anachelewa kufungua sababu ya ibada.
 
stivii poleni sana yawezekana pale anapofanyia hiyo biashara akuzingatia anavyouza na jamii inayopazumbuka hapo .

Kiuhalisia kwa hapo mjini kati hiyo biashara inahitaji muda sana kujitangaza japo pia hapo mjini kati biashara ni ushindani sana tofauti na sehemu zingine unajikuta uko mwenyewe.

Hivyo aangalie sehemu yenye uhitaji wa hivyo vitu ili aweze kufanya biashara au ajipe muda huku akitangaza hiyo biashara.

Ila mkoani ni kutamu sana kwa hiyo biashara hasa vijijini kwa wakulima kwenye misimu hii ya mavuno .

Karibu mbeya tufanye wote hiyo biashara nimewekeza pia

Ushauri tu [emoji120][emoji120][emoji120]

TEKERI
Asante mkuu ila nikimwamishia Mbeya roho yangu itakuwaje mzee mwenzangu 😂😂😂
 
Back
Top Bottom