Registered_jf
JF-Expert Member
- Nov 27, 2024
- 1,237
- 2,110
Kalaghabaho!Sasa hizo stori Zina ukweli gani bro?
Mm nimesoma nikaona blablabla nyingi na Imani za ujinga tu

Hamna mtu anataka story za bible sijui story za yesu alitembea juu ya maji, au Nuhu kupanda meli, au Mtu kusimamisha jua(not debating, just leaving this here)
Highlight:
1) Kweli inaweza isiwe na mantiki
2) Ukweli ni mkubwa kuliko uthibtisho
3) Sheria za mantiki zina mipaka yake.
4) Kuna kweli za kudumu na kweli za upande fulani.
Dr. Michael Guillen anasema:
Ukristo na Sayansi umeanza karibia wakati uleule, karibia miaka 2000 iliyopita (tuki assume sayansi ya kisasa imeanza na Aristotle).
Tangu vimeanza, Ukristo (Biblia) ni kama mlima uliosimama imara, haujabadilika. Huku sayansi ikiwa mto unaoenda ukiyumbayumba.
Tangu mto wa sanyansi uanze, je unazidi kwenda mbali na Mlima huu, au unazidi kuusogelea?
1) Zamani wanasayansi waliamini ulimwengu ulikuwepo milele. Wakaja kugundua ulimwengu ulikuwa na mwanzo.
"Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia."
Mwanzo.1.1.NENO
2) Wanasayansi wamegundua kuwa Uhalisia wa ulimwengu (Reality) kwa kawaida hauonekani, ni takriban asilimia 5 tu ya uhalisia ndio inaonekana (dark matter, dark energy hazionekani, tunaona tu matokeo yake).
Ndomaana tumeagizwa:
"Kwa hivyo hatuangalii yale yanayoonekana, bali yale yasiyoonekana. Kwa maana yale yanayoonekana ni ya kitambo tu, bali yale yasiyoonekana ni ya milele."
2Wakorintho.4.18.NENO
Sayansi haipingi neno la MUNGU, inaithibisha.
3) Wanasayansi wamegundua kuwa Kweli nyingi za ulimwengu hazina mantiki, zinapita mantiki (Dr. Guillen anaziita translogical).
Mfano:
A) Quantum Physics.
Quantum Physics ni Sayansi ya vichembe vidogo kabisa, katika kiwango ambacho sheria za kawaida za fizikia hazifanyi kazi.
Kwenye Quantum Physics:
i) Kitu kinaweza kuwa katika hali mbili tofauti kwa wakati mmoja (Superposition).
ii) Vitu viwili vinaweza kuathiriana papo hapo hata vikiwa mbali kabisa (Entanglement).
iii) Kitu kinaweza ku behave kama mawimbi na kama kitu kigumu kwa wakati mmoja.
Haya mambo matatu yako kinyume na sheria za mantiki lakini ni kweli zinazopimika na ndio msingi wa teknlojia za kisasa kama GPS.
B) Mfano mwingine: Gödel’s incompleteness theorem.
Hii nadharia ya kutokamilika ya Gödel inasema kuwa: katika mfumo wowote wa kimantiki wenye uwezo wa kuelezea hesabu, kuna kauli za kweli ambazo haziwezi kuthibitishwa kimantiki ndani ya mfumo huo.
Sasa ona: "Kauli hii haiwezi kuthibitishwa ndani ya mfumo huu."
i) Basi, Ikiwa mfumo unaweza kuthibitisha kauli hiyo, basi kauli hiyo ni ya uongo (kwa sababu imesemwa kuwa kauli hiyo haiwezi kuthibitishwa), na mfumo unakuwa unathibitisha jambo la uongo, maana yake mfumo huo si thabiti.
iii) Lakini, Ikiwa mfumo hauwezi kuithibitisha, basi kauli hiyo ni ya kweli, lakini haiwezi kuthibitishwa ndani ya mfumo huo.
iv) Kwa vyovyote vile, kuna kauli ya kweli ambayo mfumo huo hauwezi kuithibitisha.
