Nilifungua duka dogo la Ujenzi, wiki tatu za mwanzo mauzo yalikuwa 1m hadi 1.5 kwa siku nikashukuru Muumba, aisee baada ya miezi 4 duka likawa linauza elfu therathini hadi elfu kumi kwa siku. Vitu vimejaa ila watena wanalipita tu kama hawalioni.
Wengi watasema ni bei ya bidhaa zetu, ubora, Lugha kwa wateja, upangaji wa vitu dukani nk - vyote hivi vilizingatiwa kwa umakini mkubwa, kuna wakati tukashusha vitu vyote kwa 500 hadi 1000 compared na wenzetu ila kitu kikagoma.
Nikaamua kulifunga, nikasema mali za kuamika na wanadamu wanaziona zina changamoto zake.