Dullah Mbabe umetuonesha wewe ni kichwa cha familia

Dullah Mbabe umetuonesha wewe ni kichwa cha familia

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya Mzambia Mbachi Kaonga, Bondia Dullah mbabe alifanya mahojiano mafupi na vyombo vya habari.
1741127571242.jpg

Mwandishi: Ulilionaje Pambano?

Dullah: Lilikuwa gumu, siko sawa, siko fit nina 'hogo' (Akaonesha picha katika simu), nilikuwa kwenye matibabu kwa miezi sita. Tunapigana kwa sababu hatuna pesa, lazima tupambane riziki ipatikane lakini siko fit.

Nilijua ni mechi ya kawaida, ndio maana niliwaambia mapromota tutafute mechi ya kawaida lakini mechi imekuja kuwa ngumu.

Mwandishi: Ulimwonaje mpinzani wako?

Dullah: Sio bondia mzuri sana, sema mwenyewe nilikuwa unfit.

Mwandishi: Kwa nini ulikubali kucheza na unajua unaumwa Dullah?

Dullah: Day after day lazima zipatikane riziki za watoto, wanatakiwa waende shule, wanatakiwa wasome pia tupate riziki za kula na familia.

Mwandishi: Kwa maana hiyo una-sacrifice kwa ajili ya familia?

Dullah: Yes, lazima..lazima tupambane!
__________________________________
MY TAKE: Sikuwa nikimsikiliza loser, bali nilikuwa namsikiliza baba, nilikuwa namsikiliza mwanaume, mpambanaji haswa.
 
Baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya Mzambia Mbachi Kaonga, Bondia Dullah mbabe alifanya mahojiano mafupi na vyombo vya habari.
View attachment 3259327

Mwandishi: Ulilionaje Pambano?

Dullah: Lilikuwa gumu, siko sawa, siko fit nina 'hogo' (Akaonesha picha katika simu), nilikuwa kwenye matibabu kwa miezi sita. Tunapigana kwa sababu hatuna pesa, lazima tupambane riziki ipatikane lakini siko fit.

Nilijua ni mechi ya kawaida, ndio maana niliwaambia mapromota tutafute mechi ya kawaida lakini mechi imekuja kuwa ngumu.

Mwandishi: Ulimwonaje mpinzani wako?

Dullah: Sio bondia mzuri sana, sema mwenyewe nilikuwa unfit.

Mwandishi: Kwa nini ulikubali kucheza na unajua unaumwa Dullah?

*Dullah: Day after day lazima zipatikane riziki za watoto, wanatakiwa waende shule, wanatakiwa wasome pia tupate riziki za kula na familia.

Mwandishi: Kwa maana hiyo una-sacrifice kwa ajili ya familia?

Dullah: Yes, lazima..lazima tupambane!
__________________________________
MY TAKE: Sikuwa nikimsikiliza loser, bali nilikuwa namsikiliza baba, nilikuwa namsikiliza mwanaume, mpambanaji haswa.

Kila mtu eneo lake, sema yeye eneo lake la kazi linampima hapo hapo, haya yetu sio hapo hapo ila wote tunapigwa
 
Inafanana na wale wanenguaji kwenye bars , kuna mmoja alihojiwa akasema ''anapambia familia japo watu wanamuona malaya '' ..Yye ni single mother wa watoto wawili bila kwenda kukata viuno hapo bar kwa kucheza mziki , basi wanae watalala njaa .

Dunia ngumu sana hasa huu uchumi wa pesa , lazima upambane upate chochote kile .
 
Visingizio tu,

Ni huyu huyu aliwahi kuwaambia mabondia wa bongo wasiende Urusi kisa wale jamaa wanapiga ngumi kama mawe!
 
Thats what it takes to be a real men, unapambana kufa na kupona ili familia uliyoianzisha isipate tabu hapa duniani
Ila wanaume wenzangu tusisahau kuipa pole mioyo yetu pindi nafasi ya kufanya hivyo inapopatikana, Maisha mafupi sana hapa duniani.
 
Back
Top Bottom