Kitabu cha Mwanzo, nadhani ndicho kitabu kibovu kabisa kwenye Bible.
Hakina logic, ni contradiction mwanzo mwisho.
Kitabu cha mwanzo kinasema kwamba watu waliumbwa baada ya kuumbwa kwa mimea na wanyama,wanyama waliumbwa[Mwa.1:11-24], kisha watu mke na mume wakaumbwa kwa pamoja [Mwa.1:26-31]
Yaani kwenye hizoo nukuu, Mungu aliumba wanyama na mimea halafu watu wakawa wa mwisho kuumbwa.Kwenye hizo nukuu, Bibilia inasema mwanaume na mwanamke waliumbwa kwa wakati mmoja.
Sehemu nyingine ya kitabu cha Mwanzo inaeleza kwamba mtu aliumbwa kabla ya kuumbwa kwa wanyama.
Kitabu kinasema Mungu almuumba Adam kwanza[Mwa.2:7], halafu mimea ikaoteshwa baada ya kuumbwa kwa Adamu[Mwa.2:8-9].....Halafu wanyama wakaumbwa baada ya kuumbwa kwa Adamu[Mwa.2:18-19]
Halafu Eva akaumbwa mwishoni baada ya kuumbwa kwa Adam, mimea na wanyama[Mwa.2:21-23]
Hivi kweli kitabu chenye mikanganyiko kama hii unaweza kukitumia kama njia ya kujifunza chanzo cha uhai?