Mfano wa mfano huu:
a) Fikiria kitabu kinacholenga kuwa na kauli zote za kweli za kihisabati. Kinatumia sheria maalum (axioms) kuthibitisha kauli hizo.
b) Gödel anaonyesha kuwa kitabu hicho kama ni thabiti, hakiwezi kuwa kamili kwasababu sikuzote kutakuwa na kauli ambazo ni za kweli lakini haziwezi kuthibitishwa kwa kutumia sheria za hicho kitabu.
c) Kuongeza sheria zaidi hakutatui tatizo bali kweli mpya zisizothibitishika zitaendelea kuonekana.
d) Hivyo, ukweli ni mkubwa kuliko uthibitisho, na sheria za mantiki zina mipaka yake. (Ukisikia Mantiki ya bei rahisi).
Ndomaana MUNGU anatuambia:
“Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu,” asema Mwenyezi Mungu.
“Kama vile mbingu zilivyo juu kuliko dunia, ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu na mawazo yangu kuliko mawazo yenu."
isaya.55.8-9.NENO
Dr. Guillen anasema YESU si wa kimantiki (lakini ni moja ya kweli tunaoshuhudia ulimwenguni)
4) Uhalisia (Reality) ni wa ajabu usio na kikomo (Infinitely mysterious)
Dr. Guillen anasema alifikiri Sayansi ikipewa muda ingejibu maswali yake yote.
Lakini anakuja kugundua Sanyansi ikijibu swali moja, 100 yanazuka. Kila wakigundua kitu, wanagundua na mengine hivi kwamba wanajikuta wanahitaji teknolojia kubwa zaidi, mashine kubwa zaidi kulichunguza, ni kama shimo lisilo na mwisho!
"Yeye hutenda maajabu yasiyoweza kutambuliwa, miujiza isiyoweza kuhesabika."
Ayubu.5.9.NENO
5) Muda ni mstari ulionyooka.
Zamani wanasayansi walifikiri muda ni duara, kwamba historia itajirudia.
(Ni kama zile imani za kule mashariki wanavyoamini kuwa ulimwengu unaanza na kuharibiwa over and over forever, na nafsi zetu zinarudi tena na tena).
Ukristo umejua kuwa ulimwengu uliumbwa mara moja, na YESU atarudi mara moja.
“Tazama, naja upesi! Thawabu yangu i mkononi mwangu, nami nitampa kila mtu sawasawa na alivyotenda.
Mimi ni Alfa na Omega, wa Kwanza na wa Mwisho, Mwanzo na Mwisho.
Ufunuo.22.12-13.NENO
6) Kwenye kiini chale kabisa, Ulimwengu ni wa kiroho (Supernatural).
Ukisoma Sayansi ya kisasa, mfano Quantum Mechanics (Sayansi ya tabia za chembe ndogo zaidi), unaelewa kuwa ni ngumu kutofautisha kipi ni cha kimwili na kipi kimepita mwili (Supernatural, cha kiroho).
Quantum Mechanics kwakweli imepita mwili, ni ya kiroho, na ndiyo msingi wa Sayansi ya kisasa.
Bilbia ilishatuambia kuwa tunakabiliana na viumbe ambao wamepita mwili (Supernatural):
"Kwa maana kushindana kwetu si dhidi ya mwili na damu, bali dhidi ya falme na mamlaka, dhidi ya wakuu wa ulimwengu huu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Waefeso.6.12.NENO
7) Wanabayolojia wa mageuzi wanakubali kuwa Binadamu (Homo sapiens sapiens) si kama wanyama wengine. Ni wa kipekee.
8) Ulimwengu umesetiwa mahususi kwa ajili ya kutegemeza maisha. Vipimo vyake thabiti visivyobadilika visingekuwa mahususi kama vilivyo, ulimwengu usingekuwepo.
Mfano:
i) Fine Structure Constant: inashikilia atoms
ii) Electron to proton mass ratio: inaongoza sheria za kemia.
iii) Strong Nuclear Force: inaunganisha atoms.
iv) Electromagnetic Force constant: ina support sheria za kemia.
v) Gravitational constant: inashikilia nyota, sayari, anga za sayari n.k
vi) Kasi ya mwanga: inaongoza sheria za kemia.
vii) Planck's constant: ina support sheria za kemia.
