Mimi moja kwa moja napingana na CREATIONISM kwa maana haina mantiki.Nasema haina mantiki kwa sababu inatuachia maswali yasiyo na majibu na kutulazimisha tuiamini badala ya kuielewa.Mimi nina maswali yafuatayo kuhusu CREATIONISM.
1.Kama watu wote walitokea sehemu moja(mf.Mashariki ya kati), ni technologia ipi iliyotumika kusambaza watu kutoka mashariki ya kati kwenda maeneo mbalimbalina ya Dunia kama Chile, Madagascar n.k?
walivukaje bahari? Kama walisafiri, kwa nini wasingekuwa wanawasiliana kwa safari za mara kwa mara? Kwa nini kina V.Da Gama, C.Columbus wawe wagunduzi wa maeneo mengine? ina maana waliamini Dunia ni maeneo walimoishi pekee?
2.Kama tumetokana na Baba na Mama mmoja, kwa nini watu tunatofautiana sana? nini sababu na mechanism iliyosababisha wawepo watu weupe na weusi? Miaka 6000 inatosha kuruhusu mabadiliko makubwa tunanoyashuhudia ya tofauti miongoni mwa jamii za watu wa hii Dunia?
3.Kwa nini kuna mabaki ya kale yenye umri zaidi ya miaka milioni? kwa nini hayo mabaki hayapatikani nje ya Africa? Kwa nini fossils zinaonesha 'Life complexity' inaongezeka kutoka matabaka ya chini kuja matabaka ya juu ya miamba?
4.Kwa kuwa Watu waliumbwa kutokana na udongo, ni material yepi yaliyotumika kuumba viumbe wengine kama wanyama na mimea? Mbona watu wanafanana sana na hawa viumbe wengine?
5.Ukowapi ushahidi/mabaki ya bustani ya Eden, masalia/makaburi ya Adam na Eva?
Yako wapi masalia ya safina ya Nuhu? Mbona Palaeontology haioneshi kama mafuriko ya Dunia nzima yamewahi kutokea na kuua watu?
6.Kwa nini vitabu vya dini havizungumzii uwepo wa sayari nyingine?, Kama hizo Sayari ziliumbwa na Mungu, ni za kazi gani?
7.Kama Mungu ndiye muumbaji wa kila kitu, kwa nini aumbe viumbe hatarishi kwa watu wake kama vile; Virus, bacteria na Fungus wenye kusababisha magonjwa na vifo kwa watu? Mungu mwenye upendo wote anaweza kuumba vyanzo vya matatizo kwa watu wake?
8.Kwa nini miili ya viumbe vya Mungu iwe na vestigial organs?
9.Kwa nini Mungu aumbe Dunia yenye majanga asilia kama matetemeko ya nchi, mafuriko, vimbunga na milipuko ya volcano? Intelligent designer anaweza kuumba dunia yenye majanga kama hii ya kwetu?
10.Kwa nini Mungu alisikitika na kuhuzunika baada ya kumuumba Binadamu(Mwa.6:5-8)? Mungu gani mjuzi wa yote afanye jambo la kumsikitisha na kumhuzunisha siku za mbeleni?