TumainiEl mgogoro huu umeanza zamani sana na kufikia kilele 2014 baada ya Marekani kuingilia siasa za ndani ya Ukraine na kuchochea maandamano ya kumtoa raisi halali wa Ukraine siyo huyu kibaraka Zelenskyy . Pitia hapa
Ukraine crisis: Transcript of leaked Nuland-Pyatt call
Kwanza utambue Crimea ilikuwa sehemu ya Russia toka 1783 hadi mwaka 1954 pale Raisi Khrushchev wa USSR (Urusi) alipowapataia Ukraine eneo hili.
Kumbuka Khrushchev alikuwa mtu wa asili ya Ukraine, yaani kama hapa Mama Samia achukue Mafia awakabidhi Zanzibar. Sasa ukitaka kuona watu wako wa magharibi na kibaraka wao Zelenskyy wanavyotaka kusababisha vita ya 3 ya dunia wanakataa haki ya watu wa Crimea kurudi kwenye nchi yao mama (Russia). Wanasema lazima waichukue kwa nguvu kivita Crimea iende tena Ukraine.
Hao unaowashabikia wana nadi demokrasia na kututaka nchi maskini tuheshimu matakwa ya wananchi wao hawataki kuheshimu kura ya maoni ya wana Crimea waliochagua kurudi Russia.
Kuanzia 2014 serikali ya Kiev imekuwa ikiwalipua kwa mizinga na kuwauwa kikatili watu wanaotaka kujitenga na Ukraine, Putin kaenda kuwalinda kama vile watu wa magharibi walivyo enda kuwasaidia watu wa Libya waliompinga Ghadaf au watu wa Cosovo walipotaka kujitenga na Yugoslavia ya zamani. sasa kwanini Russia akifanya kama wao anaonekana katili mpenda vita?