Jumbe Brown
JF-Expert Member
- Jun 23, 2020
- 12,077
- 12,786
Kila lenye mwanzo halikosi mwisho....Marekani iliipiga changa ya macho dunia kwa muda mrefu. Ikalazimisha dola iwe ndio pesa rasmi katika biashara za kimataifa na uchumi wa dunia. Wanachofanya ni kuchapisha noti tu za dola na kuipa thamani kwa kauli tu.
Dunia nayo ikawa imejikuta inakubaliana na changa hilo la macho. Lakini Urusi imeiamsha dunia na marekani imepaniki. Urusi imesema kila nchi inaweza kutumia pesa yake ya ndani kwenye miamala ya kimataifa.
Uamuzi huo ghafla ukairudishia thamani pesa yake ya ruble iliyokuwa imeshuka sana thamani kwa zaidi ya asilimia 90.
Kwa sasa mataifa kama india, China, Brazili tayari yamejifunza kitu na yataanza kutumia pesa za mataifa yao kwenye biashara baina yao na mataifa mengine yatakayokubali.
Urusi imeandaa mfumo wake kama ule wa SWIFT kwa ajili ya miamala ya kimataifa na nchi zimeshajiunga tayari na kwa kuanzia mataifa hayo (ukiacha mataifa ambayo hayaogopi kitu kama India na China) hayataainishwa ili kuyakinga na vitisho na vikwazo vya marekani.
Ndio maana Marekani inahaha kuongeza vikwazo kila siku na kupeleka silaha ukraine, si kwa kuwa inaipenda sana ukraine lakini inataka kuangusha kabisa uchumi wa urusi na kuipunguza nguvu kijeshi.
Japo mpaka sasa marekani inaonekana haijafanikiwa kwa hilo ila mambo yanaigeukia yenyewe kuwa mabaya!