9) Dr. Guillen anasema Time, Space and Matter sio kati ya Kweli za kudumu (Absolute truths), hizo ni kweli za upande fulani (Relative truths).
Kwahiyo akisikia mkristo anabishania umri wa ulimwengu anajua hajui wanaongelea nini, ukweli ni kuwa Ulimwengu una mabilioni ya miaka au umri wake haujafika hata sekundi moja, ikitegemea unatazamia kutoka wapi.
Sayansi inaongea kutoka upande mmoja na Biblia kutoka upande mwingine na zote ni kweli kwasabu ni pande tofauti.
Muda ni mfumo rejeleo (reference frame), muda sio kweli ya kudumu.
(Taarifa: dunia ina umri wa miaka elfu chache tu)
Post in thread 'Kipindi siamini MUNGU, sikuwa na muda na imani za watu' Kipindi siamini MUNGU, sikuwa na muda na imani za watu
EBO!Hamna mtu anataka story za bible sijui story za yesu alitembea juu ya maji, au Nuhu kupanda meli, au Mtu kusimamisha jua
I need burden of proof not stories.
Logic vs faithWaite mabwana zako waje wakutekenye masikio.
JESUS IS LORD!
MAKE WAY FOR THE KING OF KINGS!
Huyo Yesu ni fictional character wa kwenye hekaya za Biblia. Kama alivyo Abunuwasi wa kwenye hekaya za Abunuwasi.(not debating, just leaving this here for Genuine Truth Seekers)
Proof of Jesus
HAKUNA mtu aliyeacha nyayo nyingi kwenye historia kama Yesu Kristo, HAKUNA!
Yesu Kristo ndiye Mtu mashuhuri kupita wote kwenye historia, nakuhakikishia.
1) Kwanza dini zote (ikiwemo dini ya atheism) zinamkubali Yesu Kristo, halafu Yesu anajikubali mwenyewe tu.
Wayahudi wanasema Yesu alikuwa Rabi/mwalimu.
Waislamu wanasema Yesu alikuwa nabii.
Wabuddha wanasema Yesu ni mtu aliyeangaziwa (enlightened).
Wahindu na imani za huko Mashariki wanasema Yesu alikuwa udhihirisho wa Mungu, mungu flani aliyechukua umbo la binadamu, mwalimu, mtawa, mtu mtakatifu aliyeamua kuachana na ya ulimwengu n.k.
New age spiritualists wanaohubiri power of the mind, wanasema Yesu alikuwa ni mtu aliyefuzu kwenye hiyo sekta.
Waamini sayansi kuwa ndo itawapa majibu ya kila kitu (wakana Mungu) wanasema Yesu alikuwa jamaa mjanja mjanja, mwanasiasa flani ambaye alianzisha chama chake na kupata wafusi.
Kuna viazi vichache vinasema Yesu hakuwepo kabisa.
YESU KRISTO hamtaji yeyote yule, anasema yeye pekee:
• ndiye Njia inayotafutwa na watu,
ndiye Kweli inayotafutwa na watu,
ndiye Uzima wa binadamu
unakopatikana,
• ndiye Mwanga kwenye ulimwengu
huu wenye giza,
• ndiye Ufufuo kwani kifo sio mwisho,
• ndiye Mlango wa kuingilia Next
Level,
• ndio Jina pekee tunalopaswa kuliitia,
sio majina ya watu waliokufa,
• ndiye Mchungaji mwema atatupa kila tunachohitaji,
• ndiye Mwana wa Mungu, Muumba aliyeingia ndani ya uumbaji wake mwenyewe, akawa Mwana wa. Binadamu
• ndiye Kristo/ Masihi/ Mwokozi, anayetuokoa na uharibifu (dhambi) na kifo ambacho binadamu anahangaika kukiepuka.
View attachment 3555599
(kuna mtu atakwazika kisa YESU ni ngozi nyeupe. Acha ushamba! Katafute ngozi nyeupe uoe uachane na hizi hoja za bei rahisi)
2) Hakuna mtu mwenye rekodi nyingi kumhusu kwenye historia kama Yesu Kristo.
