Dunia bila uwepo wako. Wewe ni nani hasa? (Soma hadi mwisho, itabadilisha mtazamo wako)

Dunia bila uwepo wako. Wewe ni nani hasa? (Soma hadi mwisho, itabadilisha mtazamo wako)

Davidmmarista

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2024
Posts
3,114
Reaction score
6,309
Wadau za wakati huu,

Tuna muda kidogo hatujaonana uzi wangu wa mwisho wiki kama 3 zilizopita lakini katika kukaa kwangu na kufikiria nimefanya uchambuzi pamoja na utafiti mbalimbali kuhusu hii mada yetu hii ya leo. Mada hii ya leo imeibuka baada ya siku moja swali hili kutokea: "Kama nisingewepo duniani, dunia ingekuwa tofauti vipi?"

Swali hilo linauma. Na ndilo hasa unalostahili kujiuliza leo.

TATIZO KUBWA KATIKA JAMII YETU.
Tunazunguka kila siku na watu ambao wanajisikia ni bora kuliko wengine kwa sababu ya mambo ambayo yanaweza kupotea kesho asubuhi:
- Ana pesa nyingi: anakudharau
- Ana digrii: anaona wengine ni wapumbavu
- Ana kipaji: anajifakhiri bila kusimama
- Ana cheo: anasahau alikotoka
- Ana marafiki wenye nguvu: anakuonyesha huwezi kumfikia

Hizi ni LABEL tu. Si yeye.

Fikiria hivi: mtu akiondolewa pesa zake kesho: bado yupo.
Akiondolewa cheo chake: bado anapumua.
Akiondolewa shahada aliyonayo: bado ana akili ile ile.

Maana yake nini? Maana yake mambo hayo si yeye.
Ni vitu anavyobeba tu. Na kitu unachobeba kinaweza kuanguka.

Mtu anayeamini yeye NI pesa zake, ataanguka pamoja nazo.

Hii ni just an intro ya kukujaribu kuonesha namna gani sisi ni makontainer ambayo yamebeba thamani, ujuzi na vipawa mbalimbali wakati uleule kila kilichopo kwenye kontainer kinaweza kuondolewa na bado kontainer likawa tupu.
Ok ngoja twende kwenye kipande kingine tujiribu kuelewa zaidi.


JINSI MAISHA YANAVYOFANYA KAZI.
Watu wengi wanaishi maisha yao yote wakifuata jibu baya la swali moja:

Swali: "Nitakuwaje na thamani maishani?"
Jibu baya: "Nijikusanyie vitu vingi pesa, vyeo, sifa."
Jibu sahihi: "Nitatoa nini kwa wengine ambalo hawana?"

Formula halisi ya kutafuta thamani maishani:
Thamani yako duniani = Kina cha ujuzi wako/Bidhaa Yenye Uhitaji/ Huduma Inayohitajika × Idadi ya watu unaowafikia

Mtu mwenye mamilioni lakini hajachangia chochote kwa mtu yeyote
ana thamani NDOGO kwa dunia kuliko mwalimu wa kijiji
ambaye amebadilisha jinsi watoto 500 wanavyofikiri.


NJIA MBILI ZA KUISHI.
Kila mtu anaishi njia moja kati ya mbili. Angalia vizuri uone uko wapi:

NJIA YA KWANZA: Mtu wa Kutumia (Consumer)
Maswali ya kila siku:
"Nitapata nini?"
"Watu wananikiona vipi?"
"Yeye ana zaidi yangu mbona?"
"Nitajilindaje?"

Matokeo yake:
Maisha ya mashindano yasiyo na mwisho.
Furaha fupi fupi, wasiwasi wa kudumu.
Ukisimama unasahauliwa haraka sana.

NJIA YA PILI: Mtu wa Kujenga (Contributor)
Maswali ya kila siku:
"Ninaweza kujenga nini?"
"Nani anahitaji ninachojua?"
"Tatizo gani ninaweza kulisuluhisha?"
"Nitaacha nini nyuma yangu?"

Matokeo yake:
Maisha yanayokua kila siku.
Furaha ya kudumu, sio ya kuigiza.
Ukisimama kazi yako inaendelea kukuzungumzia.

Kinachochekesha 😅: watu wa kujenga ndio wenye mafanikio zaidi
mwishowe. Kwa sababu dunia haiwezi kupuuza mtu
anayeifanya kuwa bora

Hukuja duniani kutumia tu.

Ulikuja kuongeza kitu, kitu ambacho kisingewepo bila wewe.
  • Swali si: "Mimi ni muhimu kiasi gani?"
  • Swali ni: "Ninajenga nini, na kwa ajili ya nani?"


Nitaendelea but leo ni short introduction, nimeandaa huku nimechoka kidogo. Jitahidi kuelewa maana ya dunia, si neno kama tunavyofikiria "Earth" imetumika kuwasilisha maana fulani kwenye uzi huu.
 
Acha wivu wa kike. Mbona hoja inaeleweka kabisa. Kama umekuwa mhariri wa jf utuambie na uweke credentials zako hapa, ikibidi na wewe uje na hoja yako tuone weledi wako.
Ni mtazamo wake tu, anaona hivyo ila siyo lazima iwe hivyo.. watu wa aina hii huwa wapo tu
 
Back
Top Bottom