-Waongo na wazushi wanasema hamna uthibitisho. Ni nini hasa kinastahili kuwa uthibitisho?
Shida sio kuwa hamna uthibitisho, shida ni hawapendi kuona wanachoona.
Yesu angekuwa ni mwalimu tu mwenye hekima ambaye hakuzaliwa na bikra, hakufanya miujiza, hakufufuka na kupaa mbinguni, hakuna ambaye angepinga kuwa hakuna mtu mwengine kwenye historia ambaye kumbukumbu zake zilitunzwa kwa wingi kama Yesu.
- Kwa sasa tuna takriban hati za zamani 6000 za agano jipya katika lugha ya Kigiriki peke yake! Wastani wa hati moja ni kurasa 450!
- Tukiongeza na nakala zilizotafsiriwa karne za kwanza kwa kilatini, kiCoptic, kiSyriac n.k tunakuwa na makumi ya maelfu ya nakala za agano jipya. NI AIBU kwa waongo na wazushi!
- Hakuna maandiko yoyote kwenye historia yenye shehena la nakala kama agano jipya! HAKUNA.
View attachment 3555598
3) Vitabu vya Injili viliandikwa na watu walioshuhudia hayo matukio.
Mpelelezi wa mauaji, James Warner Wallace (J.W.W), mkana Mungu aliyegeuka na kumwamini Yesu anasema akiitwa kwenye tukio la mauaji, maelekezo ya kwanza anayotoa kwa polisi ni kuwa wawatenganishe walioshuhudia hilo tukio. Maana wakikaa wote wataanza kujadili hilo tukio mpaka aje afike atakuta wana maelezo yanafanana fanana.
Lakini wakitenganishwa, akija kuwahoji mashahidi, maelezo yao huwa ni shagala bagala, huenda yakaonekana hata kuwa yanapingana. Lakini hiyo haimaanishi kuwa yanapingana.
Tena ukija kuchanganya maelezo yao yanayoonekana kupingana ndo unapata picha vizuri kwasababu kila mtu anakuwa anasimulia kutokana na mazingira aliyokuwepo wakati wa tukio, alichokuwa ana focus, hamu yake, mtazamo wake, makuzi yake n.k.
- Sasa basi, kitabu cha Luka kinasema kabisa anayoandika daktari Luka ni shuhuda za mashahidi alioenda kuwahoji (Luka 1).
- Mathayo na Yohana wanasema waliyoandika walishuhudia kwa macho yao.
- Injili ya Marko inakubalika na wachambuzi kuwa ni Marko alikuwa akiandika kwa niaba ya mtume Petro aliyekuwa anamsimulia, akimsaidia kutafsiri kwenda Kigiriki.
View attachment 3555593
Je kuna sababu yoyote ya kushuku shuhuda hizi?
a) Utasikia "haiwezani kitabu cha 1 Petro kiwe kiliandikwa na mtume Petro kwasababu kimeandikwa kwa Kigiriki cha kisomi kabisa na mtume Petro alikuwa mvuvi kutoka Galilaya".
Sasa kwanini asijue kigiriki wakati maisha yake yote aliishi eneo ambalo watu waliongea kigiriki! !
Lakini pia inaoneka kuwa Petro alikuwa anamsimulia mtu anamuandikia.
Kama wazee wa kanisa (church fathers) wa karne ya kwanza na ya pili kwenye barua zao walikuwa wanarejea maandiko na wanakubaliana kuwa yaliandikwa na flani na flani, unakataa nini? ?
View attachment 3555592
b) Au utasikia "maandiko yenyewe yameandikwa mamia ya miaka baada ya matukio kwahiyo yamebadilishwa au kutungwa ".
i) Kwanza hatuna nakala halisi zilizoandikwa kwa mikono ya mitume wenyewe, sababu ni wazi:
•Nyenzo walizotumia (ngozi) hazingeweza kudumu.
•Muda mrefu umepita.
Nakala za historia zilikuja kuanza kudumu wakati walipoanzisha taasisi za kutunza nakala hizi, ndomana unapokuja kukutana na nakala yoyote ya historia ya zamani zaidi iliyotunzwa unaweza kukuta ni ya miaka zaidi ya 90, 300, 1000 baada ya kuandikwa kwa nakala ya kwanza kabisa.
ii) Pia Nakala nyingi ziliharibiwa na waliochukia ujumbe wa Wakristo.
iii) Inawezekana pia waliiga utamaduni wa Wayahudi ambao waliharibu nakala za zamani zilizochakaa kila waliponakili maandiko kwenye sehemu mpya.
View attachment 3555591
c) Kama watu wangetaka kubadilisha biblia, ingebidi wapitie njama za viwango vitatu:
i) Kwanza njama ya hati - ingebidi wachukue zaidi ya hati 6000 za kigiriki agano jipya wazibadilishe na wafiche ushahidi kuwa wamefuta wino wakabadilisha.
ii) Pili njama ya lugha - Kisha itabidi wakatafute maelfu ya hati za agano jipya zilizotafsiriwa kwenda kilatini, kiCoptic na kiSyriac wazibadilishe zote ziendane na uongo waliyoandika kwenye zile za Kigiriki.
iii) Tatu njama ya maoni ya wazee wa kanisa (early church fathers) - wazee wa kanisa wa karne za kwanza walikuwa na utamaduni wa kuandika maoni/uchambuzi kuhusu biblia.
Tukisema tutupe biblia zote, tunaweza kuunda asilimia 95 ya agano jipya kwa kutumia maandishi ya wazee wa kanisa tu! Kwahiyo wanaotaka kubadilisha biblia ingebidi pia wapitie barua zote za wazee wa kanisa wabadalishe iendane na uongo walioandika kwenye Kigiriki na kilatini, kiCoptic na kiSyriac.
Kusema kuwa Biblia imebadilishwa ndio Conspiracy Theory kubwa kuliko zote kwenye karne yetu (ikifuatiwa na Evolution)
View attachment 3555590
d) Bila kusahau kopi tulizonazo za Injili zinakaribiana umri na nakala halisi, mfano tuna kopi za miaka 100AD.
Linganisha na nakala zingine za kihistoria, mfano za mwanahistoria Josephus ambaye kopi yake ya zamani kabisa tuliyonayo ni ya miaka 1000 baada ya Josephus! ! !
Au za Julius Caesar na vita zake kopi tuliyonayo ya zamani kabisa kumhusu ni ya miaka 900 baada ya Caesar mwenyewe! ! !
Au Aristotle, kopi yake ni ya miaka 1400 baaya ya Aristotle! ! !
View attachment 3555709
e) Je tunaweza kujua wakati ambapo nakala ya kwanza kabisa iliandikwa?
Kwa mfano, kitabu cha Matendo kilichoandikwa na Luka kinaongelea utabiri wa kuharibiwa kwa Yerusalemu (Matendo 6:14). So tunaweza kuhitimisha kuwa kiliandikwa kabla ya 70AD.
Kwenye kitabu cha Luka, Luka anasimulia jinsi Yesu alivyotabiri kuwa Yerusalemu itakuja kuharibiwa.
Hakuna kitabu chochote kwenye agano jipya kilichosimulia tukio la kuharibiwa kwa Yerusalemu, zaidi ya kutoa unabii kuhusu kuharibiwa kwa Yerusalemu (70AD)!
Unakuta mtu badala ya mtu kuhitimisha kuwa Yesu anaweza kutabiri kwa usahihi, mtu anasema hivyo vitabu viliandikwa baada ya tukio kwasababu haiwezekani kutabiri! ! !
Kwahiyo mtu ameshaamua akilini kwake miujiza haiwezekani kwahiyo akiona simulizi la utabiri uliokuja kutimia maana yake liliandikwa baada ya tukio! Hapo tayari umeleta ubaguzi (bias) kwenye kupima umri wa hizi nakala za kihistoria.
Kingine, wakati vitabu vya Matendo na Luka vinaandikwa bado kina Paulo, Petro, Yakobo walikuwa hai (miaka ya vifo vyao unajulikana), wakati vifo vya wafuasi wengine wa Yesu kama Stephano na Yakobo kaka ya Yohana vinatajwa.
Inawezekana mtu aandike historia ya Tanzania ya miaka ya 90 asitaje kifo cha Nyerere?
View attachment 3555585
View attachment 3555710
f) Sasa tutajuaje kuwa nakala hizi za agano jipya zilizonakiliwa vizazi baada ya vizazi hazijabadilika?
Tutafuata mlolongo wa ulinzi (chain of custody).
Kwa mfano, aliyeandika kitabu cha Yohana, alimpa nani hiyo nakala?
Tunawajua baadhi ya wanafunzi wa Mtume Yohana: Ignatius, Polycarp, Papius.
Hawa wanafunzi nao wana wanafunzi wao wanajulikana.
So tunaangalia kwenye huu mlolongo wa wanafunzi, Je simulizi kumhusu Yesu linabadilika? Je Yesu alianza kama mtu wa kawaida kadri muda ulivyoenda akageuka kuwa Mungu mtu?
Hapana! Tangu kitabu cha Yohana hadi barua za wanafunzi wake (wazee wa kanisa) na wanafunzi wao, simulizi ni lilelile: Yesu alizaliwa na bikra, alifanya miujiza, alikufa, akafufuka! ! !
Kitabu kama 1 Wakorintho kinakadiriwa kuwa cha miaka ya 50AD, na kinaongelea Ufufuo wa Yesu (1 Wakorintho 15). So Ufufuo wa Yesu ni habari iliyokuwepo tangu karne ya kwanza, haikutungwa baada ya miaka kupita!
View attachment 3555654
Hata kuhusu vitabu vilivyokuja kurasimishwa kwenye Baraza la Laodicea (363AD), ndo hivyo hivyo vilivyokuwa vinanakiliwa kwenye barua za wazee wa kanisa tangu karne ya kwanza, na vilikuwa vinaitwa hivyo hivyo vinavyoitw - Injili ya Luka, ya Mathayo n.k.
Baraza halikuja kuamua lolote jipya kuhusu vitabu zaidi ya kukataa vitabu vilivyokuja kuibuka baadae ambavyo wazee wa kanisa hawakuvitambua!
View attachment 3555712
g) Kingine cha kutujuza kuwa nakala hazijabadilika ni uwepo wa mamia na maelfu ya nakala za awali kabisa za agano jipya kwa visehemu au nzima nzima, kwa lugha zaidi ya nne tofauti.
Zingekuwepo kopi mbili tu kungekuwa na utata. Lakini ni maelfu ya nakala tena kwa lugha nne tofauti! !
View attachment 3555582
h) Utasikia "kitabu cha Mathayo hakijasema kimeandikwa na Mathayo kwa hiyo hatujui nani kakiandika na hakiaminiki".
Unajua ni historia kiasi gani itabidi tuitupilie mbali tukitumia hii hoja?
Hakukuwa na utamaduni wa mtu kuandika jina lake kwenye makala zake.
Tumeona hapo juu (f), uhalali wa waandishi wa nakala hizi tunaupata kupitia mlolongo wa umiliki (chain of custody).
i) Vipi kuhusu zinazodaiwa kuwa ni utata (contradictions) zinazoonekana kwenye zile Injili nne?
Kwanza contradiction maana yake haziwezi kupatanishwa. Kilichopo kwenye Injili ni tofauti (variation) sio contradiction.
Kwa mfano, kwenye ukoo wa Yesu, Mathayo 1:16 inasema baba ya Yosefu ni Yakobo huku Luka 3:23 inasema baba ya Yosefu ni Heli. Mtu anakimbilia kusema ni contradiction.
Lakini Mathayo kafuata ukoo wa Yesu kupia Solomon Mwana wa Daudi (Mathayo 1:6),
huku Luka akifwata ukoo kupitia Nathani mwana wa Daudi (Luka 3:31)!
Njia mbili tunazoweza kupatanisha kisa hiki:
a) Mathayo anafuata ukoo wa Yesu kupitia Yosefu baba yake mlezi huku Luka akifwata ukoo kupitia Maria mama yake.
Ndomana Luka anasema "...na watu walidhani yeye ni mtoto wa Yosefu mwana wa Heli...." (Luka 3:23 BHN).
Yosefu anakuwa mwana Heli kupitia ndoa yake na Maria, hivyo Yesu anakuwa mwana wa Daudi kupitia Maria kisheria.
b) Au kupitia ile Sheria ya kurithi mke (levirate marriage), kwamba Heli na Yakobo walikuwa Ndugu, kisha Heli alikufa bila mwana kwahiyo Yakobo akamuoa mjane wake akamzaa Yosefu, kwahiyo Yosefu alikuwa mwana wa Heli kisheria.
Unaweza kutafiti zaidi.
Je maelezo haya hayapatanishi Injili hizo?
View attachment 3555581
Mfano mwingine, kulikuwa na malaika mmoja au wawili kwenye kaburi la Yesu?
Mathayo 28 na Marko 16 inasema mmoja. Luka 24 na Yohana 20 inasema wawili.
Mpelelezi J.W.W anakwambia hajawahi kusikia mashahidi wawili wa tukio wakikubaliana kila kitu.
Kwanza chochote atakachojibu shahidi kinategemea swali ulilomuuliza, ndomana anaweza asitaje jambo muhimu sana kwenye kesi, ukija kuumuliza kulihusu anakwambia hukuniuliza!
Na ndo anachoona kwenye kisa hiki cha malaika kwenye kaburi la Yesu. Waandishi wanaonekana kujibu maswali tofauti.
Mathayo na Marko hawajasema kulikuwa na malaika mmoja tu! Lakini Yohana na Luka wanasema waliwepo wawili.
Sasa kama kuna wawili si kuna mmoja! ! Hakijaharibika kitu.
Ili kuwe na contradiction, Mathayo na Marko waseme alikuwepo mmoja tu.
Ukisoma vizuri utaona Mathayo na Marko walikazia issue ya tetemeko na jiwe la kaburi.
Mathayo anaonekana kujibu swali "Ni nini kilisababisha tetemeko"?
Marko anaonekana kujibu swali "ni nani aliondoa jiwe kwenye kaburi"?
Luka anaonekana kukazia fikra kupotea kwa mwili kwenye kaburi.
Yohana yeye alikazia fikra ripoti ambayo wanawake hao walienda kutoa.
J.W.W anasema anavyoona jinsi ambavyo waandishi wa Injili hizi hawakujihangaisha kulinganisha masimulizi yao Ili yafanane, ni uthibitisho kuwa masimulizi haya ni ya kutegemeka.
Hata yangefanana neno kwa neno, wazushi wangekataa pia! Wangesema hawa watu wametunga.
View attachment 3555580
4) Masimulizi kwenye agano jipya (na la kale) ni yenye kutegemeka kihistoria.
Kuna taarifa nyingi za zisizo za kikristo za kihistoria kwenye biblia. Yani kama utamsoma Josephus (36-100AD) ukamwamini na usijiulize mara mbili kama yuko sahihi au la, basi hata Injili unaweza kusoma bila kujiuliza.
Ukikuta tofauti kwenye taarifa fulani ya kihistoria (mfano issue ya sensa ya Quirinus wakati Yesu alipozaliwa) sio unampuuza Luka na kumsikiliza Josephus, maandishi ya Josephus hayana mamlaka yoyote zaidi ya Luka.
Kwanza Injili inakuwa na mamlaka zaidi kwakuwa yalionekana kuwa maandiko yenye thamani kubwa kwahiyo yalilindwa sana, yalitunzwa, yalisambazwa na kutafsiriwa!
Tofauti na maandishi ya wanahistoria kama Josephus ambaye hakuwa na watu waliofuatilia na kulinda maandishi yake! ! Kama kuna uongo amesema hakuna wa kumpinga!
Daktari Luka anasema: "....Watu wengi wamejitahidi kuandika juu ya mambo yale yaliyotendeka kati yetu. Waliyaandika kama tulivyoelezwa na wale walioyaona mambo hayo kwa macho yao tangu mwanzo, na waliotangaza ujumbe huo. Inafaa nami pia, Mheshimiwa, baada ya kuchunguza kwa makini mambo yote tangu mwanzo, nikuandikie kwa mpango, ili nawe uweze kujionea mwenyewe ukweli wa mambo yale uliyofundishwa." (Luka 1:1-4 BHN)
Mtume Petro naye anasema: "Wakati tulipowafundisheni juu ya ukuu wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, hatukutegemea hadithi tupu zisizo na msingi. Sisi tuliuona utukufu wake kwa macho yetu wenyewe." (2 Petro 1:16 BHN)
Mtume Paulo anasema: "....alizikwa, akafufuka siku ya tatu kufuatana na Maandiko Matakatifu; kwamba alimtokea Kefa, na baadaye aliwatokea wale kumi na wawili. Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya 500 kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa." (1 Wakorintho 15:4-6 BHN)
Biblia ni nyaraka zenye kutegemeka kabisa za historia.
Sio hekaya au hadithi!
Biblia sio Gilgamesh epic!
Biblia iliandikwa na mashahidi wa matukio halisi ya historia, wakishuhudiwa na mashahidi wenzao wa hayo matukio.
View attachment 3555579
5) Bila kusahau kuenea kwa ukristo karne za kwanza kulihusisha mateso makali sana kwa wakristo.
Walichohitaji ni kumkana Yesu halafu waepuke kifo waendelee na maisha yao,
lakini mamia na maelfu walikubali kuuawa: walisulubiwa, walipigwa mawe hadi kufa, walichomwa moto wakiwa hai, walitupwa waliwe na wanyama!
Kuna faida waliyokuwa wanapata kwa kushikilia hiyo Imani?
Pesa? Mamlaka? Wanawake?
Zaidi ya mateso na kudharaulika!
Au wote walikuwa wanaota?
Ni nini kilichowasukuma?
Na kuna tofauti ya mtu kukufuata kukuua kwasababu ya imani yako, na mtu aneyeenda kujitoa kafara kwasababu ya imank yake.
View attachment 3555562
View attachment 3555578
6) Tuna uthibitisho wa kutosha kabisa wa kukubali masimulizi ya Yesu bila shaka yoyote (beyond reasonable doubt).
Haiwezekani kuwa na uthibitisho bila shaka kabisa (beyond possible doubt).
Hiyo itahitaji kujua KILA KITU na haiwezekani kujua kila kitu.
Hakuna anayeishi maisha kwa kiwango hicho cha bila shaka kabisa maana hata nyumbani tusingetoka hadi mtu uwe na uhakika bila shaka kabisa kwamba hutogongwa na gari kesho, hutopigwa na radi, hutotekwa n.k.
Hata hukumu za wahalifu wabaya kuliko wote wanaohitaji kunyongwa hazihitaji uthibitisho bila shaka kabisa.
Nafasi ndogo iliyobaki kati ya uthibitisho bila shaka yoyote na uthibitisho bila shaka kabisa ndo nafasi ya maswali yako yasiyokuwa na majibu.
Ni nafasi ya wewe kuchukua hatua moja tu, ya IMANI.
Sio Imani kipofu: ni Imani yenye uthibitisho usio na shaka yoyote!
Kuwa na TUMAINI sio kuwa na matamanio ya kufikirika.
Ni kuwa na uhakika wa mambo unayoyatarajia kutokana uthibitisho usio na shaka uliopata.
"Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu? Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye."
Yohana.6.28-29.SRUV
"Basi, pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Kwa maana kila mtu anayemwendea Mungu ni lazima aamini kwamba Mungu yuko, na kwamba huwatuza wale wanaomtafuta."
Waebrania.11.6.BHN
"Pimeni kila kitu: Zingatieni kilicho chema."
1Wathesalonike.5.21.BHN
View attachment 3555561
Leta uthibitisho na ushahidi sio stori za mitaani.Sema hujawahi kulishuhudia. Usiseme haliwezekani
Jifunze, soma vitabu, utaujua ukweli.Blind acceptance hii
JINSI YESU ALIVYOKUFA(not debating, just leaving this here for Genuine Truth Seekers)